Kauli ya Heche kukosoa Congo kuwekeza Tanzania ina ufinyu wa uelewa

Kauli ya Heche kukosoa Congo kuwekeza Tanzania ina ufinyu wa uelewa

Mzee kuna muda unaandika mashudu 100%. Tukianza na kauli ya kusema viongozi hawana maarifa wala akili ni kauli sahihi kabisa. Ulitaka atumie neno gani kuelezea uhalisia wa “upeo” wa hao viongozi kwa kushangilia Congo kuwekeza nchini? Yaani Congo awekeze Tanzania! Kwa kipi? Kama ana huo mtaji kwa nini asiwekeze kwao?

Kwamba anaipenda Tanzania kuliko nchi yake? Kwamba Congo hakuna ardhi ya kuwekeza kwenye kilimo? Mie naungana na Heche kuwa tunaongozwa na vilaza. Ila mie naenda hatua moja zaidi kwa kusema hata wewe ni kilaza promax kwa kukubali huu upuuzi wa watawala
Mwenyezi Mungu atuepushe na wapinzani wa aina hii wasio na ufahamu wa kupambanua mahusiano ya nchi mbili zaidi ya ujuaji kama huu. Sasa huyu anashindwa kujua kuwa Tanzania na DRC wameingia kwenye ushirikiano wa kimkakati wenye kunufaisha pande zote mbili.

Ni mpuuzi pekee anayeweza kufanya uchambuzi kama huu wa Heche kwa relevance ya Uchumi wa DRC katika Dunia ya leo.

Yarabi tuepushie na domokaya anayejua kula fedha za wahindi.
 
Sema Mzala anatumia Lugha kali sana ila ni kweli DRC hawawezi kutushauri au kufanya uwekezaji wa aina yeyote ya chakula Tanzania labda walete mtaji sisi tulime kwao wanaagiza kila kitu kutoka Nje hapo Kasumbalesa truck ni za chakula,mafuta na copper zinazotoka kwao viongozi wengi DRC wanapelekewa chakula na hizo bus za kwenda Congo..
Kilimo ni pesa, wapo wakongo matajiri na wanauwezo wa kuja kuwekeza hapa Tanzania, Heche aache kudanganya watu, Kwani Nigeria wana technology ipi mbona Dangote anawekeza kila kukicha ? Heche ana mawazo ya kitumwa kichwani mwake, dunia haipo hivyo acha upotoshaji.
 
Nawe unajiandikia ujinga-ujinga tu! Wewe leo hii unavyoona kuna nani serikalini mwenye akili?
Samia alipokwenda Russia uliambiwa faida ni kuwekeza kwenye Mahoteli. Huyo ni kiongozi au mzaha wa akili? Mahoteli ndo yanamsafirisha rais?

Hali ya hewa na ubora wa ardhi Congo ukilinganisha na Tanzania, unawezaje kumshwishi mtu aje kulima Tanzania? Rubbish!
Huu uzi siyo saizi yako, hata sijui ulichoandika. Uwekezaji ni fedha tu
 
View attachment 3653552

Kauli ya Heche inaleta dharau isiyostahili kwa viongozi wa Taifa. Kuwaambia “hakuna watu wenye akili na maarifa” si hoja, ni matusi yanayodhalilisha taifa badala ya kujenga. Uongozi una majukumu magumu; kukosoa kwa lugha ya kejeli hudhoofisha heshima ya nchi.

Kwa uwekezaji wa kutoka nje, teknolojia ni mojawapo tu. Mtaji ndiyo msingi mkuu, bila pesa hakuna kitu. Soko kubwa, utulivu wa kisiasa, sera nzuri, miundombinu, na motisha ya kodi ni muhimu zaidi. Mwekezaji wa Congo anaweza kuleta mtaji wake na kununua au kuleta teknolojia. Congo ina madini mengi na idadi kubwa ya watu, soko linalokaribiana nasi. Kuwaalika katika kilimo, uvuvi na madini kunafungua milango ya biashara ya pande zote, si kudhoofisha.

