Kauli ya Waziri wa Mambo ya Ndani inatekelezeka? Kitambulisho kilichoisha muda kinaweza kuwa hai kwa amri ya Waziri?

Resilience

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2023
Posts
1,096
Reaction score
4,948
Nimemsikiliza Waziri wa Mambo ya Ndani na nimesoma sheria inayotoa vitambulisho vya NIDA sijaona sehemu ambayo Waziri ana mamlaka yaku-extend validity ya kitambulisho cha NIDA Bila kuprint kitambulisho kipya.

Niombe wanasheria watusaidie legal gap endapo kitambulisho kilichomalizika muda wa matumizi kitatumika kuweka dhamana, kufanya bank transaction au any legal activity! Nauliza haya kwa Sababu siamini kama kitambulisho chenye uhai kinapoisha muda wa matumizi kinaendelea ku save the same purpose.

Lakini pia serikali natambua inakwepa gharama za uzalishaji vitambulisho jambo ambalo kwangu mimi nI la msingi hasa tukizingatia mdororo wa uchumi Duniani. Basi pamoja na nia nzuri kauli ya Waziri ipate backup ya government gazette inayokidhi au tibu mwanya wa kisheria uliopo.

Tukiendelea kufanya kazi au kutoa tamko bila proper citations za sheria itafika mahali utakuwepo mgongano wa hoja mahakamani kuhusu matumizi ya NIDA ID na mahakama inaweza kutoa hukumu ambayo itashangaza serikali.

Tumsaidie Waziri lakini pia taasisi zinazoathiriwa na vitambulisho hivi kwenye huduma ebu kuweni makini msiingizwe mkenge mwisho tamko lisiwasaidie.

Kama mnaamini kauli hii ina legal stand basi let us proceed.
 
Nimemsikiliza Mhe. Waziri wa Mambo ya ndani na nimesoma sheria inayotoa vitambulisho vya NIDA sijaona sehemu ambayo Mhe. Waziri ana mamlaka yakuextend validity ya kitambulisho cha NIDA Bila kuprint kitambulisho kipya.

Niombe wanasheria watusaidie legal gap endapo kitambulisho kilichomalizika muda wa matumizi kitatumika kuweka dhamana, kufanya bank transaction au any legal activity! Nauliza haya Kwa Sababu siamini kama kitambulisho chenye uhai kinapoisha muda wa matumizi kinaendelea ku save the same purpose.

Lakini pia serikali natambua inakwepa gharama za uzalishaji vitambulisho Jambo ambalo kwangu Mimi NI la msingi hasa tukizingatia mdororo WA uchumi Duniani. Basi pamoja na nia nzuri kauli ya Mhe. Waziri ipate backup ya Government gazeete inayokidhi au tibu mwanya WA kisheria uliopo.

Tukiendelea kufanya kazi au kutoa tamko Bila proper citations za sheria itafika mahali utakuwepo mgongano WA hoja mahakamani kuhusu matumizi ya NIDA ID na mahakama inaweza kutoa hukumu ambayo itashangaza serikali.

Tumsaidie Mhe waziri lakini pia taasisi zinazoathiriwa na vitambulisho hivi kwenye huduma ebu kuweni makini msiingizwe mkenge mwisho tamko lisiwasaidie.

Kama mnaamini kauli hii ina legal stand basi let us proceed.
Katibu Mkuu wa wizara husika na DG wa NIDA watoe Government Notice kwenye gazeti la serikali.
 
Tatizo ni NIDA, wamejaribu kila kitu pale lakini ile taasisi haifanyi kazi kwa ufanisi. Image hadi leo hii kuna mamilioni ya watu hawajapata vitambulisho vyao vya mara ya kwanza, alafu linakuja wimbi jipya la amabao vime expire!

Sijui shida ni bajeti au sijui ni kitu gani, lakini NIDA imeshindikana.
 
Kwani mkuu hujasikia hayo yote yamepita kwenye baraza la mawaziri na kutangazwa kwenye gazette la serekali?

Screenshot_20230221_204434_Chrome.jpg
 
Acha Noma..!

Embu acha Na sie tulambe iyo Asali Japo kidogo.. Tushapigwa Sana Na hao nida...!

Uraia Unaekspaya Vipi.? We hujiulizi.
 
Kwani mkuu hujasikia hayo yote yamepita kwenye baraza la mawaziri na kutangazwa kwenye gazette la serekali?
Amesema kanuni, lakini kumbuka kanuni inayotungwa Leo imelenga kuondoa validity onwards siyo backwards maana kitambulisho kimeshatoka na kimemalizika muda.

