Kauli tatu za ajabu sana Tanzania kuhusu vifo vya viongozi

Kauli tatu za ajabu sana Tanzania kuhusu vifo vya viongozi

Kifo ni njia ya binadamu na viumbe wengine wote. Inakuwaje mtu anafurahia kifo cha mwenzie kwa sababu za kisiasa? Nape na Makamba hawataishi milele; wanaisubiri siku yao ambayo haiko mbali sana ambapo maneno yao hayo yatawarudia.
 
Ukweli ni kwamba tumekuwa na siasa za vyama vingi rasmi kuanzia 1992 lakini hapakuwa na uhasama wa aina hii hadi 2015 awamu ya 5 ilipoingia madarakani.
Tuwe wakweli, baada ya Magufuli kuingia madarakani chuki, wivu, uhasama na visasi vikachukua nafasi na yote hayo yakipata baraka zake mwenyewe ndio maana hakukemea.
Vifo vya ajabu, kushambuliana na kutekana kukachukua nafasi. Mbaya ni kuwa wapambe wake wakawa na kauli za kusapoti na kukejeli bila woga.
Baada ya Magufuli kufa, sio kuwa hawa waliopo kuanzia Samia ni wageni bali walikuwa naye. Hivyo kauli aliyo isema Lissu kule Katoro Geita ni ya msingi sana kuwa Rais ili alete maridhiano ya kweli (sio vyama tuu bali wato wote wenye chuki) yeye na viongozi wenzake WAWAOMBE RADHI waathirika wote na wakulaumiwa alaumiwe ili tuponye nchi.
Baada ya hayo atakaye mnenea mwingine mabaya ataonekana wa ajabu na upendo ule wa zamani wa Mke CCM na Mume Chadema na wanaishi pamoja utarudi.
 
1. Mungu kaamua ugomvi
2. Watu wazuri hawafi
3. Keshaanza kuoza.

Naona kama vile kauli hizi zitatutesa sana kwenye umoja wetu kama taifa huko tuendako.
We Mzee unazeeka vibaya hiyo kauli Mama Samia aliisahisha hapo hapo juu na kumuombea radhi Makamba mbona mnakuza mambo.

Kingine hiyo kauli ya Makamba alimwambia pia Samia kuwa hata yeye akifa atakuja Rais mwingine.... I wonder why inaonekana kama imelenga upande mmoja pekee!!

Cha ajabu kipindi JPM anapambania uhai wake wewe ulikua unakataa unasema yupo kwenye mfungo wa maombi. Yaani ulijua kabisa unadanganya alafu baada ya kifo ndio unajifanya una uchungu naye sana kwa kurudia maneno ya chuki yaliyokwisha ombewa radhi na Rais!!

Aisee
 
Narudia na ntaandika tena na tena.

Usitarajie binadamu yeyote auhuzunike na kifo chako wakati ulipokuwa hai ulimtesa kumnyima haki zake za msingi na hata kujaribu kumuua.

Binadamu wa hivyo hayupo.

Hata mitume awakuwa hivyo.

Ukiwatendea watu ubaya ukifa lazima wafurahie.

Jiwe kama aliwatendea watu uovu lazima wafurahie kifo chake.

Unafkiri lissu aliyeponea chupu chupu kuuliwa atamfurahia mtesi wake?

Hapana lazima afurahi akisikia amekufa.

Hapo sijaongelea ndugu wa Ben sa nane.

Viongozi wanapaswa kuongoza kwa hekima na busara bila kusahau kufuata sheria tulizojiwekea.

Ukijiamulia wewe kama wewe na kuwaumiza wengine lazima maneno kama 'anaoza' ,'kazikwe nae' Mungu kaamulia ugomvi' yawepo tu.

Cha kujiuliza mbona Nyerere na Mkapa wamekufa lakini hawakuandamwa kwa maneno mabaya kama jiwe?
 
We Mzee unazeeka vibaya hiyo kauli Mama Samia aliisahisha hapo hapo juu na kumuombea radhi Makamba mbona mnakuza mambo.

Kingine hiyo kauli ya Makamba alimwambia pia Samia kuwa hata yeye akifa atakuja Rais mwingine.... I wonder why inaonekana kama imelenga upande mmoja pekee!!

Cha ajabu kipindi JPM anapambania uhai wake wewe ulikua unakataa unasema yupo kwenye mfungo wa maombi. Yaani ulijua kabisa unadanganya alafu baada ya kifo ndio unajifanya una uchungu naye sana kwa kurudia maneno ya chuki yaliyokwisha ombewa radhi na Rais!!

Aisee
Kila mtu ana imani yake, kuna wale hawatubu kosa ila kwa kuombewa, na wapo wengine hutubu kwa kauli na ndimi zao wenyewe wakasamehewa lakini bado wakarudia yale yale.

Hii ndio Bongo akili mu kichwa
 
1. Mungu kaamua ugomvi
2. Watu wazuri hawafi
3. Keshaanza kuoza.

Naona kama vile kauli hizi zitatutesa sana kwenye umoja wetu kama taifa huko tuendako.
Na kama kuna funzo lolote tunaloweza kujikumbusha juu yake kuhusu haya uliyoandika hapa ni kutazama tulikoanzia toka wakati ule tunapata uhuru wetu.

Funzo lipo hapo hapo.

Vikabila chungu nzima, na kila kimoja kimeshikilia mambo yao na machifu wao.

Ile kazi ya kujenga umoja ule sasa watu hawaioni kuwa ilikuwa ni kazi iliyofanywa kwa umakini mkubwa sana. Watu sasa wanabeza juhudi hizo.

Ili tuepuke kudidimia huko tunakoelekea, ni muhimu sana wapatikane viongozi wanaojali zaidi utaifa wetu, viongozi wazalendo kwelikweli, na siyo wa uzalendo wa kuvaa kwenye 'mikono ya mashati' anaoweza mtu kuuvaa na kuuvua wakati wowote anavyopenda yeye.

Sijui hawa watu tutawapata vipi, kama hawataki kujitokeza mbele waifanye kazi hii muhimu.
 
Back
Top Bottom