Kushughulikia bandari ni jambo zuri, lakini si kisingizio cha kukataa ushirikiano mbalimbali. Ushirikiano wa kikanda unajenga nguvu pamoja. Kukosoa bila kuona fursa ni kudumaza maendeleo. Hoja yake inakosa uelewa wa biashara za kimataifa na inaonekana zaidi kama siasa kuliko uchambuzi wa kiuchumi.
Mwendo kasi mlishindwa kununua Uganda, zimekufa za wachina. Leo jirani ndio aje kufanya nini?
 
Ila heche anawapigisha jaramba sio mchezo na awe makini tu nahisi Kuna jambo mbogamboga mnalitengeneza kwa heche maana sio kawaida kwa CCM kuona mnakosolewa alafu muache kuwatuma wale watekaji wakiZanzibar
 
kwa mfumo wa tanzagiza jinsi ulivyo kuongoza halmashauri hakuna maana yoyote ile kwa maana power yote iko kwa mkuu wa wilaya na mkuu wa mkoa hapo kuna waziri sijui wa tamisemi mpka waziri mkuu wakati mwingine hao wote wanaingiliana na haijulikani mpaka ulipo, angalia mfano tu mambo anayofanya chalamila huko dar, je ni jukumu lake au la meya? katiba inasemaje khs hilo? madiwani wako wapi? mipaka iko wapi ni wapi power ya meya inaanzia na kuishia na mkuu wa wilaya na mkuu wa mkoa je?

i mean, kwa tanzagiza kumhukumu meya au sijui mwenyekirti wa halmashauri kwa kushindwa kwa halmashauri au mji kufanya vizuri siyo fair kwa maana serikali ina overrides kila kitu, hivyo tumia kipimo kingine kumpima lkn siyo kuongoza halmashauri tanzagiza.

na ndiyo maana katiba mpya inapaswa iangalie mambo kama haya ili kama chama kikishinda umeya na kuongoza halmashauri basi hiyo halmashauri kweli iiwe huru na chini yao na kuondoa mambo ya mkuu wa wilaya, mkoa au sijui tamisemi au mipaka iwekwe kikatiba kabisa, juzi tu hapa nimesikia kitila mkumbo anazifokea halmashauri sasa yeye kama nani? kwa power ipi? ...
Muundo wa uungozi tz upo clear kabisa na unafahamika, viongozi ngazi za wilaya na mkoa wana kofia kadha kadha kulingana na muktadha wa eneo.

Madiwani wanapokuwa ktk vikao vya council wanakuwa wamevaa kofia ya ubunge na Mwenyekiti wa council/mayor anakuwa na kofia ya uspika, katika bunge hili la wilaya wana mamlaka ya kupanga bajeti na jinsi gani ya kutumia mapato yao ya ndani. Baada ya maazimio ya bajeti mkurugenzi mtendaji anavua kofia ya ukatibu wa bunge na kuvaa kofia ya uwaziri mkuu na ndiye anawajibika kusimamia utekelezaji wa bajeti bila kuingiliwa na dc wala rc.

Councillor na ded hawana mamlaka na vyombo vya ulinzi na usalama so katika utekelezaji wa majukumu wakikumbana na kikwazo kinachohitaji nguvu ndo humuona dc au rc ambao ndo wenyeviti wa kamati za ulinzi na wana kofia za urais katika maeneo yao.

So asaiv unamwona chalamila kama anaingilia majukumu ya mayor, si kweli mayor keshakaa na wajumbe wake ktk baraza wakabaini mapato ya jiji upande wa usafiri yamepangua so soln ni stand ya magufuli itumike ipasavyo ili tuweze kukusanya, baada ya wajibu wao ndo wamepeleka maazimio ktk kamati ya ulinzi ishughulike na kuingiza Mabasi ndo hapo sasa mwenye kamati yake chalamila anatamba, lkn pia mayor na ded wake watatamba kwenye kamati yao ya fedha na mipango kwa kusanya mapato humo stand na kuyapangia kazi ya kufanya bila kuingiliwa na dc au rc.

