Uchaguzi 2020 Kauli mbiu ya Uhuru na Kazi yampaisha Tundu Lissu

Uchaguzi 2020 Kauli mbiu ya Uhuru na Kazi yampaisha Tundu Lissu

Dhana ya Uhuru zaidi kujiamulia mambo yao wenyewe ni dhana yenye maana pana sana. Watu jamii ya waislam wanaamini nadharia ya Serikali kutokuwa na dini ni nadharia iliyowekwa ili kuzuia ustaarabu wa dini yao kustawi.

Tundu anapaswa kusema bila kutafuna maneno endapo ataendeleza ukandamizwaji huo au kuweka wazi ili apate kura za wenye dini inayokandamizwa.

Huwezi kuwakandamiza watu kwa muda mrefu pasipo wao kuzinduka. Binafsi najaribu kuwaza ni jinsi gani CHADEMA itatatua tatizo hili. Watu wanajifunza asili yao na pale wanapojihisi wanabaguliwa huwa tayari kutetea haki zao na ikibidi ghasia hutokea.

Kwani watu hubadilika na kamwe hawatoridhika kujiona wao no jamii ya daraja la pili iwapo kuna chama kinaweza kuwapa Uhuru wa kujiamulia mambo hao ikiwemo utamaduni wao.
Uliloandika hapa ndiyo msimamo wa Tundu Lissu Rais mtarajiwa
 
Sio chama Cha siasa tu Ni chama tawala, vijimaneno vya Wana Sacco's havitusumbui tupo na jembe magufuli HAPA KAZI TU [emoji23][emoji1787]
Naona uko night shift, piga kazi buku 7 iende kihalali taga.
 
Naona uko night shift, piga kazi buku 7 iende kihalali taga.
Wanaccm wanajitambua wamejiajiri/kuajiriwa,sio nyie Wana Sacco's kazi kucheza pool table na kushinda mitandaoni bila kutumia mitandao hiyo kuingiza faida halafu mnalalamika Hali ngumu shukran kwa awamu ya 5 kwa kutupeleka kipato cha kati
 
UCHUMI WA KATI WEE ULIUSIKIA WAPI??
tapatalk_1597847643297.jpg
 
Ni ukweli uliowazi Sasa kwamba mgombea Urais kupitia Chadema Tundu Lissu ni kama amewameza wagombea wenzake na hawasikiki tena.

Tangu ateuliwe na chama chake CHADEMA na kisha kuchukua fomu za kuteuliwa kutoka tume ya uchaguzi NEC Lissu amekuwa gumzo kila kona huku akijadiliwa zaidi kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii.

Lissu amekuwa akifanya ziara mikoa mbalimbali ya kusaka wadhamini huku akilakiwa na Maelfu kwa maelfu kokote anakopita.

Mojawapo ya sababu kubwa ya kupata uungwaji mkono huo kutoka kwa wananchi hasa waliohojiwa kila anakopita ni kauli Mbiu yake ya 'Uhuru na Kazi' akimaanisha pamoja na kutakiwa kufanya kazi lakini katika serikali yake wananchi watakuwa huru hasa katika kufanya siasa, kupata habari mbalimbali bila ubaguzi, vyombo vya Habari kuwa huru bila kufungiwa hovyo, waandishi wa habari kutokunyanyaswa na watu kuwa huru kukosoa serikali yao bila kuogopa kukamatwa na kufungwa.

Pia Lissu amekuwa akijinasibu katika serikali yake ni mwiko kuingilia Bunge na mahakama bali kuiacha mihimili hiyo kuwa huru katika maamuzi yake. Pia wananchi kuwa huru kuangalia LIVE Bunge lao.

Mgombea huyo wa Chadema anasema kutaka watu wafanye kazi tu huku ukiwanyima Uhuru wao ni dhambi kubwa ambayo kamwe serikali yake haitafanya.
Amesema amekodi msemo huo kutoka kwa Baba wa Taifa Mwl. J K Nyerere...?
 
Tatizo Watanzania wengi hawajaguswa sana na ishu ya Uhuru.

Ongeleeni kuhusu Uchumi.

Uhuru ndiyo hoja ya msingi kabisa hiyo kamata kamata hiyo imemgusa kila mtanzania hasa wa mijini uhuru hauna substitute pata vyote maishani mwako kukosa uhuru utatamani ukose kila kitu uwe na uhuru kama alivyosema Nyerere ni afadhali kuwa masikini lakini uko huru
 
Nani kama Tundu Lissu, cheki alivyovuta nyoyo za waTanzania kudai uhuru katika kazi zao za ukulima, uvuvi, ufugaji , biashara na haki ya mlipa-kodi kupata Uhuru ndani ya Maendeleo yake ktk kila kona ya nchi

1597875037526.png

treni ya arusha na tundu lissu nan amejaza zaidi ya mwingine, imagine treni ina watu wengi kuliko mgombea sasa jamaa alieleta treni mwenyewe akianza kuzunguka itakuaje, nafurahi kuona upinzani wa vyama vingine unakua hili cdm kichefuchefu lipishe wengine wawafundishe kazi
 
Uhuru ndiyo hoja ya msingi kabisa hiyo kamata kamata hiyo imemgusa kila mtanzania hasa wa mijini uhuru hauna substitute pata vyote maishani mwako kukosa uhuru utatamani ukose kila kitu uwe na uhuru kama alivyosema Nyerere ni afadhali kuwa masikini lakini uko huru
Umenena vema sana.Ingelikuwa Uhuru hauna maana tusingemtoa mkoloni
 
Amesema amekodi msemo huo kutoka kwa Baba wa Taifa Mwl. J K Nyerere...?
Kwani Kuna neno gani geni na jipya Dunia hii ambalo halijawahi kutamkwa na mtu? Lina Hatimiliki kwani kwamba ni marufuku mtu mwingine kulitamka kinywani?
 
Back
Top Bottom