UPOTOSHAJI JUU YA KAULI YA PAPA FRANCIS NA KANISA LA ROMAN CATHORIC KUHUSU NDOA ZA JINSIA MOJA NA TAARIFA ZA VYOMBO VYA HABARI
Papa akajibu; ".....Hatutakiwi kuwauwa wala kuwatenga na akasema,inapotokea watu wanaojihusisha na usagaji,ushoga na usenge wameenda Kanisani wasifukuzwe wala kuadhibiwa kwa kuuliwa bali ni kazi ya Kanisa kuwapokea na kuwaombea ili wabadilike na kumrejea mwenyezi Mungu..."
Kama Papa alijibu hivi, then, bila hata kujitetea saaana hapa ndugu
deblabant, kumbe ni kweli haina maana ya kuwa Kanisa Katoliki limerihusu ndoa za jinsia moja...
Pamoja na kuwa haya ni maoni yake binafsi Papa lakini pia huu ndio ukweli wenyewe ya namna ambayo kanisa linapaswa kumtendea mwenye dhambi yeyote anapokuwa ndani ya kanisa. Dhambi si ushoga na usagaji tu. Makanisani na misikitini kuna waongo, mafisadi, wezi, waongo, watukanaji nk nk. Wote hawa wanalihitaji kanisa kuwasadia kubadili mienendo yao mibaya na kushika mwenendo mwema na mpya...
Kama makanisa yatakuwa na utamaduni wa kuwatenga au kuwanyanyapaa wenye dhambi, basi hiyo itakuwa ni kwenda kinyume na mafundisho ya injili ya Yesu Kristo na Kwa namna hii maana yake ni kusema kuwa Yesu Kristo hakuwa na maana kuja kuuokoa ulimwengu..
Yesu Kristo mwenyewe katika maisha yake na huduma yake hapa duniani alikuwa ni rafiki wa wenye dhambi wote. Kamwe hakuwahi kumnyanyapaa mwenye dhambi awaye yeyote aliyekuja kwake..
Katika kitabu cha Yohana sura ya 8, tunamuona Yesu akiwa ameletewa mwanamke mmoja na wafia dini wakimshitaki kwa kutumia sheria ya Musa (TORATI) ya kuwa amefumaniwa akifanya uzinzi na kwa mujibu wa sheria hiyo eti mtu wa namna hiyo hupigwa kwa mawe mpaka afe. Wakamuuliza wewe Yesu unasemaje?
Yesu aliwajibu jibu rahisi sana lililowatawanya wote mmoja mmoja na akabaki mwanamke peke yake akiwa na Yesu. Aliwaambia;
"....
ni kweli, sheria ya Musa inasema hivyo. Hata hivyo, mimi nataka yeyote miongoni mwenu mnaomshitaki mama huyu ambaye hana dhambi, basi awe wa kwanza kumtupia jiwe mwanamke huyu.."
Kwa jibu hilo, mmoja baada ya mwingine aliondoka bila kuaga kuthibitisha kuwa kumbe hata wao walikuwa na dhambi kubwa na pengine nyingi na mbaya zaidi kuliko ya huyu mama...!
Ndivyo ilivyo hata kwa sisi leo. Tuna tabia ya kuwahukumu wengine zaidi kuliko kujiangalia na kujihurumia sisi kwanza.
Watu wamekomaa tukidhani ubaya au dhambi ni ushoga na usagaji tu. Tunasahau Kila mtu ni mwenye dhambi (uchafu) katika kiwango na range yake...
Kanisa linalowanyanyapaa mashoga na wasagaji hilo sio kanisa la Yesu Kristo. Kazi ya kanisa ni kurekebisha tabia za watu. Ni kubadilisha tabia za watu kutoka kwenye mwenendo mbaya na kuwaongoza kwenda kwenye mwenendo mwema unaokubalika mbele ya Mungu Kwa kutumia mafundisho ya injili ya Yesu Kristo..
Kanisa halibariki mwenendo mbaya. Kanisa linawakaribisha wote wenye mwenendo mbaya katika jamii mfano: mashoga, wasagaji, watukanaji, majambazi, wezi, wauaji, mafisadi, wazinzi, waasherati, wachoyo, wabinafsi, wakorofi, wapiga waume su wake zao nk nk na kanisa litawabadilisha na kuwa watu wema..
Asante