Uchaguzi 2020 Kauli mbiu ya Uhuru na Kazi yampaisha Tundu Lissu

Molemo

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
14,620
Reaction score
13,358
Ni ukweli uliowazi Sasa kwamba mgombea Urais kupitia Chadema Tundu Lissu ni kama amewameza wagombea wenzake na hawasikiki tena.

Tangu ateuliwe na chama chake CHADEMA na kisha kuchukua fomu za kuteuliwa kutoka tume ya uchaguzi NEC Lissu amekuwa gumzo kila kona huku akijadiliwa zaidi kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii.

Lissu amekuwa akifanya ziara mikoa mbalimbali ya kusaka wadhamini huku akilakiwa na Maelfu kwa maelfu kokote anakopita.

Mojawapo ya sababu kubwa ya kupata uungwaji mkono huo kutoka kwa wananchi hasa waliohojiwa kila anakopita ni kauli Mbiu yake ya 'Uhuru na Kazi' akimaanisha pamoja na kutakiwa kufanya kazi lakini katika serikali yake wananchi watakuwa huru hasa katika kufanya siasa, kupata habari mbalimbali bila ubaguzi, vyombo vya Habari kuwa huru bila kufungiwa hovyo, waandishi wa habari kutokunyanyaswa na watu kuwa huru kukosoa serikali yao bila kuogopa kukamatwa na kufungwa.

Pia Lissu amekuwa akijinasibu katika serikali yake ni mwiko kuingilia Bunge na mahakama bali kuiacha mihimili hiyo kuwa huru katika maamuzi yake. Pia wananchi kuwa huru kuangalia LIVE Bunge lao.

Mgombea huyo wa Chadema anasema kutaka watu wafanye kazi tu huku ukiwanyima Uhuru wao ni dhambi kubwa ambayo kamwe serikali yake haitafanya.
 

Attachments

  • VID-20200819-WA0080.mp4
    4.9 MB
Kwa kweli hata mimi nahitaji uhuru , mtu anayenizuia hata kumwombea mtu aliyepigwa risasi 16 nitampaje kura yangu? Heri nilale njaa ila niwe huru.Siku zote wanadamu timamu wanausaka uhuru.Sitachoka kuusaka na kuupigania uhuru.
 
Nani kama Tundu Lissu, cheki alivyovuta nyoyo za waTanzania kudai uhuru katika kazi zao za ukulima, uvuvi, ufugaji , biashara na haki ya mlipa-kodi kupata Uhuru ndani ya Maendeleo yake ktk kila kona ya nchi

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…