Uchaguzi 2020 Kauli ya Sheikh Ponda yakanushwa na wahadhiri wa Dini ya Kiislam

Uchaguzi 2020 Kauli ya Sheikh Ponda yakanushwa na wahadhiri wa Dini ya Kiislam

Hizi njaa mbaya saana hata hawajasikia nini aliongea kwa kuwa wapo kwenye payroll ya CCM wanafanya lolote kumridhisha Boss wao.
 
Haya maugoro nenda kalishane na mabeki tatu wenzako.

Unawadharau mabaharia wewe, angalia asije kukuungia mboga na haja kubwa kubwa na ndogo ndogo ukirudi jioni ukaishia kujilamba vidole kwa utamu. Wape heshima yao mmoja ni mwasisi wa hii imani Ponda na Lissu wanayo jaribu kuihujumu na kuichafua.
 
Yule sheikh ponda naye anazeeka vibaya.

kama mwanazuoni na mtu mwenye ushawishi hakutakiwa ajipe jukumu la kuwasemea waislamu wote.bado alipaswa awawekee mzani wa kuchagua.

hii tabia za viherehere sijui hata zimeubukia wapi!!!!!
 
Hao wachumia tumbo wangeamua kukaa kimyaa ndio ingekuwa busara zaidi kuliko kuongea ongea hovyo.

BAKWATA ni tawi la CCM hilo linajulikana muda tu.

Sisi wa Sheikh PONDA ISSA PONDA tunasema Kila mpenda haki 28/10/2020 KURA zote kwa TUNDU LISU full Stop.
 
Hongera ponda hawa akina kipozeo hawajapigwa risas na hawajuwi kua kuna waislaam wanateswa kwa Sababu ya CCM
 
Hawa masheikh wote wanakula kitimoto sioni jipya kutoka kwao.....alafu watanzania wa Leo sio wajinga wanajua Hali ya siasa unayoendelea nchi
 
Ponda sio mufti, hana mamlaka ya kuwazungumzia waislam wa Tanzania, mwambieni awe anajizungumzia mwenyewe.
Afadhali ya Ponda,kuliko yule mufti wa Bakwata, maana Tanzania hakuna Mufti
 
Sidhani Kama Itakua Sahihi Yeye Kuwaongelea Waislam Ikiwa Sio Kiongozi Rasmi...
Issa Ponda Ni Mwanazuoni Mzuri Lakini Mihemko ya Kisiasa Imekua Ikimchukua Mara Kwa Mara Na Kuifanya Elimu Aliyonayo Kuwa Useless Kwa Hapa Hapana Ajipange Na Waislam Sio Wakupelekwa Hivo!!

Masheikh wakiisifia CCM hawana mihemko ya kisiasa, lakini wakiikubali Chadema wana mihemko ya kisiasa.
 
Bado tunaendelea kufuatilia ile spika ya pale Kawe ya kuomba kwa jina la Mtume S.A.W na jina na Yesu ule waya ulitokea wapi? Tumefikia hatua nzuri Ponda endelea kusema zaidi ili hawa vipenyo uchwara wajitokeze zaidi
 
Haya mambo yabkuingiza dini kwenye siasa bila exit plan, ndo yameifanya dini ya kiislamu kuhusishwa na ugaidi kwa muda mrefu sana hapa duniani. Kuna wapuuzi wachache wameibadilisha sana taswira ya uislam, Cha ajabu wengine ni viongozi kabisa.

Halafu baadae mtaanza kusema kwamba ni propaganda za watu wa magharibi kuuchafua uislam. Haya bwana kwahiyo waislam msiposhinda kwenye huu uchaguzi itakuwaje Sasa🤔!
Ponda kashaagiza waisilamu wapenda haki wapigie kura upande wa haki. Tunasubiri tume isiyo huru ya uchaguzi ichezee matokeo ya kweli ili tujue tunatokaje hapa.
 
Sheikh Ponda ndiye kiongoxi wa waislaum wa Tanzania, shuguli ya ile kamati yake inajulikana nchi nzima, piga spana, pigaaa spanaa ma CCM adi yakimbie bila mwano
Unapiga spana tarehe 28 unapigwa kifo cha mbwa koko,
 
Ila wahadhiri hao hao wanakubaliana na Sheikh Alhadi Salum kuwananga wapinzani na kuiombea CCM na Maghufuli miaka mitano tena?! Unafiki asili yake Uswahili
 
Haya ndio madhara ya kukosekana kwa haki.

Ponds keshaumizwa sana, wakati mwingine anaongea kwa uchungu sana.

Mkija kuumiziwa ndugu zenu ndo mtaelewa umuhimu wa Haki.

Mimi na familia yangu October 28 kama ni mapumziko na kupiga kura ni bure basi tutamchagua TUNDU LISSU.
 
Back
Top Bottom