Uchaguzi 2020 Kauli hii ya Magufuli ya kuongezewa miaka 5 inaashiria kakata tamaa?

Uchaguzi 2020 Kauli hii ya Magufuli ya kuongezewa miaka 5 inaashiria kakata tamaa?

Hizo ndege zitatua maswa,SGR itapita Mwanza kuelekea Isaka,yaani inaenda kinyume nyume
 
Lisu mpaka tukamfundisha cha kuongea

Mwanzo ilikuwa habari ya risasi tum

Tukamwambia waambie watu utafanya nini sio habari za Risasi kutwa kucha

Ndio akabadilika
kilaza kama wewe utamfundisha nini Lissu aliyeshika bunge zima.
 
Ana miaka mingine mitano ya kuongoza taifa. Tunasubiri 28th October ifike tu, zingine ni lugha za kutafuta kura tu.
 
Nimemwona leo Bariadi nyumbani akiomba kura kwa huruma sana nadhani amegundua kitu kwamba unyenyekevu huzidi nguvu.
“Baba wa Taifa Mwl.Nyerere mlimpa miaka 27, akaja Mwinyi mkampa miaka 10, akaja Mzee Mkapa (Mungu amlaze mahali pema) mkampa miaka 10, amekuja Kikwete mkampa miaka 10, Mimi nina dhambi gani mnataka mnipe miaka 5 tu!?, nawaomba nipeni miaka mingine 5 zaidi”-JPM


Kauli ya kawaida sana kuomba kura kwa wananchi. Magufuli ni mnyenyekevu sana.
Hiyo kauli ina harufu ya woga na kukata tamaa. Ukishaanza kuhoji 'kwanini Mimi?' ujue kimbunga ni kikali unatamani kingewasomba waliotangulia siyo wewe.
Duu! Yaani CCM mpaka leo hamjamwambia mgombea wenu dhambi zake ni zipi? Pengine ndio maana hajaanza kuziungama kwa kutojua dhambi zake, Lakini pamoja na dhambi nyingine nyingi kubwa kuliko zote ni kujali na kuabudu maendeleo ya vitu visivyo hai huku akikandamiza na kupuuza vilivyo na uhai! Kupuuza maendeleo ya watu hapa lazima akubali gharama zake! Na asipoungama na kujirekebisha mauti yake kisiasa yako hapo! Hao wote aliowataja walijali maisha na maendeleo ya watu na sio vitu!
Magufuli ni kweli na muwazi pia ni msikivu sana kwa mambo ya msingi
Bora apumzike tumechoka ...ahaaaaaaaa bwana jpm kaa pembeni tumechoka
 
Copied from somewhere in Tanzania;

#1
SISI SIO WAJINGA
Ulipochukua tu madaraka ukaanza na kubomoa nyumba zetu katika bonde la Msimbazi. Bila huruma ukatuacha tumelala nje na watoto wetu. Ulidhani tutahama mjini lakini sisi bado tupo.

SISI SIO WAJINGA
Ulipokuwa unapanua barabara ya Ubungo - Kibaha ukabomoa nyumba zetu. Mbunge wetu Mnyika aliomba utulipe fidia ukampinga mbele yetu. Lengo lako tufe masikini lakini kwetu sisi maisha yanaendelea.

SISI SIO WAJINGA
Hukutaka tuwaone wawakirishi wetu, wakiwakirisha matatizo yetu Bungeni. Ulisema gharama za kurusha matangazo Live ni kubwa. Lakini leo hii unatuomba tufungue TBC tukuangalie ukikata mitaa kuomba kura.

SISI SIO WAJINGA
Baada ya kuwa tumefanya kazi kwa miaka 40 na tumebakiza miezi 3 tustaafu ukatufukuza kazi kwa kisingizio cha vyeti feki. Ulidhani tutakufa kwa njaa lakini Mungu anatupigani bado tunaishi.

SISI SIO WAJINGA
Tulipopata tetemeko la ardhi Watanzania wenzetu walituchangia pesa nyingi lakini wajanja wakatafuna. Ulipokuja Bukoba tulidhani utatutetea wanyonge badala yake ukatusimanga na kutukumbusha majanga ya Ukimwi, MV Bukoba kwamba yote yanatupiga sisi. Sasa nasikia unakuja kuomba kura kwetu! Je, ni kweli wewe utakanyaga Bukoba?

SISI SIO WAJINGA
Tulipokuwa tuna njaa. Njaa iliyotokana na ukame. Tukakuomba msahada wa chakula. Hii sio kwako tu, hata Serikali zilizopita zilitusaidia tulipokumbwa na ukame. Lakini ulitujibu kwa kejeli na kiburi cha hali ya juu. Eti tusikuombe chakula, Serikali haina shamba. Leo hii unakuja tena kuomba kura?

SISI SIO WAJINGA
Tukaenda Mtwara kulima korosho. Ukatuma askari wako wakatunyang'anya korosho halafu wakadai tuwaonyeshe mashamba yetu. Mbona wanaolima Mahindi, Pamba, Mpunga, n.k. hamuwaulizi mashamba yao? Ukasema hao askari watabangua korosho kwa meno ili kila Mtanzania atapata kilo 2, lakini hatujapata mgao. Sasa nasikia unakuja kuomba kura! Labda uishie Nangurukuru kwa sababu.

SISI SIO WAJINGA
Tumeitumikia nchi yetu kwa bidii kubwa. Tumefanya kazi kwa uzalendo mkubwa, huku tukipokea mishahara kidogo. Leo hii tumestaafu, tupo nyumbani miaka ikikatika. Lakini hutaki kutulipa mafao yetu. Bila aibu unakuja kutuomba kura tena?

#SISI_SIO_WAJINGA.

My take;
Watu wanahasira sana na huyu mzee, free and fair election kama itakuwepo basi akijipatia 30% ya kura zote basi akatambike.
Kama mnabisha mshaurini aitishe mkutano kavukavu kama hajajikuta na mabalozi wake wa nyumba kumi kumi
 
Wapinzani na wapingaji wajue jambo moja, hata Wamchukie Rais kwa kiwango gani lakini ndiye rais wa JMT kwa miaka 5 mingine

Kwa sababu Lissu hawezi kuongoza nchi hii, nchi sio familia msela yeyote anaweza kuongoza

Utaona mtu anabishabisha kwanza vikura vyenu ni maoni tu, asipofaa hapewi hata ashinde
 
Si mshamba, anaona kuwa na Yale madude ni ufahari
Hivi Magufuli anshindwa nini kubadilisha gia angani akaja na hoja ya kujenga miundombinu ya umwagiliaji kwa wananchi, maji kwa wote, umeme kila kitongoji, masoko ya mazao na viwanda vya kusindika mazao, nyasi za bandia viwanja vyote vya michezo kila mkoa, trecta kila Kijiji? Naona Bado kakomaa na kuongeza ndege.
 
Kashashindwa huyo Jiwe. Kaona reli, ndege, barabara, flyovers, havilipi.. Watanzania hawaelewi aisee, wako kwa Tundu Lissu. Tumemchokaaa Jiwe hatufai.
 
Back
Top Bottom