Kauli ya Waziri Mkuu imebeba ujumbe mzito si ya kubeza. Jaribu kufikiri kwa upana

Huna unachokijua zaidi ya kuwa kipaza sauti cha hao unaowasujudia!
 
Bosi wake leo kasema nchi wanaovaa barakoa ndio wanakufa zaidi kwa corona, sasa nchi waliokufa zaidi ni boss wa mabeberu, USA, yeye sijui anatumiwa corona kwenye barakoa na nani?
Kwani tanzania tuna takwimu kamili, hata hivo USA kuna watu million 600 ulitaka wafe wangapi?
 
Mtoa mada

Tufanye hisia zako na za wakuu wetu ni sawa, sasa nikuswalike

1. Ni nchi gani hiyo inayotumia COVID-19 kama biashara?.

2. Je hizo barakoa zote zinazoingia nchini zinatoka kwenye nchi hiyo tu?

3. Na hizo chanjo pia zote zinatoka Huko?.

4. China ni marafiki zetu tangu uhuru, je na wao barakoa zao na chanjo zao nazo zina lengo la kutudhuru.

Mimi nipo na msemo wa JK wa akili za kuambiwa changanya na zako.
 
Huna unachokijua zaidi ya kuwa kipaza sauti cha hao unaowasujudia!
Wewe umeandika nini Cha maana. Acha wenye akili na uwezo watoe mawazo positive.Hizi si hoja za wavulana km wewe. Nenda jukwaa la utanashati utakuta wavulana wenzio humo.
 
UPUUZI MTUPU! Kuna nchi gani duniani imetoa kauli ya kipuuzi kama hii?
 
Kwa akili yako wewe unafikiri chanjo zinatolewa bure?

Pili,wewe unadhani hii mipango ya kutuangamiza siyo collective?

Kwa akili zako wewe kabisa unafikiri na unathubutu kusema mchina ni rafiki yako. Kuna bebari rafiki na maskini. Akikupa 5 lazima anajua atachukua 10.Jaribu kuwaza tofauti. Jielimishe pia jinsi uchumi wa kibepari ulivyo na zaidi Ni nini China anataka kwa ulimwengu wa leo.
 
Watanzania tunakoelekea siko. Tumefika mahali pa kushuku vibaya kila kitu kitokacho nje. Watu wanaoitwa mabeberu kwetu ni wabaya kiasi kwamba hakuna jema wanaloweza kufanya. Mimi nakubaliana na wazo kuwa mabeberu ambao nadhani kwa kingereza ni imperialists nia yao ni kutunyonya. Lakini ili watunyonye wanahitaji tuwe hai na ikiwezekana wenye afya. Kama vile wamiliki wa watumwa enzi hizo walikuwa wanawalisha watumwa na kuwapa tiba ili waweze kuzalisha kwa ufanisi. Wangetaka kutuua wangefanya hivyo siku nyingi kupitia chanjo mbalimbali na misaada mingine ya afya kama vile vidonge vya ukimwi tunavyopata. Kwa kweli kama wangetaka tuteketee hata vidonge vya kupunguza makali ya ukimwi wasingetupa. Inashangaza kuwa msaada wa HIV tunaona ni sawa lakini linapokuja suala la Covid 19 tunatoa hoja kuwa wanataka kutuua. Miaka karibia 20 baada ya Uhuru tunatakiwa tuwe tunatoa maamuzi ya kisayansi badala ya hisia na imani. Tumefika mahali tumakuwa paranoid na kuhisi hujuma kwa kila jambo hata kama jambo lenyewe ni kwa maslahi mapana ya nchi na watu wetu.
 
na barakoa zote zinatoka china.
 
sio watanzania, hizo ni akili za magufuri, siasa pekee anazojua ni zile za enzi za kudai uhuru na wakati wa vita baridi mambo ambayo yako nyuma sana ya muda wa sasa.
 
Ni vichaa wasiokuwa na akili wanabeza kauli za viongozi wa serikali. Kuna muda watu China walikusanya barakoa zenye maambukizi wakazileta Afrika, ila mijinga eti inabeza, eti inafurahia serikali ifunge kila kitu,
 
UPUUZI MTUPU! Kuna nchi gani duniani imetoa kauli ya kipuuzi kama hii?
Kwa hiyo viongozi wetu wanatakiwa kufuata kile wanachofanya au kuongea wengine.

Kama hakuna nyingine basi ipo moja nayo ni Tanzania.

Kwahiyo sisi km Watanzania hatuna tujualo lazima litoke nje.

Mtazamo wa mtu mjinga sana huu.Kauli ya kujidharau,kauli ya mtu asiyejiamini anayeamini kila kitu lazima aambiwe au asikie kwa wengine ndiyo adandie.Ingekua Ni Muingereza au Mmarekani hapo sawa na sisi tinatakiwa kufuata.

Hawa ndiyo Watanzania.
 

Herd immunity
 
Ondoa upumbavu wako wewe! Watanzania kama wewe ni hasara kubwa kwa Taifa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…