Kauli ya tafuta hela, inapotosha vijana.

Kauli ya tafuta hela, inapotosha vijana.

Inatakiwe isomeke na ieleweke kuwa ni tafuta kazi na si tafuta hela; ili kuweza kudumisha maadili na afya za vijana.

Kwa sababu kazi ndio chanzo cha kupata hela.

Hii ya kutafuta hela, ndio inapelekea vijana wengi kuwa legelege, kutembea huku wakiyumbisha makalio na kupelekea kuchagua chagua kazi za kufanya.

Vijana wamekuwa wakishawishika kutafuta utajiri wa haraka na kupoteza utu wao, bila kuangalia madhara watakayo yapata huko mbeleni kwa kutafuta hela badala ya kutafuta kazi.

Unaweza kuwa na hela bila kazi maisha yako yakawa ni mateso tu; mfano, kupumuliwa, kufanya matambiko, kutokuoa, kutokuwa na watoto, kupoteza jinsia yako n.k

Kauli yetu inatakiwa iwe, tafuta kazi na sio tafuta hela.​
Vijana watafute kazi halali kwa njia halali na wafanye kazi kwa bidii.
 
Nazani maneno hayo mawili ya "tafuta hela" ni maneno ambayo tumezoea kuambiana tukiwa kazini ko tutafute hela wakuu. Ila makosa ni kumwambia asie na kazi eti tafuta hela.
 
Pesa ni matokeo ya tija na uzalishaji. Bila hivyo vitu pesa itatoka wapi? Kwa hiyo ili upate pesa focus kwanza, tija na uzalishaji.
 
Back
Top Bottom