Kauli ya Chongolo ni ufedhuli kwa wasomi wa vyuo vikuu. Ipingwe!

Aseme wazi hakuna haja ya vijana kwenda vyuo vikuu kwanza baada ya kumaliza sekondari. Yani wakimaliza tu kidato cha nne wote waende VETA kwanza au pia badala ya kwenda kuruka kwata JKT wale vijana wa kidato cha sita waende VETA ndipo wajiunge na vyuo vikuu.
Huo ndio ukweli ndugu, mtu aliehitimu VETA ni bora kwa kila kitu ukilinganisha na wa chuo kikuu, ndivyo ilivyo, The way the cookie crumbles..
 
Huo ndio ukweli ndugu, mtu aliehitimu VETA ni bora kwa kila kitu ukilinganisha na wa chuo kikuu, ndivyo ilivyo, The way the cookie crumbles..
Wewe mpika vitumbua uliyehitimu veta usijpe faraja kwa kauli ya Chongolo.

Masomo ya vyuo vikuu hayakupswa kutolewa kama mahubiri ya Mwamposa. Yalipswa kuambatana na vitendo kwa wingi. CCM imefanya siasa ktk elimu ya juu badala kufanya uwekezaji mkubwa utakaowezesha wanafunzi kusoma kwa vitendo
 
Huyo Chongolo angesema hivyo wazi, sio kusubiria watu wamemaliza vyuo vikuu wakiwa kwenye madeni makubwa ya mkopo halafu anasema hatuwezi kuwapa ajira wa vyuo vikuu badala yake warudi kusoma VETA.
Hakukuwa na haja ya mlolongo mrefu wa kidato cha sita na chuo kikuu na gharama za fedha baada ya kumaliza kidato cha nne wakati mpango mzima na suluhu la matatizo ni VETA.
 
CCM ndiyo tatizo. Wame-politicize elimu ya chuo kikuu inonekana Kama ya chekechea. Suluhisho siyo kukimbilia veta bali kuwekeza zaidi ili mafunzo ya vitendo yatolewe. CCM wanalikimbia hili
 
Chongolo ailekeze CCM ianze kubadilisha mfumo wa elimu baada ya kidato cha nne vijana waelekee VETA badala ya Advance level na vyuo vikuu na atoe hizi sababu zenu.
Hakuna haja ya kusubiria waende katika mlolongo mrefu wa zaidi ya miaka mitano ambapo wanakuwa wamepoteza muda na fedha wakati VETA na kuwa fundi bomba, ujenzi, gari, seremala n.k ndio mpango mzima
 
Uko sahihi kwa 100%
 
Mbona kasema ukweli, amedhihirishia umma kwamba elimu yetu ni ya ovyo, kwahiyo ni apingwe tu hata kama kasema ukweli et
 
Yaani na bachelor yake akaanze kusoma tena kupiga rangi sijui kuunganisha umeme?

Halafu hata hizo kazi za ufundi zenyewe zitawasaidia hao vijana kupata hela ya kula tu hakuna la maana watafanya.

Nachukia sana watu wanaorahisisha vitu wakati mfumo wa elimu wametengeneza wao. Like seriously, uanze tena kusoma kuunganisha mabomba?

Halafu hivi yeye amewahi kujiajiri hata kidogo, kama hajui kujiajiri ni moja ya kazi ngumu sana, yaani anakuwa na maisha ambayo uncertainly hana tofauti na "deiwaka" ukiamka mpaka mtu awaze kuja kwako kupata huduma.
 
Nakazia. Wanafunzi wawe huko field kwa miaka yote 3 au 4 mpk siku wanahitimu.
 
Nchi zilizoendelea ni kwa sababu walifanya na wanafanya "division of labour".
Nainga kauli yake mkono. Hatujuwi kazi nyingine wasomi hii ni hatari. We will die masikini sana
 
Weweee!Ebu kosome VETA huko.Usitusumbue na fikra mfu zako.
 
Hii ni kweli.
 
Unaweza kutaja japo nchi moja tu duniani iliyojitosheleza kiajira kwa raia wake wote?.
 
Wewe uliyesomea MAENDELEO YA JAMII,nje ya kuajiriwa unaweza kujiajiri kufanya kipi?.
 
Nb 3: Mtaa una kanuni, sheria na taratibu zake ambazo hutafundishwa chuoni!!!!!!!!!!

Ni mtazamo!!!!!!!!!!!!!!!!
Na bado unasisitiza wahitimu wa chuo kikuu, wakajiunge chuo cha ufundi, VETA.
 
Vitendo katika fani ipi?Anayesomea maendeleo ya jamii anaweza fanya mafunzo ya vitendo vipi ili mtaani ajiajiri?.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…