Makinikia yanasafirishwa nje Kama kawaida?Rais Samia Suluhu aliingia madarakani Machi 2021 hadi August 2021 tayari Tanzania kumekuja uwekezaji mkubwa zaidi ya miaka yote aliyokuwepo Magufuli madarakani. Mikataba yote iliyokwamishwa na Magufuli kama vile mkataba wa LNG, Bagamoyo port, Katanga Nickel na kadhalika, Rais Samia ameifanya imekuwa smooth na uwekezaji umekuwa zaidi. Tanzania ina more favorable investment environment kuliko Taifa lolote EA, sasa we endelea kula upupu kudhani kwamba katiba inaleta wawekezaji.
Hoja ya msingi ni ile inayohusu utawala wa sheria na wananchi kuweza kusimama kidete na kumwajibisha binadamu yeyote nchini anayevunja Katiba inayompa madaraka na sheria zitokanazo na Katiba iliyopo. Hayo ndiyo mazingira bora ya uwekezaji ambayo Walimwengu wanajua; na siyo sura ya mtu. Hivi kweli wote tunaishi dunia moja hii au kuna watu wanajitoa ufahamu !?Tuna matatizo sana vijana wa Kitanzania. Hakuna hata uhusiano kati ya Kingereza chake na akili zake, wala utajiri wake. Tunashinda kutilia maanani hoja za msingi tunahangaika na vitu petty. Haya nitajie mtu anayejua kiingereza zaidi halafu ni tajiri zaidi ya Mo, hapa Tanzania. Mnawaza kwa kutumia kitu gani?
alitekwa na Magu wakati wa MaguKwani nani amesema kuwa alitekwa magu? au nimesema kwamba alitekwa wakati wa magu?
Katika Qatar Economic Forum, moja kati ya wazungumzaji alikuwepo Mo Dewji, tajiri namba moja Tanzania na mbali ya hayo, ni moja kati ya hayo ni mtu ambaye amewekeza sana Tanzania na kutoa maelfu ya ajira kwa watanzania. Katika mazungumzo yake, alitoa kauli nzito sana na nzuri ambayo kama ni mtu wa kutazama kwa jicho la mbali, utaona kali hii ni mtaji mkubwa kwa Tanzania hasa katika kuleta uwekezaji zaidi Tanzania. Nanukuu.
"Now we have a new President, she a woman, a very very vibrant, she's doing a fantastic job, she's moving around the whole world. So-called the 'Royal Tour', we can already see the impact in terms of a huge influx of tourists bringing foreign revenues and a lot of investments coming into the country I think she's doing a fantastic job and Tanzania is ready to fly."
Kauli hii ukiisikiliza vizuri utajua tu hapa Mo amefanya jambo kubwa sana kwa Taifa lake. Sasa basi kwa nini narejelea kusema kwamba kauli ya Mo ni mtaji mkubwa sana kwa Taifa la Tanzania?
Kauli ya Mo itarejesha imani ya wawekezaji wenye mitaji mikubwa. Miaka kadha nyuma wakati wa JPM, kutokana na aina ya uongozi wake, imani ya wawekezaji ilishuka sana.
Hata kama wawekezaji walifika nchini, lakini waliwekeza fedha zao kwa woga sana kutokana na kutoeleweka kwa Serikali ya JPM aliyokuwa na maamuzi ya kushutukiza ambayo wawekezaji waliohofia pengine wangeteketeza mitaji yao. Kwa kauli ya Mo, kutokana na nafasi yake nchini Tanzania na fedha alizowekeza, ni wazi kwamba wawekezaji wa aina yake ambao Tanzania inawahitaji sana, wanaweza kuja Tanzania, kuwekeza na kuleta ajira zaidi kwa Watanzania.
