Kauli hii ya mke wangu ina maana gani?

Na wewe ungemjibu hivyo hivyo, halafu ukaendelea na maisha kama kawaida.
 
Umetoa wapi muda wa kuja kupost huku hivyo umeshindwa hata kufanya maamuzi juu ya hilo..??
Ila watu tunatofautiana sana aisee
Kabisaa...Mimi binafsi kwa venye ningemfanya walah Angenifafanulia kuhusu hio kauli yeye mwenyewe...
 
Alishachapwa tayari na watu wa Dar wakati anaonyeshwa mjini. Lakini watamdampo tu
 
Red flag hiyo mzee, kakwambia kuwa wewe sio type yake na bila shaka yupo in open relationship akimpata type yake wewe ndio utakua mchepuko.

Tafuta mwanamke mwengine wanaume hatutakiwi kuwa na option moja, NEVER EVER.
 
KAMA UMEFUNGA NAE NDOA YA KIISLAAM...NA HAMNA MTOTO BADO...ACHANA NAE OA MWINGINE...

KUNA ANAOWAONA NI TYPE YAKE BAADA YA KUJA MJINI...MWACHE AENDE...
Hata kama mna watoto inawezekana kuachana.
 
Dah mkuu umenipiga penye mshono hiyo kauli niliambiwa jana mpaka najiuliza kwanini anayasema haya kipindi hiki ambacho sina kazi mbona nilipokuwa kazini hakuyasema haya,M/MUNGU atusaidie sana wanaume tulio ktk ndoa
 
Kuna mambo huwa mwanamke anaficha sana, ila ukiona yanaanza kuonekana kupitia yeye mwenyewe ni heri kufanya maamuzi magumu.
 
Pia wapo wengi wanaotamani kurudi kwa wapenzi wao. Mpenzi ajaye ni bora kuliko aliyopo mpaka anapofika.
 
Hawa viumbe huwa hawana siri, asipoongea kwa mdomo ataongea kwa vitendo au hisia.
Hapo amekutana na wajanja wa jiji wewe waonekana mshamba
 
Dah mkuu umenipiga penye mshono hiyo kauli niliambiwa jana mpaka najiuliza kwanini anayasema haya kipindi hiki ambacho sina kazi mbona nilipokuwa kazini hakuyasema haya,M/MUNGU atusaidie sana wanaume tulio ktk ndoa

Hapana mkuu, Wala isikuumize sana. Kikubwa jitahidi na jipange kipindi Cha mpito kiishe salama. Nnaimani tu dhoruba zitatulia na utarudi kwenye Hali Yako.

Nimeandika hayo Kwa sababu Hawa wenzetu, wanategemea uhakika wa vitu vingi kutoka kwetu, Sasa wanapoona Kuna Hali inatetereka, wanaingiwa na hofu ya mustakabal wa maisha. Na Kwa wenzetu Kuna wakati hawajali sana jinsi maneno yanavyotuumiza, wakishaongea ikawapa ahueni wanajua imeisha kumbe kwetu hayo maneno yanapiga kelele Kila siku kichwani.

Nawasihi wake zetu ni kweli Kuna wakati tunakosea ila nanyie mjitahidi kutumia vizuri maneno, mchague Kwa uangalifu kipi Cha kusema, hata kama tumekosea, maneno yanararua na kuchoma sana nafsi, Kuna makovu na majeraha hayaponi upesi.

Cha msingi, jitahidi kutekeleza wajibu wako na nikutakie uvumilivu na Kila la kheri Mwenyezi Mungu akufanyie wepesi katika mitihani Yako uvuke salama.
 
Umetoa wapi muda wa kuja kupost huku hivyo umeshindwa hata kufanya maamuzi juu ya hilo..??
Ila watu tunatofautiana sana aisee
Japo nawe ulishindwa kufanya maamuzi pale kwenye s pool🤣🤣🤣
 
Alishachapwa tayari na watu wa Dar wakati anaonyeshwa mjini. Lakini watamdampo tu
Wanasemaga kuwa mke wa mtu ni mtamu akiwa kwa mmewe, akiachwa kila mtu anamkimbia
 
Mbona rahisi tu hiyo, anamaanisha umeokota dodo chini ya mnazi akili zilikuwa zimelala, hamaanishi saizi zimeamka hapana yuko katika Hali ya kujuta maana hata kama zikiamka Hana option jua limeshazama makeup haikai vizuri
 
Hihihi pole mkuu, ila akipata type yake maumivu yatakuhusu
 
Wanawake ni waoga kwa waume zao Ila Hadi kapata ujasiri wa kukuambia hivyo basi jua amekuona wewe ni bonge la bwege
 
Aiseh Pole sana hapo mke hauna sa hv umebaki na kiburudisho tu.
 
Toa way forward sasa amwache au aendelee nae?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…