robinson crusoe
JF-Expert Member
- Oct 22, 2020
- 842
- 1,425
Nawe unajiandikia ujinga-ujinga tu! Wewe leo hii unavyoona kuna nani serikalini mwenye akili?View attachment 3653552
Kauli ya Heche inaleta dharau isiyostahili kwa viongozi wa Taifa. Kuwaambia “hakuna watu wenye akili na maarifa” si hoja, ni matusi yanayodhalilisha taifa badala ya kujenga. Uongozi una majukumu magumu; kukosoa kwa lugha ya kejeli hudhoofisha heshima ya nchi.
Kwa uwekezaji wa kutoka nje, teknolojia ni mojawapo tu. Mtaji ndiyo msingi mkuu, bila pesa hakuna kitu. Soko kubwa, utulivu wa kisiasa, sera nzuri, miundombinu, na motisha ya kodi ni muhimu zaidi. Mwekezaji wa Congo anaweza kuleta mtaji wake na kununua au kuleta teknolojia. Congo ina madini mengi na idadi kubwa ya watu, soko linalokaribiana nasi. Kuwaalika katika kilimo, uvuvi na madini kunafungua milango ya biashara ya pande zote, si kudhoofisha.
Kushughulikia bandari ni jambo zuri, lakini si kisingizio cha kukataa ushirikiano mbalimbali. Ushirikiano wa kikanda unajenga nguvu pamoja. Kukosoa bila kuona fursa ni kudumaza maendeleo. Hoja yake inakosa uelewa wa biashara za kimataifa na inaonekana zaidi kama siasa kuliko uchambuzi wa kiuchumi.
Mkuu, embu tulia kidogo, weka uccm au uchadema pembeni kama upo halafu jiulize kwanini raia wa Congo asiweze kuwekeza Tanzania?Mzee kuna muda unaandika mashudu 100%. Tukianza na kauli ya kusema viongozi hawana maarifa wala akili ni kauli sahihi kabisa. Ulitaka atumie neno gani kuelezea uhalisia wa “upeo” wa hao viongozi kwa kushangilia Congo kuwekeza nchini? Yaani Congo awekeze Tanzania! Kwa kipi? Kama ana huo mtaji kwa nini asiwekeze kwao? Kwamba anaipenda Tanzania kuliko nchi yake? Kwamba Congo hakuna ardhi ya kuwekeza kwenye kilimo? Mie naungana na Heche kuwa tunaongozwa na vilaza. Ila mie naenda hatua moja zaidi kwa kusema hata wewe ni kilaza promax kwa kukubali huu upuuzi wa watawala
Hii sio kweli. Tanzania ina fursa zake na Congo ina fursa zake. Raia wa Congo anaweza kuja hapa na akawekeza kwenye kilimo hata kama kwao ipo ardhi.Hali ya hewa na ubora wa ardhi Congo ukilinganisha na Tanzania, unawezaje kumshwishi mtu aje kulima Tanzania? Rubbish!
Tatizo la Heche anajionaga ana akili sana kuliko yoyote, 2010 halmashauri ya tarime ilikuwa chini ya chadema na yeye akiwa diwani, hakuna cha maana chochote walichofanya.
Kama eneo dogo tu wilaya kachemka nchi nzima ataiwezea wapi?
View attachment 3653552
Kauli ya Heche inaleta dharau isiyostahili kwa viongozi wa Taifa. Kuwaambia “hakuna watu wenye akili na maarifa” si hoja, ni matusi yanayodhalilisha taifa badala ya kujenga. Uongozi una majukumu magumu; kukosoa kwa lugha ya kejeli hudhoofisha heshima ya nchi.
Kwa uwekezaji wa kutoka nje, teknolojia ni mojawapo tu. Mtaji ndiyo msingi mkuu, bila pesa hakuna kitu. Soko kubwa, utulivu wa kisiasa, sera nzuri, miundombinu, na motisha ya kodi ni muhimu zaidi. Mwekezaji wa Congo anaweza kuleta mtaji wake na kununua au kuleta teknolojia. Congo ina madini mengi na idadi kubwa ya watu, soko linalokaribiana nasi. Kuwaalika katika kilimo, uvuvi na madini kunafungua milango ya biashara ya pande zote, si kudhoofisha.
Kushughulikia bandari ni jambo zuri, lakini si kisingizio cha kukataa ushirikiano mbalimbali. Ushirikiano wa kikanda unajenga nguvu pamoja. Kukosoa bila kuona fursa ni kudumaza maendeleo. Hoja yake inakosa uelewa wa biashara za kimataifa na inaonekana zaidi kama siasa kuliko uchambuzi wa kiuchumi.
Nahisi hiyo siyo taaluma yako na hujui uwezo wa DRC ktk kilimo. Anakuja kulima nini TZ? Mahindi na Mpunga? ardhi iko wapi? au kuwafukuza wenyeji kama alivyofanya Mkapa na kulima miwa kwa kiwanda cha Mtibwa?Hii sio kweli. Tanzania ina fursa zake na Congo ina fursa zake. Raia wa Congo anaweza kuja hapa na akawekeza kwenye kilimo hata kama kwao ipo ardhi.
Labda tuponde serikali kwenye mapungufu ya sera, sheria, ukusanyaji kodi, urasimu na taratibu za uwewekezaji ila hichi unachokisema hapa sioni kama ni sahihi kwa maoni yangu.
Fursa za Tz ni kuharibu matokeo ya kura.Hii sio kweli. Tanzania ina fursa zake na Congo ina fursa zake. Raia wa Congo anaweza kuja hapa na akawekeza kwenye kilimo hata kama kwao ipo ardhi.
