Kauli ya Magufuli kuwa Kabudi na Lukuvi hawatagombea Urais haikuwa ya ghafla, ilipangwa siku nyingi na ndio mwanzo wa mgogoro ndani ya CCM

Tulia dawa ipenye
 
Atakaye pita ni yule amabaye anatakiwa na mkuu, mwenye maamuzi ni yule mwenye dola
 
Tangu lini Urais unaamuliwa na kura za wananchi?

Sent from my Infinix X653 using JamiiForums mobile app
 
Acheni kufananisha uraisi na vitu vya kijinga kama Kabudi,
Unatakiwa uwe realistic. Angalia historia ya uraisi wa nchi hii kwamba ni Mkapa tu ndie ilipangwa rasmi awe raisi. Uraisi wa Mwinyi ulikuwa accident baada ya kugoma kuchomoa jina lake kumpisha Salim Ahmed Salim - na baada ya wajanja kumwondoa Sokoine kimaajabu; uraisi wa Kikwete ulilazimishwa baada ya kutishia angegombea na upinzani na kuiangusha CCM ikiwa wangemweka Salim Ahmed Salim au Mwandosya; uraisi wa Magufuli alikuwa accident baada ya mgongano wa Kikwete kumtaka Membe na wajumbe kumtaka Lowasa. Hakuna raisi wa kupangwa Tanzania, ilitokea mara moja tu kwa Mkapa, na yeye bila Nyerere Mrema angekuwa raisi.
 
Mwinyi asifikiri Tanzania ni nchi ya kisultani, atuondokee huko. Tanzania sio kichwa cha mwendawazimu cha kujaribishia watu uraisi. Kwanza katika maraisi wote waliopita yeye ndie alikuwa the most ineffective leader, hata watu walikuwa hawamwogopi wala kumheshimu kila mtu anajifanyia la kwake, na Wahindi wakawa ndio wanaendesha TRA na nchi. Ikulu likawa pango la wafanya biashara. Hatutaki damu hiyo ikulu, watu ambao hawawezi hata kumkatalia kitu mke japo kinahusu kuongoza nchi.

In fact, wakati Mwinyi akiwa raisi, yeye mwenyewe kwa maneno yake alikuwa akimsema huyu mtoto wake Mwinyi raisi wa Zanzibar kuwa yuko weak, hajui hata ku-socialize. Alikuwa anamsifia mdogo wake. Aje hapa Mwinyi tumkumbushe.
 
Kwani Rais ajaye wa TZ 'anachongwa' na Rais aliyepo madarakani? Kumwandaa Rais ajaye hufanywa na 'watu' mbalimbali na wengine hutumiwa kumwandaa Rais ajaye bila wao kujua..
Rais ajaye atapatikana 'in what will appear to be either a very natural or coincidental process'..
 
Mkuu, ukiondoa Mwinyi, hakuna raisi ambaye hajawahi kuwa na mtu wake tangu Nyerere, japo huwa hawafanikiwi mara nyingine
  1. Baada ya awamu ya Kwanza Nyerere alitaka sana Sokoine amrithi - wajanja wakamuondoa. Kisha akataka Salim Ahmed Salim. Zanzibar wakawa hawamtaki Salim, wakamchomeka Mwinyi
  2. Mwisho wa awamu ya pili, Mwinyi hakuwa na powers za kumweka mrithi mbele ya Nyerere, hivyo Nyerere akamweka Mkapa
  3. Mkapa alitaka sana Omar Juma amrithi, maajabu yakatokea. Kisha akaamua basi itakuwa Salim, lakini Kikwete akamtishia kufanya mapinduzi ya kuiua CCM, ikabidi Mkapa asalimu amri amuweke Kikwete kwa makubaliano maalum
  4. KIkwete alitaka kumweka Membe, wajumbe wa NEC wakamtaka Lowasa, Magufuli akaangukiwa na ngekewa - vita vya panzi kunguru akafaidi!
 
Aiseeee [emoji4][emoji4][emoji4]
 
'Fair enough' Mkuu Synthesizer lakini Rais Magufuli hakuangukiwa na ngekewa kama wengi wanavyoamini('at least' yeye ana amini hivyo) lakini aliandaliwa.. Ijapokuwa anaweza asijue moja kwa moja..
Kwa kifupi jaribu kuangalia sheria zilizopitishwa haraka haraka kabla ya uchaguzi wa Rais wa 2015..'statistics act 2013' ,'The Access to Information Act, 2015','Cyber crime act 2015','The media Services Act,2015 etc..
 
Swali aliandaliwa na nani?

Sent from my Infinix X653 using JamiiForums mobile app
 
Hapa Mzee Alikosea.
Hata yeye hakujua alipitaje pitaje mpaka akawa Mgombea wa CCM 2015.
Yeye mwenyewe alisema Urais hupangwa na Mungu. Sasa vipi kawa msemaji wa Mungu?

Ni vzr akajenga umoja wa kitaifa, upendano na udugu kwa kipindi hiki alichobakiza. Huku akijitahidi na kujiandaa kustaafu vizuri.
 
Safu ya CCM 2025
1st preference =Majaliwa
2nd = Jafo
3rd= none
4th= none
Ni zamu ya Rais Muislamu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…