Kauli ya Mo Dewji juu ya Rais Samia ni mtaji mkubwa kwa Tanzania

Kauli ya Mo Dewji juu ya Rais Samia ni mtaji mkubwa kwa Tanzania

Nimekuuliza kwanini amteke Mo na sio tajiri mwengine? Ukasema nimuulize aliyemteka ambaye mie sina ushahidi wa kwamba huyo mtu uliyemtuhumu ndio kweli alimteka hadi aweze kujibu kwanini alimteka Mo.
Kwani ni wapi iliwahi kuthibitika kwamba Mo alitekwa na JPM?
 
Umekimbia huko Twitter unakuja kuleta maneno yako huku, ukae kwa kutulia binti.
Kwani kuna mipaka ya kuwa katika mtandao wowote ule wa kijamii? Acheni hayo mambo, sidhani kwamba ni sawa kutamka maneno uliyotamka. Niko hadi Linkedn kama hujui na nakiwasha kama kawaida.
 
Kwani ujui kuwa waarabu mafisadi wanajambo lao ......kwa kumtumia sa100 hadi sasa team msoga imeanza kuvurugana na team sultani...japo ni kwambali
Waarabu gani tena? au ulitaka kusema kwamba Mo ni Mwarabu? heheh
 
Waarabu gani tena? au ulitaka kusema kwamba Mo ni Mwarabu? heheh
Sultan unawajua ...ni wale masultan wenye kumchukia Nyerere kuliko vitu vyote ndiyo walio zuia hotuba za nyerere zisisikike popote tanzania ....sasa kama unayo akili utawajua
 
dada yangu huwajui matajiri sasa hivi wapo free wanaiba wanavyoweza biashara zote haramu zimerudi kuliko awamu zoote duniani. kwa sasa hivi hakuna tajiri atakaeponda wote watamsifia mamy, ona baharesa alikuwa anapataka magogoni akanyimwa awamu zilizopita naona kuna figisufigisu kafanya sasa kaingia anahudumia mwisho atamiliki yeye
Nashauri aondoke boti zake watu waogelee mpaka ng'ambo ya pili
 
Katika Qatar Economic Forum, moja kati ya wazungumzaji alikuwepo Mo Dewji, tajiri namba moja Tanzania na mbali ya hayo, ni moja kati ya hayo ni mtu ambaye amewekeza sana Tanzania na kutoa maelfu ya ajira kwa watanzania. Katika mazungumzo yake, alitoa kauli nzito sana na nzuri ambayo kama ni mtu wa kutazama kwa jicho la mbali, utaona kali hii ni mtaji mkubwa kwa Tanzania hasa katika kuleta uwekezaji zaidi Tanzania. Nanukuu.

"Now we have a new President, she a woman, a very very vibrant, she's doing a fantastic job, she's moving around the whole world. So-called the 'Royal Tour', we can already see the impact in terms of a huge influx of tourists bringing foreign revenues and a lot of investments coming into the country I think she's doing a fantastic job and Tanzania is ready to fly."

Kauli hii ukiisikiliza vizuri utajua tu hapa Mo amefanya jambo kubwa sana kwa Taifa lake. Sasa basi kwa nini narejelea kusema kwamba kauli ya Mo ni mtaji mkubwa sana kwa Taifa la Tanzania?

Kauli ya Mo itarejesha imani ya wawekezaji wenye mitaji mikubwa. Miaka kadha nyuma wakati wa JPM, kutokana na aina ya uongozi wake, imani ya wawekezaji ilishuka sana.

Hata kama wawekezaji walifika nchini, lakini waliwekeza fedha zao kwa woga sana kutokana na kutoeleweka kwa Serikali ya JPM aliyokuwa na maamuzi ya kushutukiza ambayo wawekezaji waliohofia pengine wangeteketeza mitaji yao. Kwa kauli ya Mo, kutokana na nafasi yake nchini Tanzania na fedha alizowekeza, ni wazi kwamba wawekezaji wa aina yake ambao Tanzania inawahitaji sana, wanaweza kuja Tanzania, kuwekeza na kuleta ajira zaidi kwa Watanzania.

Tujiulize, wakati wa Magufuli ambao Mo mwenyewe alitekwa kwa wiki kadhaa hata tusijue alikuwa wapi, mbona hakuwahi kusema popote pale kama eti, Magufuli ni Rais mzuri sana na kumpa sifa kedekede? Mnadhani Mo na ukubwa wake huko nje, na jopo la watu mashuhuri wanaojuana naye, mnadhani walifurahi yeye kupotezwa? Acha hiyo, vipi kuhusu imani zao juu ya kuja kuwekeza Tanzania, nchi ambayo mtu aina ya Mo, a million dollars rich anapotea tu kama Kuku.

Matajiri aina ya Mo wanalindwa Duniani kote. Mo ni mtu muhimu sana. Ameajiri zaidi ya watu 40,000 hapa Tanzania. Imagine afunge viwanda vyake vyote hao watu 40K Serikali itawabeba kwa mbeleko gani, kama sio kuongezeka tu kwa uhalifu. Tuseme tu Mo kwa sasa ana amani na furaha kuliko wakati wowote ule. Hiyo tu, inatosha sana kuonesha Dunia sasa Tanzania ni nchi ya aina gani, na hii ni faida kwetu kwani italeta wawekezaji zaidi na kutanua fursa za kibiashara Tanzania.

Ni wazi, hii isingewekezana bila uongozi thabiti na wenye maarifa wa Rais Samia Suluhu Hassan.
Kumbe Mo naye ni msanii ....!! Yaani Royal Tour tayari inaleta watalii .... seriously. Hivi ni watalii wangapi wanapanga safari ndani ya miezi mitatu?? Mpaka sasa hiyo movie ya Maza huko Amazon ni watu wangapi ambao wameiangalia mpaka sasa ....... Hii precedence aliyotuachia JPM ya kusifia kila kitu cha Mwenyekiti inatupeleka kubaya na sijui tutamalizana nayo kivipi!!
 
Tuna matatizo sana vijana wa Kitanzania. Hakuna hata uhusiano kati ya Kingereza chake na akili zake, wala utajiri wake. Tunashinda kutilia maanani hoja za msingi tunahangaika na vitu petty. Haya nitajie mtu anayejua kiingereza zaidi halafu ni tajiri zaidi ya Mo, hapa Tanzania. Mnawaza kwa kutumia kitu gani?
Wanawaza kwa kutumia tumbo.
 
Back
Top Bottom