Labda tuponde serikali kwenye mapungufu ya sera, sheria, ukusanyaji kodi, urasimu na taratibu za uwewekezaji ila hichi unachokisema hapa sioni kama ni sahihi kwa maoni yangu.
Kama imealikwa serikali ya Congo kuwekeza upo sawa, ila kama ni wafanyabiashara it's all about mfanya biashara husika na fursa anayoitafuta.Nahisi hiyo siyo taaluma yako na hujui uwezo wa DRC ktk kilimo. Anakuja kulima nini TZ? Mahindi na Mpunga? ardhi iko wapi? au kuwafukuza wenyeji kama alivyofanya Mkapa na kulima miwa kwa kiwanda cha Mtibwa?
Achana na madhaifu ya ccm. Hoja yangu inapinga kwamba hakuna namna mtu kutoka Congo anaweza kutaka kuwekeza Tanzania kwenye kilimo. Si kweli maana fursa hazifanani. Wanaweza kuwa na ardhi yenye rutuba kutuzidi ila mfanyabiashara akawa na malengo ambayo rutuba pekee haitoshi na hayo malengo anayaona yakiwezekana Tanzania 🇹🇿.Tuache kuhamisha ujamaa wa CCM na kuamini fikra sahihi ndo mafanikio ya nchi.
Fursa za Tz ni kuharibu matokeo ya kura.
Kama unaifahamu DRC huwezi hata tetea maelezo ya aina hiyo. DRC, nchi nzima inapata equatorial rain. wewe TZ sehemu kubwa ni semi-arid. Ukitaka kuwekeza na umwagiliaji hiyo ni mabilioni. DRC haihitaji ujinga huu!
Unasahau sana mkuuTatizo la Heche anajionaga ana akili sana kuliko yoyote, 2010 halmashauri ya tarime ilikuwa chini ya chadema na yeye akiwa diwani, hakuna cha maana chochote walichofanya.
Kama eneo dogo tu wilaya kachemka nchi nzima ataiwezea wapi?
Ndo maana nikasema hii siyo taaluma yako. Unachofanya ni kuandika nadharia za darasani; Hayo mambo ya agri-tourism.Kama imealikwa serikali ya Congo kuwekeza upo sawa, ila kama ni wafanyabiashara it's all about mfanya biashara husika na fursa anayoitafuta.
Mfano, Mtu anaweza kuja kuwekeza kwenye kilimo sababu anataka kuingia kwenye utalii kupitia kilimo, agri-tourism na akaona Tanzania 🇹🇿 ipo hiyo fursa. Kuhusu ardhi si utaratibu wa wageni kumiliki upo? Labda uhoji udhaifu wa huo utaratibu.
Achana na madhaifu ya ccm. Hoja yangu inapinga kwamba hakuna namna mtu kutoka Congo anaweza kutaka kuwekeza Tanzania kwenye kilimo. Si kweli maana fursa hazifanani. Wao wanaweza kuwa na ardhi yenye rutuba kutuzidi ila mfanyabiashara akawa na malengo ambayo rutuba pekee haitoshi na hayo malengo anayaona yakiwezekana Tanzania 🇹🇿.
Akisha vuta bangi lake la Tarime anachojuwa ni kuropoka tu kama kuku mwenye kideri anavyoharishaTatizo la Heche anajionaga ana akili sana kuliko yoyote, 2010 halmashauri ya tarime ilikuwa chini ya chadema na yeye akiwa diwani, hakuna cha maana chochote walichofanya.
Kama eneo dogo tu wilaya kachemka nchi nzima ataiwezea wapi?
Samia aliposema ana macho yaliyolegea, ulimkumbusha taarabu kwamba kapigwa pasi?Kuna wapumbavu huko CHADEMA kila akiongea wanampongeza kuwa ana akili sana. Kumbe ni kiazi mbatata tu
Umejikita kwenye udhaifu wa ccm, hoja yangu haipo huko.Ndo maana nikasema hii siyo taaluma yako. Unachofanya ni kuandika nadharia za darasani; Hayo mambo ya agri-tourism.
CCM lazima waambiwe waache ujinga ktk nchi. Lazima itumike lugha kali. Nchi iko hovyo kuliko unavyoamini. Uwezo wa viongozi ni mdogo kuliko unavyoaamini. Rais anatafuta misaada wao wanasema rais anatafuta wawekezaji, anapendwa, bhla! bhla! Anasimama jukwani kujisifia macho kulegea, hakuna anayemwambia ni ujinga maana huna makalio.
Kama JF nao tutaanza kusifia yasiyowezekana wao pembeni wanacheka wakiamini wako salama kichwani.
Mentor wenu na mshauri mkuu wa Tundu na CHADEMA anasema hivi;-Umeathirika na nidhamu za woga kwa viongozi. Ni hivi, kiongozi anayeingia madarakani kwa wizi wa kura na mauaji hana heshima yoyote. Huwezi kuingia madarakani kwa njia za kishenzi, kisha utake heshima. Hilo moja.
La pili, hivi tuko serious kuwaita wacongo kuja kuwekeza kwenye kilimo, au hayo yalikuwa ni mengineyo? Nakumbuka 1998 wakati Mkapa wanafufua Jumuiya ya Africa mashariki, walikubaliana kuwa na sarafu ya pamoja, hilo limewezekana hadi leo? Kama serekali na hao majirani hawana cha kukubaliana si wakae kimya tu?