Kauli tatu za ajabu sana Tanzania kuhusu vifo vya viongozi

Kauli tatu za ajabu sana Tanzania kuhusu vifo vya viongozi

I'm not CCM ila msiba wa JPM ni CCM na Membe ni CCM Sasa inanihusu Nini mie muuza migebuka huku Nyarubanda?

Mna tatizo kudhani Kila anayekosoa JPM basi automatically ni team JK/Membe/Samia.
Mbona umepaniki
 
Kwa sasa slowly tunarudishwa kwenye ukabila au vieneo maalumu kama ulivyoita...!!. Nakumbuka hata bungeni, akina Msukuma walidai, wale ambao majimbo yao hayana madini (dhahabu in this regard) basi wakae kimya wakati mjadala wa dhahabu unafanyika, maana hawana uzoefu huo. Hii ilikuwa ni dalili ya ujimbo. Nikawaza vipi ikifika mkonge unajadiliwa waachiwe wa Tanga na Morogoro wajadili? au korosho waachiwe wa Mtwara Lindi na Ruvuma? au mahindi je waachiwe the big four? Miwa nayo ikifikwa kujadiliwa waachiwe wa Morogoro na Kagera? Na kahawa ikifikiwa, waachiwe wa Mbinga, Bukoba, Kilimanjaro na Arusha pekee wajadili? Kokoa watawaachia wa Mbeya wafanye yao? Ni hatari kwa kweli. Mwisho wa siku kila watu wangejenga bunge lao huko waliko kutegemeana na nini wanazalisha.
Huyo Mbunge uliyemtaja hapo ni mmoja wa watu wa hovyo kabisa wasiostahili kuwa mahali kama hapo alipo.
 
Ukweli ni kwamba tumekuwa na siasa za vyama vingi rasmi kuanzia 1992 lakini hapakuwa na uhasama wa aina hii hadi 2015 awamu ya 5 ilipoingia madarakani.
Tuwe wakweli, baada ya Magufuli kuingia madarakani chuki, wivu, uhasama na visasi vikachukua nafasi na yote hayo yakipata baraka zake mwenyewe ndio maana hakukemea.
Vifo vya ajabu, kushambuliana na kutekana kukachukua nafasi. Mbaya ni kuwa wapambe wake wakawa na kauli za kusapoti na kukejeli bila woga.
Baada ya Magufuli kufa, sio kuwa hawa waliopo kuanzia Samia ni wageni bali walikuwa naye. Hivyo kauli aliyo isema Lissu kule Katoro Geita ni ya msingi sana kuwa Rais ili alete maridhiano ya kweli (sio vyama tuu bali wato wote wenye chuki) yeye na viongozi wenzake WAWAOMBE RADHI waathirika wote na wakulaumiwa alaumiwe ili tuponye nchi.
Baada ya hayo atakaye mnenea mwingine mabaya ataonekana wa ajabu na upendo ule wa zamani wa Mke CCM na Mume Chadema na wanaishi pamoja utarudi.
Wachapakazi huwa Wana kazi ngumu Sana
 
We Mzee unazeeka vibaya hiyo kauli Mama Samia aliisahisha hapo hapo juu na kumuombea radhi Makamba mbona mnakuza mambo.

Kingine hiyo kauli ya Makamba alimwambia pia Samia kuwa hata yeye akifa atakuja Rais mwingine.... I wonder why inaonekana kama imelenga upande mmoja pekee!!

Cha ajabu kipindi JPM anapambania uhai wake wewe ulikua unakataa unasema yupo kwenye mfungo wa maombi. Yaani ulijua kabisa unadanganya alafu baada ya kifo ndio unajifanya una uchungu naye sana kwa kurudia maneno ya chuki yaliyokwisha ombewa radhi na Rais!!

Aisee
Wazuri Bana ndugu yangu usisahau
 
Acha kauli chafu zianikwe, vipi inakuuuma?
Rais alishaomba msamaha... Mkienda kwa staili hiyo watu wakifukua kauli za JPM kudhihaki afya ya Lowassa unadhani chuki zitaisha lini? Walikua wanasema kajinyea, mara hakuna ICU ikulu huku JPM anachekelea. Mbona mwenzie kasamehe licha ya kutokuombwa radhi ila nyie mmekalia tu kukumbushia kauli iliyokwisha futwa na Rais.
 
We Mzee unazeeka vibaya hiyo kauli Mama Samia aliisahisha hapo hapo juu na kumuombea radhi Makamba mbona mnakuza mambo.

Kingine hiyo kauli ya Makamba alimwambia pia Samia kuwa hata yeye akifa atakuja Rais mwingine.... I wonder why inaonekana kama imelenga upande mmoja pekee!!

Cha ajabu kipindi JPM anapambania uhai wake wewe ulikua unakataa unasema yupo kwenye mfungo wa maombi. Yaani ulijua kabisa unadanganya alafu baada ya kifo ndio unajifanya una uchungu naye sana kwa kurudia maneno ya chuki yaliyokwisha ombewa radhi na Rais!!

Aisee
Nitakujibu nikirudi kutoka fainali.
 
Back
Top Bottom