Kauli ya Magufuli kuwa Kabudi na Lukuvi hawatagombea Urais haikuwa ya ghafla, ilipangwa siku nyingi na ndio mwanzo wa mgogoro ndani ya CCM

Kauli ya Magufuli kuwa Kabudi na Lukuvi hawatagombea Urais haikuwa ya ghafla, ilipangwa siku nyingi na ndio mwanzo wa mgogoro ndani ya CCM

Kama unaongelea aliyosema kwa wafanya kazi wake wa wizara ya mambo ya ndani, lengo lilikuwa ni mbali zaidi. Amejionyesha wazi jinsi gani yeye ni kiongozi bora zaidi hasa katika kushughulika na mambo ya kimataifa, kuifanya Tanzania iheshime nk. Huyu sio yule mtu anaesema nimeokotwa jalalani, ndio maana nikasema huwa anaamua kujishusha ili akwezwe
Tulia dawa ipenye
 
Siku Magufuli alipotamka hadharani kwamba Kabudi na Lukuvi hawatagombea uraisi kwa sababu ya umri wao mkubwa, wengine walicheka wakiichukulia kama ni kauli ya ghafla. La hasha, hii ilikuwa ni kauli ya kimkakati ambayo Magufuli alikuwa ameitafakari na kupanga kuisema kabla hata ya kuingia uchaguzi Mkuu.

Ni kauli ambayo iliwashangaza sana Kabudi na Lukuvi, kuwashitua, kuwakatisha tamaa na hatimae kuwaudhi sana. Ilibidi tu wajichekeshe mbele za watu.

Magufuli ameitoa kauli hiyo akiwa amesoma wazi nia za Kabudi na Lukuvi kutaka kuwa maraisi wajao. Ukiangalia kwa makini, Kabudi na Lukuvi wamekuwa waaminifu sana kwa Magufuli, wakiwa nyuma yake kwa 100%, wakimpamba kila wanapopata nafasi, na lengo lao ilikuwa kupata kuungwa mkono na Magufuli ili kuwa raisi awamu ifuatayo. Kuna wakati mtu kama Kabudi anajitoa kabisa maarifa na akili (wisdom and intelligence) ili mradi tu ajiweke upande wa Magufuli na Magufuli amuone ndio Waziri anaefaa kuwa raisi ajaye.

Sasa kwa kauli hii Magufuli amefanya kosa kubwa sana. Ametangaza vita na mgogoro ndani ya CCM katika suala la raisi atakaemrithi. Magufuli ameishaanza kumpigia debe "kijana" anaetaka amrithi, kijana ambae Magufuli ataweza kumtawala (kum-influence) kirahisi wakati amemaliza awamu hii. Na watu wanajua ili Magufuli awe na "mrithi" wa kumtawala, lazima awe ni kijana wake mtiifu kabisa kama vile Makonda, au kijana wa kutoka kanda ya ziwa.

Sasa ndani ya CCM kuna watu wameanza kuliona hilo na hawataki kabisa! Kuna watu wanaona Lukuvi au Kabudi ndio mawaziri "wenye hekima na busara" wanaofaa kumrithi Magufuli.

Magufuli amekuwa na haraka mno kuanzisha vita ya wa raisi ajayo, akidhani kuwakatisha tamaa mapema Kabudi na Lukuvi itasaidia kuwaondoa uwanja wa mapambano. Magufuli alipaswa ajifunze toka kwa Kikwete, ambaye alijua kabisa Mwandosya alitaka kuwa kumrithi kiti cha uraisi, na Kikwete akajifanya kumuunga mkono Mwandosya hadi dakika za mwisho kabisa ndio akatoa majina yake mfukoni. Mwandosya akawa amepigwa knock out kwa " sucker punch" hakuamini betrayal ya Kikwete! Sidhani hata kama hata wanasalimiana hadi leo. Kikwete mtoto wa mjini, Magufuli mtu wa kuja, ndio tofauti zao.

Sasa athari za Magufuli kuonyesha karata zake mapema ni kwamba ile support aliyopata toka kwa Kabudi na Lukuvi katika awamu ya kwanza hataipata tena! Hilo ndilo kosa kubwa Magufuli amefanya. Sasa Kabudi na Lukuvi hawatampta tena ile 100% waliyompa huko nyuma. Kibaya sana kinachoweza kutokea ni kwamba wataunda makundi yao ndani ya CCM ya kuwa support, lengo likiwa kupanda mbegu ndani ya watu wa CCM kwamba Magufuli ni kiongozi asie na hekima hata kumuunga mkono juu ya chaguo lake la raisi ajae itakuwa ni kosa kubwa!

