Katika yote hatupaswi kusahau aliyetufikisha hapa tulipo sasa

Na wakati anang'atuka alikiri wazi kuwa katiba ni mbovu. Kwa kipindi hicho angeweza kuweka katiba bora pasipo kizuizi ndani ya Chama. Tunayoyaona sasa ni matokeo ya uzalendo kwa Chama kuwa juu ya uzalendo kwa nchi - kitu alichoasisi yule mzee.
Kabisa, alikuwa na nafasi ya kurekebisha hayo ya Katiba ila hakufanya hayo Ili kukilinda chama chake alichokiasisi.

Anyway kazi ipo kwetu raia kupambana kupata Katiba tunayoitaka.
 
Nyerere na Kawawa hawakuendeleza mabaya ya mkoloni.
Aliyefuata baada ya huyo umsemae anaweza kuchagua njia tofauti na mtangulizi wake.
No excuses!
Hawakurekebisha pia sehemu kubwa ya mfumo wa kikoloni wenye kuwezesha mabaya kutendeka na walijenga mfumo mwingine wa kumfanya mtu mmoja kuwa mungu mtu.
 
Tutaongea yote ila jiwe ndiye chanzo cha haya yote na ndiye aliyetufikisha hapa tulipo leo. Jini akishatoroka kwenye chupa ni vigumu sana kumrudisha, ni rahisi sana kuboma kuliko kujenga.

Kwa mema yote na kwa mabaya yote akumbukwe.
Sio Gen Mabeyo?
 
Magufuli kiasili alikuwa sio politician Ila the guy was a leader .

Ukiwa na kariba ya uongozi unaweza usiwe mwanasiasa mzuri Sana .

So siasa chafu zilianza mwaka 2017 Ccm baada ya kumleta Bashiru Ally Kakurwa.

Magufuli , he was not organizer wa haya mambo ya kuharibu uchaguzi Ila Pole Pole na Bashiru Ally kakurwa ndo walikuwa waratibu wa hayo mambo .

Being a leader and being a politician ni tofauti .

Japo wapo ambao ni wanasiasa wazuri na viongozi wazuri

Ila ukiangalia Sisiemu asilimia kubwa kuna wanasiasa amabao hawana sifa za kiuongozi
 
Umeongea ukweli wa chanzo
 
Mkuu Nyerere hakuteka na kuua kama Jiwe na Samia

Mwinyi na Mkapa walikua wana “shughulikia” kwa kukufungia mirija
Jk aliteka kidogo
Jiwe na mama wanakupoteza mazimaaaa
Ila maza kazidi,afu aibu hana wala
 
Wewe unadhani kwamba huu uuwaji na utekaji ni issue aliyohusika nayo Magufuli na sasa Samia?
Alivyokufa Magufuli basi Membe alikuwa wa kwanza kusema kuwa hakutakuwa tena na mauwaji.
Collective responsibility
 
Kama ni hivyo basi sasa tusingekuwa tuko hapa bado tunamlaumu Magufuli bali tungekuwa tushajifunza ila tunaendelea kupitia yaleyale tuliyopitia wakati wa Magufuli, na badala ya kupambana na hali iliyopo sie tunarudi kumlaumu Magufuli sasa sijui hizi lawama kwa Magufuli zitasaidia nini na kuisha lini ikiwa hatuna nia ya kukomesha hayo makosa?

Ataondoka Samia atakuja mwengine na mwengine ila sisi bado tutabaki na lawama kwa Magufuli, hii inaonyesha sie wenyewe ni sehemu ya tatizo.
 
Tutaongea yote ila jiwe ndiye chanzo cha haya yote na ndiye aliyetufikisha hapa tulipo leo. Jini akishatoroka kwenye chupa ni vigumu sana kumrudisha, ni rahisi sana kuboma kuliko kujenga.

Kwa mema yote na kwa mabaya yote akumbukwe.
Huwezi endelea kulaumu mtu aliyekufa wakati una nafasi ya kurekebisha makosa yake. Huu ni mtindio wa ubongo.
 
Yafuatayo Ndio mambo yalioanza kwa jiwe.

1.Kusifia bila kuhoji
2..Bunge Kuwa kabisa chini ya serikari
3.Wasiojulikana
4.kuuwawa kwa wapinzani.
Yameanza kwa Jiwe au hayo mambo yamekuwepo toka muda na wakati wa Jiwe ilikuwa ni muendelezo tu? Ndio maana hata sasa watu wanamuona Samia ni katili kuliko huyo Jiwe.
 
“Marehemu asemwi vibaya” ni mmoja wa usemi wa KISHENZI sana

Yaani hapa Jf hata ufungue nyuzi milioni moja za kusifia MUENDELEZO wa mambo mazuri ya Jiwe yanavyoendelezwa huta ona ngonjera kama hizi

Lakini ukifungua tu nyuzi kuhusu MUENDELEZO wa mambo mabaya ya jiwe watatoka walikotoka wafuasi wa jiwe na kuja na ngonjera za ajabu ajabu sana

Hadi leo tunaimba Nyerere alituletea UMOJA licha makabila yetu mengi

Huwezi kufuta HISTORIA kwasababu unaumizwa na historia hiyo kwa mahaba ya anayesemwa...... get used to it

Jiwe katuharibia sana nchi hii.... HII HATUTASAHAU
 
Huwezi endelea kulaumu mtu aliyekufa wakati una nafasi ya kurekebisha makosa yake. Huu ni mtindio wa ubongo.
Hawa ndio badala ya kupambana na maisha wao wanalaumu kuzaliwa familia masikini.
 
Huwezi endelea kulaumu mtu aliyekufa wakati una nafasi ya kurekebisha makosa yake. Huu ni mtindio wa ubongo.
Tunajaribu kurekebisha lakini still bado watu wanapotezwa wakijaribu kwasababu ya misingi thabiti ya kikatili aliyoweka Jiwe

Huwezi kuujua uchungu na hasira kwa ujinga aliouleta jiwe kama una faidika na ujinga huu au kama akili yako ni finyu kujua ubaya wa haya

Hata siku ujinga huu ukiisha Jiwe ataendelea kuwa reference forever
 
Hilo sio tatizo la aliyeanzisha bali anayeendeleza.
 
Wala hujaambiwa usahau au usieleze hayo mabaya ya Jiwe ila kinachosemwa hapa ni kwamba kushindwa kurekebisha hayo makosa ya Jiwe na kufanyika yenye kuonekana ni sahihi kwa wakati uliyopo badala yake tunabaki kuendelea kumlaumu tu huyo Jiwe, huo ndio ujinga tunaosema hapa.

Kama hatuna nia ya kurekebisha makosa yaliyoanzishwa wakati wa Jiwe sasa huku kuendelea kumlaumu huyo Jiwe kunasaidia nini? Maana hakuna tunachojifunza zaidi ya kuonyesha tu kwamba Jiwe alikuwa mtu mbaya basi ambalo ni suala la kihisia zaidi tu. Ataondoka Samia watakuja wengine ila bado tutaendelea na kumlaumu Jiwe.

Sasa kuna upumbavu zaidi ya huo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…