Kauli ya papa na upotoshaji wa BBC makusudi

Mbona wafiraji unawapenda, iweje uwachukie wake zao? 😆
wafiraji na wafirwaji wote sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. hii ndio mauti ya pili. mwogopeni Mungu. na hii inajumuisha wote, wanawake wanaofirwa, wanaume wanaofirwa, na wanaume wanaofira wanaume na wanawake. hukumu ipo juu yenu.
 
acha upumbavu bhn hivi n sanamu ndo zimekupumbaza au sasa nenda kwenye website ya vatican washaweka taarifa radmi....afu uje tena kivingne......
 
Tatizo waandishi wengi wa kisasa hawako imformed na hawafanyi utafiti. Kabla ya kuandika na kushabikia uzushi kama huo mwandishi anapaswa kujua taratibu za kanisa katoliki, kama papa anao uwezo wa kutoa uamuzi mkubwa kama huo kupitia mahojiano tu.
Pili nini tafsiri sahihi ya neno la kiingereza blessing?
 
Labda wanafikiri dhambi ni ushoga na usagaji tu!!, Kama hata uongo, wizi, ukahaba na mengine maovu mengi basi tutawafukuza wote kanisani, daima tambua kanisa ni la wenye dhambi,
Kwa sisi wakristo kwenye biblia Yesu aliulizwa kwa nn anashinda na kula na wenye dhambi?? Akawajibu wenye afya hawahitaji tabibu bali wagonjwa, sasa kama utawafukuza msaada wataupata wapi, inabidi wawe karibu na kanisa ili waongoke


MWISHO MWENYE KUHUKUMU NI MUNGU PEKEE SIO BINADAMU, MSIJIPE MAMLAKA HAYO, KUMBUKENI WENGINE HUONGOKA SIKU YA MWISHO YA KIFO CHAO, MWENYEZI MUNGU AWAONGOZE
 
Shida kanisa letu Lina endeshwa na brains kubwa Sasa wenye brain ndogo kama wewe au nyie hamtalielewa kamwe. Mtawaelewa akina mwamposa na mafuta ya kukanyaga tu. Shida ni elimu ndo shida kubwa
Papa kalegeza misimamo ya ushoga..
Kasema mapadri wawabariki mashoga lakini nje ya kanisa..
Kama kuwabariki nje ya kanusa sio kitu kikubwa kwanini ametoa ruhusa?
Wazungu huwajui wewe
Ushoga kwao ni utamaduni
 
Kwa hiyo CNN, BBC, Times wote wamekosea mkuu na hawakuelewa vizuri?
 
Acheni kumtetea PAPA,amekosea kweli, na mnahitaji Papa mwingine. huyu kawaharibia sana.

Ni wapuuzi na waongo ndio wanaweza kusambaza au hata kuamini kuwa Papa ameruhusu ndoa za jinsia moja. Ni uwongo mkubwa.

Papa alichosisitiza ni kuwa ushoga ni dhambi lakini siyo jinai kiasi cha mtu hao watu kuadhibiwa kwa kufungwa au kuuawa. Kanisa Katoliki halina utaratibu wa kuwaadhibu watenda dhambi, bali linasisitoza toba.

Tena kwa kukazia zaidi alisema kuwa ndoa ni kati ya mume na mke tu. Hayo mambo ya ushoga inaweza kuwa ni union tu lakini haiwezi kuitwa ni ndoa.
 
Wewe unajua maana ya neno "blessing" kwa wakatoliki?
We utatafsiri na kuchambua vitu kuliko hao native English speaker.
Yani sawa na mzungu aseme anaelewa kiswahiki kuliko native speakers...
 

Kama Papa alijibu hivi, then, bila hata kujitetea saaana hapa ndugu deblabant, kumbe ni kweli haina maana ya kuwa Kanisa Katoliki limerihusu ndoa za jinsia moja...

Pamoja na kuwa haya ni maoni yake binafsi Papa lakini pia huu ndio ukweli wenyewe ya namna ambayo kanisa linapaswa kumtendea mwenye dhambi yeyote anapokuwa ndani ya kanisa. Dhambi si ushoga na usagaji tu. Makanisani na misikitini kuna waongo, mafisadi, wezi, waongo, watukanaji nk nk. Wote hawa wanalihitaji kanisa kuwasadia kubadili mienendo yao mibaya na kushika mwenendo mwema na mpya...

Kama makanisa yatakuwa na utamaduni wa kuwatenga au kuwanyanyapaa wenye dhambi, basi hiyo itakuwa ni kwenda kinyume na mafundisho ya injili ya Yesu Kristo na Kwa namna hii maana yake ni kusema kuwa Yesu Kristo hakuwa na maana kuja kuuokoa ulimwengu..

Yesu Kristo mwenyewe katika maisha yake na huduma yake hapa duniani alikuwa ni rafiki wa wenye dhambi wote. Kamwe hakuwahi kumnyanyapaa mwenye dhambi awaye yeyote aliyekuja kwake..

Katika kitabu cha Yohana sura ya 8, tunamuona Yesu akiwa ameletewa mwanamke mmoja na wafia dini wakimshitaki kwa kutumia sheria ya Musa (TORATI) ya kuwa amefumaniwa akifanya uzinzi na kwa mujibu wa sheria hiyo eti mtu wa namna hiyo hupigwa kwa mawe mpaka afe. Wakamuuliza wewe Yesu unasemaje?

Yesu aliwajibu jibu rahisi sana lililowatawanya wote mmoja mmoja na akabaki mwanamke peke yake akiwa na Yesu. Aliwaambia;

"....ni kweli, sheria ya Musa inasema hivyo. Hata hivyo, mimi nataka yeyote miongoni mwenu mnaomshitaki mama huyu ambaye hana dhambi, basi awe wa kwanza kumtupia jiwe mwanamke huyu.."

Kwa jibu hilo, mmoja baada ya mwingine aliondoka bila kuaga kuthibitisha kuwa kumbe hata wao walikuwa na dhambi kubwa na pengine nyingi na mbaya zaidi kuliko ya huyu mama...!

Ndivyo ilivyo hata kwa sisi leo. Tuna tabia ya kuwahukumu wengine zaidi kuliko kujiangalia na kujihurumia sisi kwanza.

Watu wamekomaa tukidhani ubaya au dhambi ni ushoga na usagaji tu. Tunasahau Kila mtu ni mwenye dhambi (uchafu) katika kiwango na range yake...

Kanisa linalowanyanyapaa mashoga na wasagaji hilo sio kanisa la Yesu Kristo. Kazi ya kanisa ni kurekebisha tabia za watu. Ni kubadilisha tabia za watu kutoka kwenye mwenendo mbaya na kuwaongoza kwenda kwenye mwenendo mwema unaokubalika mbele ya Mungu Kwa kutumia mafundisho ya injili ya Yesu Kristo..

Kanisa halibariki mwenendo mbaya. Kanisa linawakaribisha wote wenye mwenendo mbaya katika jamii mfano: mashoga, wasagaji, watukanaji, majambazi, wezi, wauaji, mafisadi, wazinzi, waasherati, wachoyo, wabinafsi, wakorofi, wapiga waume su wake zao nk nk na kanisa litawabadilisha na kuwa watu wema..

Asante
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…