Kwangu mimi, Hotuba ya Kabudi aliyotoa kwa wafanya kazi wa mambo ya ndani ina kila namna ya viashiria kwamba ameanzamapambano na kujitofautisha ili watu waone anaweza kuwa raisi wa namna gani!

Yajayo ndani ya CCM yatafurahisha sana. Mpambano ndio kwanza unaanza!
Atakaye pita ni yule amabaye anatakiwa na mkuu, mwenye maamuzi ni yule mwenye dola
 
CCM wataweka mgombea wa uraisi kutoka visiwani wakijua kwa uhakika kwamba wamekubuhu katika namna mbalimbali za kuiba kura hata washindwe vipi watageuza matokeo. La sivyo siku wanaweka mgombea wa visiwani kuwania uraisi ndio siku upinzani watachukua nchi, maana hata Zanzibar watampigia mpinzani ili akipita avunje muungano
Tangu lini Urais unaamuliwa na kura za wananchi?

Sent from my Infinix X653 using JamiiForums mobile app
 
Acheni kufananisha uraisi na vitu vya kijinga kama Kabudi,
Unatakiwa uwe realistic. Angalia historia ya uraisi wa nchi hii kwamba ni Mkapa tu ndie ilipangwa rasmi awe raisi. Uraisi wa Mwinyi ulikuwa accident baada ya kugoma kuchomoa jina lake kumpisha Salim Ahmed Salim - na baada ya wajanja kumwondoa Sokoine kimaajabu; uraisi wa Kikwete ulilazimishwa baada ya kutishia angegombea na upinzani na kuiangusha CCM ikiwa wangemweka Salim Ahmed Salim au Mwandosya; uraisi wa Magufuli alikuwa accident baada ya mgongano wa Kikwete kumtaka Membe na wajumbe kumtaka Lowasa. Hakuna raisi wa kupangwa Tanzania, ilitokea mara moja tu kwa Mkapa, na yeye bila Nyerere Mrema angekuwa raisi.
 
Kuna memba humu alishaambia akaandika na uzi huu , Mahesabu makali ya Mzee Ally Hassan Mwinyi , mmesahau , alisema wakati wa kikao cha mkutano mkuu kuchagua mgombea urais ccm kuwa rais Magufuri aongeze muda wa miaka mitano , ili mwanae Hussein Mwinyi atimize miaka kumi Zanzibar ili baadaye aje amrithi Magufuri . Haya Sasa mnaiona hii coincidence ?
Mwinyi asifikiri Tanzania ni nchi ya kisultani, atuondokee huko. Tanzania sio kichwa cha mwendawazimu cha kujaribishia watu uraisi. Kwanza katika maraisi wote waliopita yeye ndie alikuwa the most ineffective leader, hata watu walikuwa hawamwogopi wala kumheshimu kila mtu anajifanyia la kwake, na Wahindi wakawa ndio wanaendesha TRA na nchi. Ikulu likawa pango la wafanya biashara. Hatutaki damu hiyo ikulu, watu ambao hawawezi hata kumkatalia kitu mke japo kinahusu kuongoza nchi.

In fact, wakati Mwinyi akiwa raisi, yeye mwenyewe kwa maneno yake alikuwa akimsema huyu mtoto wake Mwinyi raisi wa Zanzibar kuwa yuko weak, hajui hata ku-socialize. Alikuwa anamsifia mdogo wake. Aje hapa Mwinyi tumkumbushe.
 
Kwani Rais ajaye wa TZ 'anachongwa' na Rais aliyepo madarakani? Kumwandaa Rais ajaye hufanywa na 'watu' mbalimbali na wengine hutumiwa kumwandaa Rais ajaye bila wao kujua..
Rais ajaye atapatikana 'in what will appear to be either a very natural or coincidental process'..
 
