Kauli ya Chongolo ni ufedhuli kwa wasomi wa vyuo vikuu. Ipingwe!

Haya tena! Hapo bosi wako Lucas Mwashambwa anakupa ushauri wa bure kuwa uache maisha ya uchawa, na kisha uende VETA ili uanze mafunzo ya awali ya kuwa fundi mchundo.
 
Haya tena! Hapo bosi wako Lucas Mwashambwa anakupa ushauri wa bure kuwa uache maisha ya uchawa, na kisha uende VETA ili uanze mafunzo ya awali ya kuwa fundi mchundo.
CCM inawafanya watanzania kuwa mazuzu.
 
 
Nasubiri tamko la wahitimu wa vyuo kama walivyotoa Watukufu waendesha Bodaboda. Vinginevyo tutaamini tamko la Bodaboda ni la UV CCM.
 
Tusaidie- wanao maliza shahada ya sheria na kwenda shule ya sheria unawaweka wapi?
 
Huo ndio ukweli ndugu, mtu aliehitimu VETA ni bora kwa kila kitu ukilinganisha na wa chuo kikuu, ndivyo ilivyo, The way the cookie crumbles..

Punguza uongo, huko VETA wanafundishwa na walimu waliotoka vyuo vikuu, nani Bora hapo, acheni kudhalilisha vyuo vikuu kwa kuvilinganisha na VETA.
 
Hao ndio waliopewa Nchi na mawazo yao ndio haya.

Tz ni zaidi ya uijuavyo.
 

Tofautisha quality ya mwanafunzi na qualification ya lecturer. Huwezi kuwa lecturer bila vigezo vya TCU. Lakini quality ya wanafunzi inaanzia mbali.
 

Wewe ndio unapotosha. Tofautisha employment opportunities na academic opportunities. Huwezi kumdhihaki mtu aliyesoma political science kisa hawezi kujiajiri, unatakiwa kujiuliza aliposoma political science alikuwa na lengo la kujiajiri au kuajiriwa?. Kama kuajiriwa achana naye. Huwezi kucheka academic opportunities kwa sababu ya employment opportunity ya plumbing.
 
Painting & Sign writing (PS)
Kuna dogo anasomea hii course hapo UDSM, sasa akimaliza inabidi aelekee VETA akasome tena kwa mara ya pili?

Wewe kiazi mviringo ongea vizuri na Serikali yako ipanue wigo wa fikra za viongozi sio wanawaza kupokea Posho & Mishahara inachangiwa na walipa Kodi alafu hawafanyi utatuzi wa Ajira zaidi ya kuwafukuzia watu VETA ndio maana naona vyuo vya VETA vinajengwa kwa kasi sana kumbe fikra zao ndio zimeelekea huko?
 

Vyote ulivyoandika hapo na zaidi vinafundishwa chuo kikuu. Tofautisha employment opportunities na academic opportunities.

Tusilazimishe kuidharau academic opportunity kisa haina employment opportunity, tutaaanguka pabaya. Kuwaambia graduates wa uhasibu au procurement kwamba turudi VETA tukasome ujenzi wa nyumba ni sawa nakuua profession yao.
 
Ukiweka siasa pembeni ndugu Chongolo yupo sahihi kabisa.

Hawa wahitimu lazima wawe na skills nyingine za kuleta ugali mezani .

VETA isimame Kama VETA , na Vyuo vikuu visimame Kama vyuo vikuu, tukianza ujinga wa kuonesha VETA ni Bora kuliko chuo kikuu ndio tutaua kila kitu.
 
Katika wasomi, Chongolo hayumo kabisaa.
Na karibu atapewa PhD ya Heshima na VETA.
 
Kama vip elimu ya. Vyuo vikuu ifutwe sasa,ili watu wote wenye shida na shule waende veta,maana wasomi wa vyuo vikuu Wana pondwa na kulushiwa mawe kutoka Kila Kona.
 

Wewe ndio mwenye shida. Kila chuo kina muda wa practicals, kila course, Sasa nadharia imetoka wapi?. Kwa maono yako graduates wa SUA, Bugando, Muhimbili, UDSM, Mzumbe hawana maana, ila std seven aliyeenda VETA na kufundishwa na graduate wa chuo kikuu ndio wa maana. Punguza unafiki. Mnatukana elimu kisa ajira hamna. Kwenu elimu Ni ajira tu, punguza mhemko, Yani vyuo vyote havina maana kisa
 

Hao VETA wanafundishwa na wahitimu wa vyuo vikuu, sasa sijui unongea Nini. Tatizo mnashabikia kauli za wanasiasa bila kufanya utafiti.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…