Kwa ufafanuzi huu mdogo naomba sasa kauli yako ya kumtetea heche uifute.
 
Mkuu, embu tulia kidogo, weka uccm au uchadema pembeni kama upo halafu jiulize kwanini raia wa Congo asiweze kuwekeza Tanzania?

Kama ingekuwa kama hivi usemavyo kila mtu angekaa nchini kwake maana hata hizo nchi kubwa zenye mitaji sio kwamba mitaji haiitajiki kwao ndo maana wanaipeleka nje. Watu wao bado wanahitaji ajira, Mabank yanahitaji pesa n.k n.k

Au tuachane na nchi, jiji la Dar, Lina raia wangapi kutoka mikoani ni wafugaji? Mikoa wanapotoka si kuna ardhi ya kufugia? Au Tanga, hakuna watu wanatoka dar wanaenda kufungua duka Tanga? Tanga ina nini cha kuipa Dar?
Leo wale matajiri wa Mt Meru Oil kutoka Arusha ni wawekezaji wakubwa kwenye biashara ya mafuta nchi za Zambia, Malawi na DRC. Vivyo hivyo Bakhresa amewekeza Kenya, Uganda, Malawi na South Africa.

MoDewji anaingia Mozambique, Rostam Aziz yupo Kenya, South Sudan SA na Dubai.

Lake Oil yupo Dubai, Kenya na South Sudan.

Acheni kumsikiliza huyu fisadi wa hela za ToneTone amelewa bangi
 
Kama tunashindwa kwashawishi hakina Tilisho hadi wanapigwa pingu kwa masuala madogo, hatuna viongozi ila tuna kundi fulani akili zinafanana
Tilisho ni nani asipigwe pingu? Pingu haziangalii una hela ngapi!!
 
Kilimo ni pesa, wapo wakongo matajiri na wanauwezo wa kuja kuwekeza hapa Tanzania, Heche aache kudanganya watu, Kwani Nigeria wana technology ipi mbona Dangote anawekeza kila kukicha ? Heche ana mawazo ya kitumwa kichwani mwake, dunia haipo hivyo acha upotoshaji.
Unamfananisha Dangote na wakongo aisee hakuna Mkongo atafanya uwekezaji wa kilimo labda watu kutoka Zimbabwe na mataifa mengine...
Nendeni mkajifunze kilimo cha ngano Zimbabwe hapo wao ndio wazalishaji wakubwa wa ngano Afrika na kwa Duniani wanashika nafasi za juu na ni zao la biashara hilo..
 
Mentor wenu na mshauri mkuu wa Tundu na CHADEMA anasema hivi;-

View attachment 3653635 Wewe Tindo ni nami UMBISHIE?
Kwamba hatuna uwezo wa kuelewa bali lazima tumsikilize Kitima? Huyo Kitima huwa yuko upande wa haki, na wala sio kwamba anawaza kwa niaba yetu. Tutamuunga mkono kwenye lililo kweli, sio hilo la kusema tutii washenzi. Yeye kama yeye amuheshimu, sisi wengine tunaheshimu wanaojiheshimu.
 
Ndo maana nikasema hii siyo taaluma yako. Unachofanya ni kuandika nadharia za darasani; Hayo mambo ya agri-tourism.

CCM lazima waambiwe waache ujinga ktk nchi. Lazima itumike lugha kali. Nchi iko hovyo kuliko unavyoamini. Uwezo wa viongozi ni mdogo kuliko unavyoaamini. Rais anatafuta misaada wao wanasema rais anatafuta wawekezaji, anapendwa, bhla! bhla! Anasimama jukwani kujisifia macho kulegea, hakuna anayemwambia ni ujinga maana huna makalio.

