The Burning Spear
JF-Expert Member
- Dec 23, 2011
- 4,118
- 9,864
TrashUkweli ni kwamba tumekuwa na siasa za vyama vingi rasmi kuanzia 1992 lakini hapakuwa na uhasama wa aina hii hadi 2015 awamu ya 5 ilipoingia madarakani.
Tuwe wakweli, baada ya Magufuli kuingia madarakani chuki, wivu, uhasama na visasi vikachukua nafasi na yote hayo yakipata baraka zake mwenyewe ndio maana hakukemea.
Vifo vya ajabu, kushambuliana na kutekana kukachukua nafasi. Mbaya ni kuwa wapambe wake wakawa na kauli za kusapoti na kukejeli bila woga.
Baada ya Magufuli kufa, sio kuwa hawa waliopo kuanzia Samia ni wageni bali walikuwa naye. Hivyo kauli aliyo isema Lissu kule Katoro Geita ni ya msingi sana kuwa Rais ili alete maridhiano ya kweli (sio vyama tuu bali wato wote wenye chuki) yeye na viongozi wenzake WAWAOMBE RADHI waathirika wote na wakulaumiwa alaumiwe ili tuponye nchi.
Baada ya hayo atakaye mnenea mwingine mabaya ataonekana wa ajabu na upendo ule wa zamani wa Mke CCM na Mume Chadema na wanaishi pamoja utarudi.