Kauli hii ya mke wangu ina maana gani?

Kauli hii ya mke wangu ina maana gani?

Mbona kasema ukweli wa kawaida tu Mkuu. Na wewe ilitakiwa uweke utani hapo umsome vizuri sio kinyonge ungejua zaidi.

Labda ulimpata coz alikuwa akitoka job anarudi home hana mishe mishe ila kwa Dar anaona anaweza kuwq na mishe mishe zaidi akawa bize ambapo msingeonana kirahisi.

kiuhalisia maisha ya mkoani ni tofauti sana na Dar, mkoani mtumishi akitoka job saa 9 na nusu hawezi kufanya biashara ikaleta hesabu zuri ila kwa Dar hata ukitoka job saa 12 bado unaweza ukafungua biashara yako ukafanya hadi saa sita usiku watu wapo

Labda angekuwa bize sana kama angekuwa Dar tangu mwanzo hivyo msingeweza kuonana na hata kuoana.
 
dah,ila inauma kwani ni lazima kila kitu uongeee jamani,hali hiyo huwapata watu wengi ila unakaa kimya
mwambie hivi hata mi nashangaa ilikuwaje nikakuoa au uliniwekea limbwata?
by the way haya maisha ukiwa serious sana utapoteza kila kitu emu mpuuzie yawezekana ni hasira au nawe umekuwa ukimsumbua,mpotezee tu
Akimwaga mboga wewe unabomoa jiko
 
Siku hizi imekuwa kawaida kwa vijana kuja kuweka hadharani mijadala wanayofanya na wake zao wakiwa vyumbani mwao halafu wanakuja kutaka maoni ya akina sisi ambavyo hayatuhusu na wala hatujui mambo yanaendelea vipi huko nyumbani. Ni sawa na mtu kukuonyesha clip ya mjadala halafu anataka maoni yenu.

Hivi hii dunia ya kisasa ikoje? kwani mpaka kila siri ya nyumbani uilete kwenye mitandao kwa mjadala? Matokeo yake unaambia 'huyo hakufai', 'mwache' ... kitu ammbacho kinakufanya uchanganyikiwe wakati pengine bado unampenda mwenza wako.

Imefika muda sasa tuone madhara ya haya mambo na kuwa na umakini nayo.
Umemaliza..mjadala ufungwe.
 
Mke wako inaonekana ni rafiki yako mnaongea kila kitu nothing wrong apo ila be alerted
 
Sijaonaa tatizo Sana kwenye hiyo kauli kiasi Cha mtu kuvunja ndoaaa...yawezekana kbsaa muktadhaa wa mazungumzo yenu uliruhusu kutokea kwa hayoo manenoo...get cool maisha lzma yaendeleeee jamani..Hivi mnafikiri mtaacha wangapii?...Dunia hii mkamilifuu hayupooo kila mmoja ana mapungufuuu yakeee🙌🙌take a heart brooo maisha lzma yaendeleeee

We endelea kuishi na wakwako, kwa kauli nyingine kamwambia "I was desperate ndo maana nilikukubali"
 
Akili kumkichwa!! Kaa kijeshijeshi muda wowote kinanuka!! Backup iwe karibu mkuu.
 
Binti ukimtoa kijijini kumpeleka mjini hayo ndio matokeo.

Muulize Professor J kilichompata! 😀
 
Overthinking kills Brother,maisha baada ya hiyo kauli yapoje..tabia ya mkeo iko vipi? kuna tabia mpya ambayo hakuwa nayo mwanzoni ameiibua! As a man you need to be emotional strong, base with important fact..Yamkini aliongea hayo mkiwa mnabonga story za hapa na pale mwamba ukaichukulia serious!
 
Ni kweli kakosea kusema haya maneno lakini aliyasema kwenye mazingira gani? Kama kumekuwa na ugomvi baina yenu na hakuna amani kabisa ni sahihi wewe kuiona kama red flag. Lakini kama kumekuwa na amani baina yenu..na ni mke mwema kwako dont overthink hiyo maneno alosema....itakuondolea raha.

Ukiwa mtu wa kuanalyze kila neno, tendo, decision, choice za your partner..mke ama mume, utakuwa mtu wa hasira sana moyoni, uchungu utapata kao katika maisha yako. Jifunze kupuuzia mambo..ili uwe na amani. Ukiwa na amani, utaweza kufanya kazi zako vizuri..as long as anafanya majukumu yake kwako na watoto na familia kwa ujumla, potezea hiyo statement.

Wanawake kuna muda kuna kama kakichaa huwa tunacho. Na kila mwanamke hakosi haka kakichaa..sema tu inategemea kitatokaje, mwingine kwa kuongea maneno yasiyo na idadi, mwingine kwa kuropokwa kwa nguvu, mwingine kwa kwenda kupeleka poonani nje anyooshwe ili akili imkae sawa, mwingine alewe mpaka apelekwe nyumbani, mwingine kwa kutukana matusi makubwa, mwingine kwa kulia sana kwa uchungu.na mwingine kwa kuondoka nyumbani kwake, kibaya kuna mwingine mpaka aone damu au mme wake kazimia au kaumia ndo na yeye atatulia.

Sasa kwenye uchumba si rahisi sana kuyaona haya..hata kama mmedate miaka mitano sijui mkaishi pamoja..kuna kale katabia ama kakichaa katajificha, sasa isitokee mkaoana maana si utaona "ooh huyu nimemjua vizuri nishajua madhaifu yake yote na anafit kuwa mke wangu unaoa"...hahaahahaha...mambo ndo yanakuwa yananoga..wapare wanasema yanora. Utaanza sasa kuona zile rangi. Kwaiyo aso hili ana lile. Pima mwenyewe!!
Kichaaa apeleke kwao sio kwangu.
 
Acha kuzunguka ulitakiwa kumuuliza hapo hapo "unamaanisha nini?" sio kukaa na maswali moyoni uanze kujiuliza pasipo majibu.

Ningekua mimi ningemuuliza unamaanisha nini bibie, aseme anachotaka kama mimi sio mtu wa kumfaa akafie mbelee huko daaadeki😂
 
Kwa kweli Profesa Jay aliimba uhalisia uliopo katka jamii ....mkuu huyo kashakuwa mjanja
 
Nadhani ukiwa mbinga hadhi yako ilionekana kuwa juu. Sasa kaja DSM anaona wadosi wengi..watu wana makumba na magari ya kifahari, wanakula bata...anatamani kama angekuwa na yeye hivyo....anadhani kiwa angekuwa Dar angeweza kuolewa na mmoja ya hao ma don.

Usichanganyikiwe wala usijisikie vibaya. Wanawake ni watu wa kufanya comparison, wanapenda kulinganisha maisha yao na ya wengine...hawaridhiki na maisha kwani wao hupenda mashindano na kujionyesha.

Na wakati mwingine wana kauli za kuudhi..kama hizo ambazo huwa wanaropoka bila kujua madhara yake...

Utasikia, wewe naye ni mwanaume...wakiita wanaume na wewe utaenda...huna akili, angalia wenzako wenye akili wanavyofanya....n.k. Maneno kama haya ni kawaida sana sana..hata uwe umefanikiwa kiasi gani bado watakulinganisha na walio kuzidi na kukutolea maneno.

Wala usipaniki kila mwanaume anapitia unanyanyasaji huo..hadi tumezoea. Isikuumize kichwa.
 
Back
Top Bottom