Uchaguzi 2020 Kauli hii ya Magufuli ya kuongezewa miaka 5 inaashiria kakata tamaa?

Ameshajua wananchi wengi wanaamini kwamba Rais akiingia hadi amalize muhula wa pili sasa anataka autumie ujinga wa watz wamchague tu awamu ya pili kisa wenze ilikuwa hivyo

Uoga umo
 
Anapenda kuona ndege tu
 
Mbona mzee wetu amekuwa mnyonge ghafla?

"Mimi nina dhambi gani mnataka mnipe miaka 5 tu!?"

Mzee wetu mimi siwezi kukuhukumu kwamba una dhambi, hilo ni jukumu la ALLAH siku tutakayo simama mbele ya utukufu wake, ila kuna baadhi ya mambo ambayo tunahitaji kuya fahamu kutoka kwako, ili tuone kama kweli unastahili tukupe miaka mingine mitano kama watangulizi wako. Baadhi ya mambo yenyewe ni haya:

Kauli yako kwa wakurugenzi kwamba wasiwatangaze wapinzani wa chama chako.
Kisheria tume ya uchaguzi ndio yenye mamlaka yakusimamia uchaguzi na kutangaza matokeo, kwa nini jukumu hilo lipewe wakurugenzi ambao si wajumbe/wafanyakazi wa tume ya taifa ya uchaguzi?
Kuna familia na watanzania kwa ujumla adi sasa wanalia kwa tungu zao kupotea katika mazingira tatanishi.
Kuna ndugu zetu ambao miili (maiti) yao iliokotwa kwenye viroba.
Kuna ndugu zetu ambao wamepata ulemavu wa kudumu.
Kuna malalamiko ya wafanya kazi kutoongezewa mishahara wala kupandishwa madaraja kwa miaka mitano.
Pamoja na serikali kuwa na mkono mrefu lakini adi sasa kuna kikundi cha watu wasiojulikana.
Ni sheria gani uliyoitumia kwa miaka mitano kuwazuia wengine wasifanye mikutano ya kisiasa lakini wewe ukaendelea kufanya mikutano peke yako?
Uhuru wa vyombo vya habari.
Uhuru wa watanzania kuihoji serikali yao waliyoiweka madarakani kwa kura zao.
Msongamano wa wahitimu wa vyuo kukosa ajira (tatizo la hajira kwa ujumla).

Haya ni baadhi ya mambo ambayo kama mzee wetu utatupa ufafanuzi mzuri, basi wala usiwe mnyonge miaka mingine mitano tutakupa tu.

Na kwa wale wanao kuombea basi huu ndio wakati wakuzidisha maombi kuliko wakati wowote.
 
Shughuli ipo!!
 
Huu ndio kukata tamaa,Magufuli anachanja mbuga nyinyi mnachana key boards #AIBUUUU!
 
Matumaini yetu pekee yamebaki kwa mabeyo & corona
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…