Pre GE2025 Katikati ya matangazo ya 'Live' ITV Mgeni aomba watu wote studio wasimame kumuombea Rais Samia, Watangazaji wapata kigugumizi kumzuia

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Siku ya ya jana tarehe 13 Machi 2025 ITV walikuwa wakirusha matangazo mbashara kipindi cha malumbano ya hoja mada ikiwa 'kutofanyika kwa dabi ya Simba na Yanga nini kifanyike?'.

Wakati kipindi kinaendelea akakaribishwa mchangiaji mmoja akijulikana kwa jina la Ramadhan Kampira, Mwenyekiti wa wachezaji wa zamani wa Yanga ambaye kabla hajaanza kuzungumza akawaomba watangazaji na wachangiaji wengine wasimame kwa dakika 1 kumuombea Rais Samia.

Niliona watangazaji wakabaki kwenye Dilema na baadae wakaamua kusimama, katikati ya maombi mtangzaji mmoja akashindwa kujizuia akatoa kicheko.

Kujipendekeza, uchawa vimetamalaki kila kona mpaka vinakua sugu.

Pia soma: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Your browser is not able to display this video.
 
Chawa everywhere
 
Kazi kweli
 
Siku hizi.kuna.malumbano ya hoja kuhusu.simba na yanga ? Aha ha ha aha
 
Siku hizi.kuna.malumbano ya hoja kuhusu.simba na yanga ? Aha ha ha aha
 
Hivi vichekesho vingine viuzwe kimataifa, labda vitasaidia kuongeza pato la taifa.
 
Awamu hii uchawa umerasimishwa kabisa.
 
Jana wanangu wanaosoma darasa la saba waliniuliza, hivi si ndio wanawafanyia waliokufa?
Kwani wanayemfanyia amekufa !!
Sikujibu neno maana nami nilipigwa na butwaa.
 
Sasa hawataki Rais aombewe ili ashindwe kutimiza majukumu yake? Wakamate wote sukuma ndani. Rais ni wa kuombewe kila siku kama dozi ya dawa full stop na wote semeni amina,
 
Huyu ni Mpumbavu na ameipatia aibu familia yake! Mke wake na watoto wake πŸ˜” hata kama ni uchawa ila kuna kiwango! Hapo bado kidogo angesema Mungu Samia πŸ˜” Kuwa na Mshua wa namna hii ni heri uwe yatma tu! Mungu atakuelewa! πŸ˜” wazee wanazeeka ila pia na wapumbavu wanazeeka!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…