This is...
JF-Expert Member
- Dec 28, 2014
- 5,050
- 5,204
- Thread starter
- #61
Hili la kushuku limepata nguvu kutokana na msimamo wa nchi yetu kuhusu korona.Kila mtu kila nchi kila shirika wema kwa wabaya wanaitolea Tz macho.Watanzania tunakoelekea siko. Tumefika mahali pa kushuku vibaya kila kitu kitokacho nje. Watu wanaoitwa mabeberu kwetu ni wabaya kiasi kwamba hakuna jema wanaloweza kufanya. Mimi nakubaliana na wazo kuwa mabeberu ambao nadhani kwa kingereza ni imperialists nia yao ni kutunyonya. Lakini ili watunyonye wanahitaji tuwe hai na ikiwezekana wenye afya. Kama vile wamiliki wa watumwa enzi hizo walikuwa wanawalisha watumwa na kuwapa tiba ili waweze kuzalisha kwa ufanisi. Wangetaka kutuua wangefanya hivyo siku nyingi kupitia chanjo mbalimbali na misaada mingine ya afya kama vile vidonge vya ukimwi tunavyopata. Kwa kweli kama wangetaka tuteketee hata vidonge vya kupunguza makali ya ukimwi wasingetupa. Inashangaza kuwa msaada wa HIV tunaona ni sawa lakini linapokuja suala la Covid 19 tunatoa hoja kuwa wanataka kutuua. Miaka karibia 20 baada ya Uhuru tunatakiwa tuwe tunatoa maamuzi ya kisayansi badala ya hisia na imani. Tumefika mahali tumakuwa paranoid na kuhisi hujuma kwa kila jambo hata kama jambo lenyewe ni kwa maslahi mapana ya nchi na watu wetu.
Ni km tuko kwenye target ya kufanyiwa chochote.