Tujiulize, wakati wa Magufuli ambao Mo mwenyewe alitekwa kwa wiki kadhaa hata tusijue alikuwa wapi, mbona hakuwahi kusema popote pale kama eti, Magufuli ni Rais mzuri sana na kumpa sifa kedekede? Mnadhani Mo na ukubwa wake huko nje, na jopo la watu mashuhuri wanaojuana naye, mnadhani walifurahi yeye kupotezwa? Acha hiyo, vipi kuhusu imani zao juu ya kuja kuwekeza Tanzania, nchi ambayo mtu aina ya Mo, a million dollars rich anapotea tu kama Kuku.
Matajiri aina ya Mo wanalindwa Duniani kote. Mo ni mtu muhimu sana. Ameajiri zaidi ya watu 40,000 hapa Tanzania. Imagine afunge viwanda vyake vyote hao watu 40K Serikali itawabeba kwa mbeleko gani, kama sio kuongezeka tu kwa uhalifu. Tuseme tu Mo kwa sasa ana amani na furaha kuliko wakati wowote ule. Hiyo tu, inatosha sana kuonesha Dunia sasa Tanzania ni nchi ya aina gani, na hii ni faida kwetu kwani italeta wawekezaji zaidi na kutanua fursa za kibiashara Tanzania.
Ni wazi, hii isingewekezana bila uongozi thabiti na wenye maarifa wa Rais Samia Suluhu Hassan.
Kingereza sio mafanikio, wabongo bado tuko vibaya sana kwenye thinking.
WEWE WASEMA.alitekwa na Magu wakati wa Magu
Na bado. Zaidi ya makinikia yatasafirishwa, na sisi wenyewe tutanunuliwa bila ya kujitambua.Makinikia yanasafirishwa nje Kama kawaida?
Mirembe waongeze wodi zingine, Vichaa wanazidi mtaani.Hakuna wawekezaji wakubwa wanaweza kuja kuwekeza hapa Tanzania kwa katiba hii iliyopo.
Wawekezaji wakubwa siyo mbumbumbu. Wanajua kabisa kwamba katiba yetu inampa rais umungu mtu . Na haijulikani kama rais atakayefuata baada ya Samia atakuwa mungu mwenye roho safi ama mwenye roho mbaya kama jiwe.
Kwanini amteke Mo(ccm mwenzake) tu na si Bakhresa au tajiri mwengine?alitekwa na Magu wakati wa Magu
muulize mtekaji sio mimiKwanini amteke Mo(ccm mwenzake) tu na si Bakhresa au tajiri mwengine?
Hivi wakati wa Jiwe kuna mtu mwenye akili timamu aliwahi msifia?Wewe hujui watu wanaenda na upepo?
Ijue Tanzania na watanzania.
Kila Rais anasifiwa akiwa madarakani, akitoka, waliokua wanamsifia wanahamia kwa mpya.
...by imaginationI think she's doing a fantastic job
Kikubwa bwana yule kafaNa bado. Zaidi ya makinikia yatasafirishwa, na sisi wenyewe tutanunuliwa bila ya kujitambua.
Unakumbuka alipompigia kampeni simba day pale kwa mkapa mpaka kina lema wakataka kususia bidhaa zake?Wakati wa JPM Mo alimsifia kiasi ambacho anampamba Mama Samia?
Na mikataba iwe wazi wananchi waione na kutoa maoni yaoRais Samia ameifanya imekuwa smooth na uwekezaji umekuwa zaidi. Tanzania ina more favorable investment environment kuliko Taifa lolote EA, sasa we endelea kula upupu kudhani kwamba katiba inaleta wawekezaji.
sio sabuni tu hata juice zake ukinywa unajamba hovyo hovyoSawa tumekusikia,Ila mwambie Mo aache kutengeneza bidhaa hafifu, sabuni ya unga yamoto na ikufulia nguo zinapauka[emoji16][emoji16]
Wewe hujui watu wanaenda na upepo?
Ijue Tanzania na watanzania.
Kila Rais anasifiwa akiwa madarakani, akitoka, waliokua wanamsifia wanahamia kwa mpya.