Uchaguzi 2020 Kauli hii ya Magufuli ya kuongezewa miaka 5 inaashiria kakata tamaa?

Uchaguzi 2020 Kauli hii ya Magufuli ya kuongezewa miaka 5 inaashiria kakata tamaa?

Kama huyu wala hatuna huruma nae maaana alishasahau kuwa amekaa hapo kwa sababu na kwa ajili wananchi
Alijiaminisha kuwa ikifika 2020 uchaguzi atauweka mfukoni hivyo hatahitaji kura za watu ila sasa akili imemkaa sawa.

Kile kiburi na jeuri aliyokuwa nayo, usingeamini kama atakuwa 'mdogo' hivi leo, na Lissu atamnyoosha kweli kweli.
 
Mbona kwa baba wa Taifa hakumuombea alale mahala pema.pia kamuombea Mkapa tu!
Anajifananisha na watangulizi wake ambao hamna hata mmoja wao walipotawala wapinzani walipigwa malisasi!! Ni katika utawala wake mpinzani wake alipigwa risasi 16 na akapona na waliohusika hawajakamatwa mpaka hivi sasa. Utawala wake mbovu ni sababu tosha ya kumtosa!!
 
Hivi Magufuli anshindwa nini kubadilisha gia angani akaja na hoja ya kujenga miundombinu ya umwagiliaji kwa wananchi, maji kwa wote, umeme kila kitongoji, masoko ya mazao na viwanda vya kusindika mazao, nyasi za bandia viwanja vyote vya michezo kila mkoa, trecta kila Kijiji? Naona Bado kakomaa na kuongeza ndege.
 
“Baba wa Taifa Mwl.Nyerere mlimpa miaka 27, akaja Mwinyi mkampa miaka 10, akaja Mzee Mkapa (Mungu amlaze mahali pema) mkampa miaka 10, amekuja Kikwete mkampa miaka 10, Mimi nina dhambi gani mnataka mnipe miaka 5 tu!?, nawaomba nipeni miaka mingine 5 zaidi”-JPM

Acha sigara kali,itakuangamiza
 
Back
Top Bottom