macho_mdiliko
Platinum Member
- Mar 10, 2008
- 29,500
- 61,451
Hapana. Kipindi Nyerere anaongoza hali ya siasa duniani kote ilikuwa ni tofauti kabisa na sasa. Ukifananisha Nyerere na marais wengine wa kipindi hicho, Nyerere alikuwa rais bora kabisa. Hakuwa anaua watu na alikuwa na vision. Alipokuwa anaondoka alitoa tahadhari kuhusu katiba na mfomo mzima wa utawala na pia alisema vyama vingi haviepukiki. Haya yanayotokea sasa ni matokeo ya uzembe wetu wenyewe kushindwa kubadili katiba. Na Magufuli ndiye shetani hasa kwa sababu bunge bovu, mauaji na uporaji wa kura kwa kiwango unaofanywa sasa hivi yeye ndiye alianzisha.Ukiwa na akili timamu unaelewa chanzo cha haya ni nyerere aliye asisi mfumo wa chama kimoja na ujamaa uchwara, huku akipinga na kuwashughulikia watu wote wenye mawazo mbadala kama kambona, bibi titi, jumbe nk.
Yeye ndio alitengeneza mfumo wa mwenyekiti wa CCM na raisi kuwa Mungu mtu.
Walio fuata ni wanufaika wa huo mfumo ovu ambao wanautumia wanavyo penda na kujisikia.
Marehemu ni lazima alaumiwe kwa sababu yeye ndiye genesis ya haya yote. Hili bunge la sasa ni matokeo yake. Dola kupora kura ili CCM isipate upinzani ni matokeo ya huyo shetani Magufuli.Binadamu Bwana. Anayekuumiza yuko hai huna cha kumfanya unaishia kumlaumu Marehemu
Haya kafukue mifupa yake uichape.Marehemu ni lazima alaumiwe kwa sababu yeye ndiye genesis ya haya yote. Hili bunge la sasa ni matokeo yake. Dola kupora kura ili CCM isipate upinzani ni matokeo ya huyo shetani Magufuli.
ExactlyUkiwa na akili timamu unaelewa chanzo cha haya ni nyerere aliye asisi mfumo wa chama kimoja na ujamaa uchwara, huku akipinga na kuwashughulikia watu wote wenye mawazo mbadala kama kambona, bibi titi, jumbe nk.
Yeye ndio alitengeneza mfumo wa mwenyekiti wa CCM na raisi kuwa Mungu mtu.
Walio fuata ni wanufaika wa huo mfumo ovu ambao wanautumia wanavyo penda na kujisikia.
Amesingiziwa mengi...! Mnaumbuka Sasa.....jiwe....
Tunaposema mabaya ya marehemu yoyote nia yetu siyo kumwadhibu bali ni kujifunza ili yasitokee tena.Haya kafukue mifupa yake uichape.
hapana wengine ni wawivu tukianza na sisi tunaobishana mtandaoni bdala ya kwenda kufanya kaziTatizo la Africa sio kwamba watu wake hawafanyi kazi, raia wa Africa wanafanya kazi kuliko hata punda.
acha useng*Tutaongea yote ila jiwe ndiye chanzo cha haya yote na ndiye aliyetufikisha hapa tulipo leo. Jini akishatoroka kwenye chupa ni vigumu sana kumrudisha, ni rahisi sana kuboma kuliko kujenga.
Kwa mema yote na kwa mabaya yote akumbukwe.
Sasa yupo wapi!?Ukiwa na akili timamu unaelewa chanzo cha haya ni nyerere aliye asisi mfumo wa chama kimoja na ujamaa uchwara, huku akipinga na kuwashughulikia watu wote wenye mawazo mbadala kama kambona, bibi titi, jumbe nk.
Yeye ndio alitengeneza mfumo wa mwenyekiti wa CCM na raisi kuwa Mungu mtu.
Walio fuata ni wanufaika wa huo mfumo ovu ambao wanautumia wanavyo penda na kujisikia.
Nakubaliana na wewe kwa asilimia mia. Tunapokumbuka mazuri yake lazima tukumbuke na mabaya yake. Pia tuwakumbuke na wale waliotumia udhaifu huo kama upenyo wa kupitia ili kututenda maovu haya wanayotutendea watanganyikaTutaongea yote ila jiwe ndiye chanzo cha haya yote na ndiye aliyetufikisha hapa tulipo leo. Jini akishatoroka kwenye chupa ni vigumu sana kumrudisha, ni rahisi sana kuboma kuliko kujenga.
Kwa mema yote na kwa mabaya yote akumbukwe.
Ndio upumbavu wetu, labda tunasubiri huyo aliyeharibu afufuke aje aturekebishie. Very hopeless.Binadamu Bwana. Anayekuumiza yuko hai huna cha kumfanya unaishia kumlaumu Marehemu
Mkuu nakushauri fikiri tena kwa kina hilo neno kuhusu "uzembe wetu wenyewe kushindwa kubadili katiba". Na sisi ni kina nani? Tuko pamoja katika hili?Hapana. Kipindi Nyerere anaongoza hali ya siasa duniani kote ilikuwa ni tofauti kabisa na sasa. Ukifananisha Nyerere na marais wengine wa kipindi hicho, Nyerere alikuwa rais bora kabisa. Hakuwa anaua watu na alikuwa na vision. Alipokuwa anaondoka alitoa tahadhari kuhusu katiba na mfomo mzima wa utawala na pia alisema vyama vingi haviepukiki. Haya yanayotokea sasa ni matokeo ya uzembe wetu wenyewe kushindwa kubadili katiba. Na Magufuli ndiye shetani hasa kwa sababu bunge bovu, mauaji na uporaji wa kura kwa kiwango unaofanywa sasa hivi yeye ndiye alianzisha.
