Kauli ya mwisho ya marehemu rafiki yangu ilikuwa tusi la nguoni. Je, ataenda mbinguni?

Kauli ya mwisho ya marehemu rafiki yangu ilikuwa tusi la nguoni. Je, ataenda mbinguni?

Kwani nani anajua roho humtoka mtu wakati gani? Pengine alipogongwa wakati anakata roho alijitubia zake dhambi zake.
 
Mwaka jana rafiki yangu akiwa amepakiza familia yake kwenye gari binafsi alipata ajali ba kufariki hapohapo.

Kwa ufupi ni kwamba kuna lori lilifeli break likawa linakuja kasi upande wake yeye akidhani ni mbwembwe za dereva wa lori

Lori lilipomkaribia akatoa tusi ile anamalizia herufi o tu, lori likamgonga upande wake na kufariki hapohapo.

Mimi sikuwepo niliadithiwa na waliokuwemo kwenye gari.

Sasa wale wafia dini huyu mtu siku ya kiana atakuwa upande upi?

Ni amri ipi ya Mungu inasema usitukane?
Kwa hiyo kwa akili zako tukufu unadhani kuwa angesema yesu au muhammad angeingia peponi 🙄🙄🙄🙄 labda pepo za kina mwamposa kakobe na gamanywa na ngwajima na wale mashehe mandazi na maustadhi vitumbua ila siyo pepo ya Mwenyezi mungu mtakatifu wa watakatifu.
 
Unazungumziaje swala la mtu kongonoka? Je ni dhambi au siyo dhambi maana wote wanasikia raha
Dhambi maana yake ni tendo baya ambalo mtu hufanya kwa kujua ni tendo baya, na anaamua kulifanya kweli. Dhambi Ina vipengele vitatu: kukusaidia, kuamua na kufanya/tenda. Katika mahusiano dhambi hutokea kama wahusika wanalenga kutumiana (exploitation of each other). Kumbuka hapo juu nimesema (dhambi ina madhara kwa mtu mwenyewe, mtu mwingine au jamii). Katika mahusiano ambayo wahusika hawana intention ya kuwa pamoja maisha yao yote, dhambi hutokea kwa sababu wanajihusisha kwenye mahusiano yasiyo ya kweli/yasiyo na kibali machoni pa Mungu/ya kudanganyana na kutumiana kama vyombo vya anasa (fornication, adultery). Kuna athari kwa wahusika na kwa jamii (yaani kutumia viungo vya wahusika kinyume na makusudio yake). Ni kama mtu asiye na madaraka/mamlaka ya kufanya jambo fulani alifanye kama mwenye madaraka/mamlaka nalo. Anayefanya hivyo anatenda kosa (hata kama kufanya hivyo kunamfurahisha au kunawafurahisha baadhi ya watu au hata watu wote maana if one person can make a wrong, even all people can do so). Lazima tujifunze kufanya mambo ambayo tuko authorised/tuna kibali nayo na tukifanya hivi tunafanya ndani ya utaratibu. Kufanya mambo nje ya utaratibu hata kama kufanya hivyo kunamfurahisha mtu, kuna matokeo hasi kwetu wenyewe au kwa watu wengine. Lazima kwenye mahusiano tuji'envolve' kwenye 'genuine relationships' (mahusiano yenye kibali machoni pa Mungu). Hapo tutakuwa tumeepuka dhambi. Hivyo, kabla ya kufanya jambo lolote tujiulize: je, jambo hili lina kibali machoni pa Mungu? Kama jibu ni ndiyo endelea nalo, na kama jibu ni hapana, achana nalo.
 
Kwa Waislam, hukumu zetu ni Allah ajuwaye, hakuna binadam ajuwaye. Wajibu wetu ni kufanya toba.
Kea hiyo nasheikh wanatudanganya kusema tukitenda hivi titaipns pepo na tukitenda hivi ni motoni
 
Kea hiyo nasheikh wanatudanganya kusema tukitenda hivi titaipns pepo na tukitenda hivi ni motoni
Hapo bado sijakuelewa, wakisema "hivi" ndiyo vipi? Au "tukitenda hivoi" ndiyo vipi? Sijakuelewa.

Kiislam, tunaamini kuwa Mwenyezi Mungu ndiye mwenye kukubali toba zetu, siyo Sheikh wala binadam mwengine yeyote.

Qur'an ipo "crystal clear" kwenye mafundisho yake.

Ukiuliza maswali yanayohusu Uislam, Kuwa "specific" ili tukuelewe na tukupe jibu litalokufanya uuelewe Uislam. Hakuna kukisia katika Uislam.
 
Ila honestly hivi vitu tunafundishwa sio poa.....

Muda si mrefu kijana wangu kaja ananiambia "mama siku ya mwisho ya kiama watu wote tutasimama kutakua na moto, ambae haji moto utamfata na hapo tutasimama kwa miaka elf tano"

nikamjibu tu "mwanangu nenda kaoge sasa"

Ni nini hiki lakini
Umemjibu vyema usimvuruge ubongo wake bado mdogo si unaona hata kuoga mpaka useme.
 
Hapo bado sijakuelewa, wakisema "hivi" ndiyo vipi? Au "tukitenda hivoi" ndiyo vipi? Sijakuelewa.

Kiislam, tunaamini kuwa Mwenyezi Mungu ndiye mwenye kukubali toba zetu, siyo Sheikh wala binadam mwengine yeyote.

Qur'an ipo "crystal clear" kwenye mafundisho yake.

Ukiuliza maswali yanayohusu Uislam, Kuwa "specific" ili tukuelewe na tukupe jibu litalokufanya uuelewe Uislam. Hakuna kukisia katika Uislam.
Mfano mtu amekufa akitenda dhambi mfano yuko anazini akapata presha akafa ghafla bila kupata wasaa wa kuomba toba,mtu huyu ataenda wapi
 
Mzazi weka mambo sawa!
Ila honestly hivi vitu tunafundishwa sio poa.....

Muda si mrefu kijana wangu kaja ananiambia "mama siku ya mwisho ya kiama watu wote tutasimama kutakua na moto, ambae haji moto utamfata na hapo tutasimama kwa miaka elf tano"

nikamjibu tu "mwanangu nenda kaoge sasa"

Ni nini hiki lakini
 
Lori lilipomkaribia akatoa tusi ile anamalizia herufi o tu, lori likamgonga upande wake na kufariki hapohapo
Nimewaza ni tusi gani la nguoni linaishia na "o" nimeshindwa kubaini, itabidi niongeze juhudi kwenye kujifunza haya Mambo
 
Back
Top Bottom