Kauli ya Sean Paul imewashtua wengi baada yakusema hamjui Diamond wala Alikiba alipotua Tanzania, ila anatamani kufanya nao kazi

Kauli ya Sean Paul imewashtua wengi baada yakusema hamjui Diamond wala Alikiba alipotua Tanzania, ila anatamani kufanya nao kazi

Hauwezi kujua wasanii wote.....Marobot ya views wanawadanganya sana wasanii wetu.
 
Wakuu

Mwanamuziki maarufu wa dancehall kutoka Jamaica, Sean Paul, aliwasili Tanzania jana (Novemba 29) kwa ajili ya show yake inayotarajiwa kufanyika leo. Katika mahojiano na Bongo 5, alipoulizwa kuhusu Diamond Platnumz, Sean Paul alikiri kwamba hamfahamu msanii huyo lakini yuko tayari kukutana na kushirikiana na wasanii wa Kitanzania.
View attachment 3165814
Kauli hii iliwashtua mashabiki wengi, kwani baada ya wapekuzi kufukunyua mambo ikajulikana kwamba msanii hao amem-follow Diamond kwenye mtandao wa Instagram.
View attachment 3165811
Sean Paul amekuwa na ushirikiano na wasanii mbalimbali duniani, ikiwa ni pamoja na wimbo maarufu “Rockabye” alioshirikishwa na Clean Bandit na Anne-Marie.
View attachment 3165810
Kauli yake ya kutowafahamu miamba wa muziki Bongo Simba na King Kiba, ina funzo kwa muziki wetu?
View attachment 3165824
Mimi Isingenishangaza kabisa kwani najua kuwa wanamuzuiki wa Tanzania hawafahamiki kabisa katika sehemu nyingi za dunia kwa sababu siyo wabunifu wa nyimbo zinazohit. Wao wanategemea sana promotion za kufanya collaboa na wanamuziki wa Marekani, DRC na Nigeria bila kujua kuwa anayekuwa anafahamaika hapo ni huyo aliyemshirikisha, siyo yeye mwenyewe. Halafu nyimbo za wanamuziki wetu nyingi zinadumu muda mfupi sana. Mtu kama Lucky Dube alikuwa anajulikana kwa ajili ya muziki wake siyo kwa ajili ya alioshirikiana nao, na Muziki wa Dube hadi leo unahit pamoija na yeye mwenye kuuwawa zaidi ya miaka 16 iliyopita. Lakini uakiangangalia Muziki wa mwanamuzuki yeyote wa kitanzanzania wa kizazi hiki uliotolewa miaka mitanio ilyopita hausikilizwi tena na hakuna anayeujua nje ya Tanzania hata kama ulitumia wanamuziki wa nje kupata promosheni ilikuwa no boom ya muda mfupi tu ukafifia.
 
Back
Top Bottom