Kama JF nao tutaanza kusifia yasiyowezekana wao pembeni wanacheka wakiamini wako salama kichwani.
Nyie endeleeni kuponda lakini Tanzania inakuwa sana kiuchumi na kimiundombinu katika kipindi hiki kuliko Marais waliomtangulia
 
Unasahau sana mkuu
" Si magufuri alikua anasema MKICHAGUA WAPINZANI SIWALETEI MAENDELEO
Kuna mapato ya ndani na ya serikali kuu, bado alikuwa na nafasi ya kushawishi madiwani bajeti zao ziweje kuchochea maendeleo bila kutegemea chanzo cha serikali kuu.
 
Unamfananisha Dangote na wakongo aisee hakuna Mkongo atafanya uwekezaji wa kilimo labda watu kutoka Zimbabwe na mataifa mengine...
Nendeni mkajifunze kilimo cha ngano Zimbabwe hapo wao ndio wazalishaji wakubwa wa ngano Afrika na kwa Duniani wanashika nafasi za juu na ni zao la biashara hilo..
Kwanini tukajifunze ngano Zimbabwe wakati tunazalisha mahindi mengi na ni kati ya top 3 producers wa mahindi pamoja na SA na Nigeria
 
Kuna mapato ya ndani na ya serikali kuu, bado alikuwa na nafasi ya kushawishi madiwani bajeti zao ziweje kuchochea maendeleo bila kutegemea chanzo cha serikali kuu.
Unamkumbuka magufuri alivyo kua untouchable ( MKICHAGUA WAPINZANI SIWALETEI MAENDELEO) kauli ya ki huliganii

Unajua mkuu wa mkoa na wakuu wa wilaya na mkurugenzi mtendaji wa halmashauri

Ingia YouTube tafuta postcad ya m&s (mjenga na Salma Dakota) mahojiano na mbunge MWITA WAITARA atakujibu swali ulilo niuliza
 
Ajibiwe kwa hoja kama alivyojibu yeye
 
View attachment 3653552

Kauli ya Heche inaleta dharau isiyostahili kwa viongozi wa Taifa. Kuwaambia “hakuna watu wenye akili na maarifa” si hoja, ni matusi yanayodhalilisha taifa badala ya kujenga. Uongozi una majukumu magumu; kukosoa kwa lugha ya kejeli hudhoofisha heshima ya nchi.

Kwa uwekezaji wa kutoka nje, teknolojia ni mojawapo tu. Mtaji ndiyo msingi mkuu, bila pesa hakuna kitu. Soko kubwa, utulivu wa kisiasa, sera nzuri, miundombinu, na motisha ya kodi ni muhimu zaidi. Mwekezaji wa Congo anaweza kuleta mtaji wake na kununua au kuleta teknolojia. Congo ina madini mengi na idadi kubwa ya watu, soko linalokaribiana nasi. Kuwaalika katika kilimo, uvuvi na madini kunafungua milango ya biashara ya pande zote, si kudhoofisha.

Kushughulikia bandari ni jambo zuri, lakini si kisingizio cha kukataa ushirikiano mbalimbali. Ushirikiano wa kikanda unajenga nguvu pamoja. Kukosoa bila kuona fursa ni kudumaza maendeleo. Hoja yake inakosa uelewa wa biashara za kimataifa na inaonekana zaidi kama siasa kuliko uchambuzi wa kiuchumi.
Naunga mkono hoja , heche hana hoja

Kutumia kauli zinazoshambulia utu au uwezo wa kiakili wa viongozi badala ya kujenga hoja kwenye sera au maamuzi yao hubadilisha mjadala kutoka kuwa wa kiundani (substance) na kuwa wa kiuhasama (personal attacks). Lugha ya staha huongeza uzito wa ukosoaji na kulinda mshikamano wa kitaifa.
 
Unamkumbuka magufuri alivyo kua untouchable ( MKICHAGUA WAPINZANI SIWALETEI MAENDELEO) kauli ya ki huliganii
Hiyo ni kauli tu, hata wabunge wengine ktk majimbo yao si kwamba walikuwa wanatimiziwa kero zao kwa 100% wengi tu wabunge wa CCM kero zao hata kwa 30% hazikutimizwa bali walikuwa wanacheza na mapato yao ya ndani kupitia halmashauri zao.
 
Back
Top Bottom