Nsanzagee
JF-Expert Member
- Jun 28, 2023
- 2,209
- 4,769
Ni kauli ya mh Rais mstaafu Kikwete aliyowahi kuitoa katika moja ya vikao vya viongozi wa CCM akisema
CCM, haina mpango wa kuweka mgombea mwingine kwenye uchaguzi ujao (2025) labda mambo yaharibike zaidi
Ndugu watanzania, Tanzania ni nchi yetu sote, kumchagua mtu ili awe Rais wetu, ni watanzania wote tumemwamini ili akasimamie kile wananchi tumemtuma
Kunapotokea mambo hayaendi sawa, si busara kwa kiongozi huyo kuendelea kuwepo kwenye nafasi hiyo, ni vema kupisha ili wengine waje watupeleke tunakotaka kwenda
Wananchi tunataka kuishi kwa kuifurahia nchi yetu na matunda yale Mungu ametupatia yachochee kwa wepesi uchumi wetu na yasaidie kutupunguzia ukali wa maisha
Nchi yoyote Duniani, viongozi wake wanaojinasibu kwamba nchi zao zinapiga hatua kimaendeleo, maana yake utakuta, kuna unafuu wa ghalama za maisha kwa watu wa nchi zao yanajitokeza
Tofauti na hapo, maana yake nchi haipigi hatua yoyote ya kimaendeleo, na zaidi sana utakuta uchumi unashikiliwa na watu wachache walio kwenye mnyororo wa viongozi huku wananchi wakiwa kama ngazi ya wao kuwafikisha wanapotaka
Tukisema kwamba tupo sawasawa tu, sote tunajidanganya na hakuna mwenye faida katika udanganyifu wetu huu!
Mimi ninajiuliza maswali hapa
Madini yote tumewapa wageni
Mbuga za wanyama kwa sehemu nazo tumewapa
Bahari na banddari nazo tumewapa kwa sehemu
Gesi nayo tumewapa
Mapori ya misitu nayo tumetoa
Mwendo kasi pia
Ikitokea Rasilimali zote tumewapa wageni, na kwa kuwa viongozi wa kiafrica nchi bila rasilimali hujiona kama wapo jangwani na hawana akili ya kugeuza jangwa kuwa kitu kinachozalisha, itakuwaje huko tuendako?
Hakutakuwa na mzozo mkubwa?
Licha kwamba rasilimali zetu nyingi tumewapa wawekezaji, lakini ndio kwaanza umasikini ndio unazidi kuwa mkubwa
Bado tunataka tuendelee na viongozi wasio na majibu ya watoto wetu?
Kauli ya Kikwete 2025 ifanye kazi