Kauli ya Rais kwa waandishi 'Wapara' kuwa wakimpara "Atawaparua", Je Rais Samia ni katili?, Soma Jinsi ya kuwabaini makatili!. Ni kutumia macho tu!.

Mwanamke katili hawezi kuishi na mme, sifa ya kwanza
 
Mkuu P asalam aleikhum. Hebu tafakari tena hii nukuu.

“Power tend to corrupt and absolute power currupts absolutely. Great men are almost always bad men”(John Dalberg-Acton)

Hata huku kwetu pia tuna usemi wa “Madaraka hulevya” na hii huanza taratibu.

Mama achukue tahadhari.

Maneno yanaumba iwe kwa jicho la tatu au la nne!
 
Angeanza kuwapara mafisadi walioripotiwa kwenye ripoti ya CAG Ili tujue ana maanisha
 
Kuna tofauti gani akifanya ukatili kwa kutumia sheria kandamizi au physical assault kwa wahusika?Vyote hivyo ni ukatili kwa mtazamo wa jicho la tatu kama ulivyoeleza kupitia bandiko refu kama hilo.Ukatili ndani ya CCM umekuwa ni jadi tangia baada ya Mwl Nyerere.
 
Mkuu ukatili upo wa iana nyingi, hata kuruhusu mfumuko wa bei bila sababu za msingi ni ukatili mkubwa sn
 
"Ukinizingua tunazinguana" Mungu atupe nini? baada ya yule Mhutu Katili Mungu katupa Mama Samia ambae hana makuu..I love you my President.
 
Rakini! kure Kwetu Mara kure! Unadhani vimakucha tu vitapara majitu sugu vire?? yare ukitaka kuyaweza Mama yangu yare majitu hayasikii ukirimabia hvivi kesho rinarudia sasa fanya hivi yanataka, ''Kata funua twende kazi''

hapo mtaenda sana...yanaLugha yao hivi.... yakutiana Moyo sasa wakisikia hivo nimwendo wakasi ya uahlifu tyuuu! daa Taraime/SERENGETI Bhana!! kure siyo Tanzaznia kabhisa! uongo Mleta Mada???
 
Kwa vile leo ni birthday ya Rais Samia, nawaomba wana jf wote ambao ni well wishers, tuungane kumu wish Happy Birthday this lovely lady Rais wetu mpendwa, Rais wetu mpenzi, Rais wetu kipenzi, Rais Dr. Samia Suluhu Hassan, Chifu wa kabila kubwa kuliko makabila yote Tanzania, ambayo Kanda ya kabila hilo ndio Kanda determinant ya kura za urais wa JMT, Chifu Hangaya.
Happy Birthday.

P
 
Leo ndio siku yenyewe ya wanawake duniani, hongera sana kwa wanawake wote duniani akiwemo Mwanamke huyu!.
P
 
Broo P nimekuelewa Sasa Kwa yanayokuja?!!!

Kweli wewe kionambali
 
Waandishi wa habari hawajawahi kuwa huru, uhuru wao ni ukweli na ukweli ni sumu kwa watawala. Ni safari ndefu na ngumu kupata uhuru wanaouhitaji katika nchi zetu za Kiafrika ambazo viongozi wake wengi wanaongozwa na uchu na ubinafsi.

Mahali ambapo watu wapo tayari kutengeneza vita Kwa ajili ya maslahi ya mtu fulani au kikundi fulani tu cha watu. Kalamu na karatasi ni silaha hatari sana kwao. Habari na taarifa sahihi kuwa wazi kwa umma kwao ni mkosi mkubwa.

Mahali ambapo mtawala anatamani kuwaaminisha watu wote kuwa rangi nyeusi ni nyeupe na nyeupe ni nyeusi Mwandishi wa habari hawezi kuwa salama Kwa sababu Ili habari iwe habari sharti imfurahishe mtawala. Uhuru wa waandishi wa habari utatoa mwanya wa wasuopenda kuguswa " godfathers" kuguswa.

Uhuru wa waandishi wa habari utavuruga kabisa ule wimbo hususani kwenye korasi tuna imani naye. Watawala wa Kiafrika wanapenda kiitikio hiki kimbwe na wote, uhuru wa wanahabari unaweza kusababisga kiitikio hiki kutoimbika vizuri na wote.

Tunajitaji jamii huru kabla ya kuwa na wanahabari huru, wanahabari hawatokei katika ombwe ila ni zao la jamii. Waandishi hawawezi kuwa huru kama jamii haijawa huru.
 
Ni kwa vipi jamii inakuwa huru ??
 
Ni kwa vipi jamii inakuwa huru ??
Ni pale viongozi wanapoamini kwa dhati kuwa uongozi walionao wamedhaminiwa na wanajamii na pia wanajamii wanapokuwa na uwezo wa kuhoji mamlaka walizoziweka juu ya mambo mbalimbali yanayotendeka au yanayopangwa.

Ni pale wanajamii wanapokuwa na uwezo wa kiuchumi na kuweza pia kusimamia njia zao za uchumi pasi na tofauti kubwa ya kiuchumi kati ya watawala wa kisiasa na wanajamii. Uhuru huo huifanya siasa kuwa uhusiano wa kimamlaka tu " power relation" na siyo uwanja wa kujitajirisha na kujilimbikizia ukwasi.

Uhuru wa jamii ni pale utajiri unapokuwa hali ya jamii na siyo silaha ya tabaka fulani dhidi ya jingine. Uhuru wa jamii ninaousema ni zaidi ya uhuru wa kujieleza unafikia mawanda ya uhuru wa kufikiri. Ni pale ambapo kila mtu anakubali kwa dhati kuwa yeye ni zao la jamii na sehemu ya jamii.
 
Je unadhani tunawezaje kuifikia hali hiyo uliyoieleza vizuri kabisa ??!

Wapo kweli wenye dhamira hiyo ??! I mean from those who are holding the four aces !
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…