Mkuu, ukiondoa Mwinyi, hakuna raisi ambaye hajawahi kuwa na mtu wake tangu Nyerere, japo huwa hawafanikiwi mara nyingine
  1. Baada ya awamu ya Kwanza Nyerere alitaka sana Sokoine amrithi - wajanja wakamuondoa. Kisha akataka Salim Ahmed Salim. Zanzibar wakawa hawamtaki Salim, wakamchomeka Mwinyi
  2. Mwisho wa awamu ya pili, Mwinyi hakuwa na powers za kumweka mrithi mbele ya Nyerere, hivyo Nyerere akamweka Mkapa
  3. Mkapa alitaka sana Omar Juma amrithi, maajabu yakatokea. Kisha akaamua basi itakuwa Salim, lakini Kikwete akamtishia kufanya mapinduzi ya kuiua CCM, ikabidi Mkapa asalimu amri amuweke Kikwete kwa makubaliano maalum
  4. KIkwete alitaka kumweka Membe, wajumbe wa NEC wakamtaka Lowasa, Magufuli akaangukiwa na ngekewa - vita vya panzi kunguru akafaidi!
 
Mkuu, ukiondoa Mwinyi, hakuna raisi ambaye hajawahi kuwa na mtu wake tangu Nyerere, japo huwa hawafanikiwi mara nyingine
  1. Baada ya awamu ya Kwanza Nyerere alitaka sana Sokoine amrithi - wajanja wakamuondoa. Kisha akataka Salim Ahmed Salim kwa utaratibu uliokuwapo wa kubadlishana uraisi. Zanzibar wakawa hawamtaki Salim, wakamchomeka Mwinyi
  2. Mwisho wa awamu ya pili, Mwinyi hakuwa na powers za kumweka mrithi mbele ya Nyerere, hivyo Nyerere akamweka Mkapa
  3. Mkapa alitaka sana Omar Juma amrithi, maajabu yakatokea. Kisha akaamua basi itakuwa Salim, lakini Kikwete akamtishia kufanya mapinduzi ya kuiua CCM, ikabidi Mkapa asalimu amri amuweke Kikwete kwa makubaliano maalum
  4. KIkwete alitaka kumweka Membe, wajumbe wa NEC wakamtaka Lowasa, Magufuli akaangukiwa na ngekewa - vita vya panzi kunguru akafaidi!
Aiseeee [emoji4][emoji4][emoji4]
 
Mkuu, ukiondoa Mwinyi, hakuna raisi ambaye hajawahi kuwa na mtu wake tangu Nyerere, japo huwa hawafanikiwi mara nyingine
  1. Baada ya awamu ya Kwanza Nyerere alitaka sana Sokoine amrithi - wajanja wakamuondoa. Kisha akataka Salim Ahmed Salim. Zanzibar wakawa hawamtaki Salim, wakamchomeka Mwinyi
  2. Mwisho wa awamu ya pili, Mwinyi hakuwa na powers za kumweka mrithi mbele ya Nyerere, hivyo Nyerere akamweka Mkapa
  3. Mkapa alitaka sana Omar Juma amrithi, maajabu yakatokea. Kisha akaamua basi itakuwa Salim, lakini Kikwete akamtishia kufanya mapinduzi ya kuiua CCM, ikabidi Mkapa asalimu amri amuweke Kikwete kwa makubaliano maalum
  4. KIkwete alitaka kumweka Membe, wajumbe wa NEC wakamtaka Lowasa, Magufuli akaangukiwa na ngekewa - vita vya panzi kunguru akafaidi!
'Fair enough' Mkuu Synthesizer lakini Rais Magufuli hakuangukiwa na ngekewa kama wengi wanavyoamini('at least' yeye ana amini hivyo) lakini aliandaliwa.. Ijapokuwa anaweza asijue moja kwa moja..
Kwa kifupi jaribu kuangalia sheria zilizopitishwa haraka haraka kabla ya uchaguzi wa Rais wa 2015..'statistics act 2013' ,'The Access to Information Act, 2015','Cyber crime act 2015','The media Services Act,2015 etc..
 
Swali aliandaliwa na nani?

Sent from my Infinix X653 using JamiiForums mobile app
 
Hapa Mzee Alikosea.
Hata yeye hakujua alipitaje pitaje mpaka akawa Mgombea wa CCM 2015.
Yeye mwenyewe alisema Urais hupangwa na Mungu. Sasa vipi kawa msemaji wa Mungu?

Ni vzr akajenga umoja wa kitaifa, upendano na udugu kwa kipindi hiki alichobakiza. Huku akijitahidi na kujiandaa kustaafu vizuri.
 
Safu ya CCM 2025
1st preference =Majaliwa
2nd = Jafo
3rd= none
4th= none
Ni zamu ya Rais Muislamu.
 
Back
Top Bottom