Wewe unadhani kwamba huu uuwaji na utekaji ni issue aliyohusika nayo Magufuli na sasa Samia?Mkuu Nyerere hakuteka na kuua kama Jiwe na Samia
Mwinyi na Mkapa walikua wana “shughulikia” kwa kukufungia mirija
Jk aliteka kidogo
Jiwe na mama wanakupoteza mazimaaaa
Kama hatuwezi kurekebisha sasa huko kujifunza kutasaidia nini? Ndio maana hadi leo bado tunalaumu makosa ya Nyerere ambayo hatujaweza kurekebisha halafu mkuu unataka tujifunze kupitia makosa ya Magufuli.Tunaposema mabaya ya marehemu yoyote nia yetu siyo kumwadhibu bali ni kujifunza ili yasitokee tena.
Upo sahihiTutaongea yote ila jiwe ndiye chanzo cha haya yote na ndiye aliyetufikisha hapa tulipo leo. Jini akishatoroka kwenye chupa ni vigumu sana kumrudisha, ni rahisi sana kuboma kuliko kujenga.
Kwa mema yote na kwa mabaya yote akumbukwe.
Hatuwezi kurekebisha lakini tunajifunza ili tusiyarudie. Nikupe mfano: Ndege inapopata ajali, kunakuwa na repoti ya kina kuhusu ni nini kilijiri. Japokuwa hatuwezi kurekebisha (kurudisha) uhai na mali zilizopotea, lakini tunajifunza ili makosa kama yale yasitokee tena.Kama hatuwezi kurekebisha sasa huko kujifunza kutasaidia nini? Ndio maana hadi leo bado tunalaumu makosa ya Nyerere ambayo hatujaweza kurekebisha halafu mkuu unataka tujifunze kupitia makosa ya Magufuli.
Wa kulaumiwa ni sisi wananchi. Na hii ni kwa sababu tuna mawazo kama yako i.e. kudhani kuwa watawala watatuonea huruma na kuja na katiba nzuri bila sisi kuidai. Kwa hili tutasubiri sana. CCM jana wamesema ilani yao ina kipengele cha katiba mpya. Watch out! Itakuja katiba mbovu kuliko hii. Hii ni kwa sababu sisi wananchi tumekaa na kudhani kuwa watawala wataleta wenyewe. Kipindi cha Nyerere, katiba za nchi nyingi hasa Afrika zilikuwa siyo nzuri. Wananchi tuungane tudai na siyo kusubiri.Mkuu nakushauri fikiri tena kwa kina hilo neno kuhusu "uzembe wetu wenyewe kushindwa kubadili katiba". Na sisi ni kina nani? Tuko pamoja katika hili?
Kwa taarifa yako tangu enzi za Nyerere wamekuwepo Watanzania majasiri wanaojaribu kugusa eneo la Katiba kwa namna mbalimbali lakini mwisho wao haukuwa mwema. Katiba kwa kundi la watawala ndani ya chama tawala, ni eneo tukufu lilisogusika kabisa (sacred text). It is untouchable. Touch at your own peril. Hakuna ambaye angeweza wala anayeweza kufanikisha marekebisho ya msingi ya katiba ya nchi hii bila kusababisha machafuko na maafa makubwa nchini. Awamu zote. Hadi leo Watanzania hawako tayari kwa mapambano hayo na vyombo vya dola.
Kila kukicha AMANI inasisitizwa, inahubiriwa, inaombewa kitaifa kwenye nyumba za ibada. Wapinzani wanasoteshwa kwa kutishia amani ya taifa kwa kushirikiana na mabeberu. Wanatekwa, wanatiwa ulemavu, wanauawa, wanapotezwa. Kina Lissu wako ndani. Wenzao wengine wananunuliwa kila kukicha. Sijui kama kweli, kwa kadhia hizi, bado ni "uzembe wetu wenyewe" kushindwa kubadili katiba.
Nyerere ndiye aliyekuwa na nguvu ya kipekee, uelewa mkubwa na ujasiri wa kipekee wa kuitisha na kusimamia hayo marekebisho yanayotakiwa mara tulipoanza mfumo wa vyama vingi. Kama vile alivyofunga mjadala wa ama kuingia vyama vingi au kubaki na chama kimoja pamoja na wengi (80%) kutaka chama kimoja. Alipoacha status quo, waliopokea madaraka walikuwa kama mafisi walioachiwa bucha nzima milango yote ikiwa wazi. Si rahisi wakakubali ifungwe. Ni mwendo wa kurithishana tu.
Btw, katiba zote za taifa hadi ya 1977 na marekebisho ya 1984 (yaliyoingiza haki za binadamu) wakati anang'atuka ziliandikwa na Nyerere mwenyewe kwa msaada wa vijana wake kina Warioba na wengineo. Na alijua vizuri sana hatari ya hiyo katiba (tuliyo nayo hadi leo). Lakini naona hakuwa na ujasiri wa kushuhudia CCM ikiondolewa madarakani akiwa hai. Kuuawa kwa Azimio la Arusha na tishio la Muungano kuuawa na wale G55 vilimkosesha raha sana.
Muungwana Kikwete alijaribu kuachia mwanya kidogo tu akatishiwa kuondolewa madarakani akituhumiwa kutaka chama kimfie mikononi. Unaelewa msimamo wa Magufuli na wa utawala wa sasa. Not an easy task at all.