Pili, Duniani validity ya nyaraka uwekwa Kwa Sababu za kusaidia kuboresha taarifa mfano mwonekano wa Sura, kama Sura ikibadilika maana yake inaleta utata WA mwonekano Kati ya ID na mmiliki WA ID

Kitambulisho hiki kilipaswa kiwe na international standard means kiwe accepted nje ya mipaka ya Tanzania. Kwa kuzingatia kimemalizika muda itakulazimu unapotaka kukitumia uambatanishe na sheria au kanuni inayosema invalid NI valid

Mwisho, pamoja na lengo zuri bado tulipaswa kupata tamko la serikali linalokwenda kwenye taasisi za kitaifa na kimataifa lenye msingi WA kisheria kuhusu vitambulisho vilivyomalizoka muda.
 
Naelewa concerns zako ila nilikuwa najibu hoja yako ya awali kuwa unashauri tendo hili lipate Baraka za serekali na kutangazwa kwenye gazeti la serekali
 
Tatizo ni NIDA, wamejaribu kila kitu pale lakini ile taasisi haifanyi kazi kwa ufanisi. Image hadi leo hii kuna mamilioni ya watu hawajapata vitambulisho vyao vya mara ya kwanza, alafu linakuja wimbi jipya la amabao vime expire!

Sijui shida ni bajeti au sijui ni kitu gani, lakini NIDA imeshindikana.
Na hao wananchi karibia milioni 2 ambao hawajaenda kufuata vitambulisho vyao inakuwaje?!hii nchi ngumu sana kwani viongozi hawaelewi pa kuwapeleka wananchi na wananchi nao hawajui hata wako wapi?ni vulugu tupu.
 
Nimemsikiliza Waziri wa Mambo ya Ndani na nimesoma sheria inayotoa vitambulisho vya NIDA sijaona sehemu ambayo Waziri ana mamlaka yaku-extend validity ya kitambulisho cha NIDA Bila kuprint kitambulisho kipya.

Niombe wanasheria watusaidie legal gap endapo kitambulisho kilichomalizika muda wa matumizi kitatumika kuweka dhamana, kufanya bank transaction au any legal activity! Nauliza haya kwa Sababu siamini kama kitambulisho chenye uhai kinapoisha muda wa matumizi kinaendelea ku save the same purpose.

Lakini pia serikali natambua inakwepa gharama za uzalishaji vitambulisho jambo ambalo kwangu mimi nI la msingi hasa tukizingatia mdororo wa uchumi Duniani. Basi pamoja na nia nzuri kauli ya Waziri ipate backup ya government gazette inayokidhi au tibu mwanya wa kisheria uliopo.

Tukiendelea kufanya kazi au kutoa tamko bila proper citations za sheria itafika mahali utakuwepo mgongano wa hoja mahakamani kuhusu matumizi ya NIDA ID na mahakama inaweza kutoa hukumu ambayo itashangaza serikali.

Tumsaidie Waziri lakini pia taasisi zinazoathiriwa na vitambulisho hivi kwenye huduma ebu kuweni makini msiingizwe mkenge mwisho tamko lisiwasaidie.

Kama mnaamini kauli hii ina legal stand basi let us proceed.
Kwa sheria gani inayokazia utekelezaji huo? Hata tamko/amri ya rais (decree) inaweza kuondolewa na mwingine akiingia madarakani kwa sababu zake.

Lazima sheria ipelekwe bungeni itamke hivyo kisha vitambulisho vilivyopo mikononi mwa watu vihuishwe katika mfumo huo na vilivyokuwa bado vitolewe.

Hata hivyo kuna hatari kubwa sana ya kupata wageni wengi vitambulisho vya taifa maana kuna tamko lilitolewa mwaka 2022 kwamba wageni watapatiwa vitambulisho vya NIDA kitu ambacho ni kinyume na usalama wa nchi.
 
Tatizo la watu wengine ni kutosikiliza vizuri maelezo,waziri kasema wamekwisha badilisha kanuni za sheria husika na kuchapishwa kwenye Gazeti la Serikali, Kanuni ni sehemu ya sheria na mwenye mamlaka nazo ni waziri mwenye sekta na sheria inamruhusu kufanya marekebisho. Tatizo ni nini huelewi?suala la renewal kwa vitambulisho ni la kikanuni tu linamalizwa na siyo sheria kuu, main legislation. Soma kanuni zinazohusika. Kufanya renewals ni usumbufu mkubwa na matumizi ya fedha mabaya.
 
Back
Top Bottom