Kauli za Chalamila zinazua maswali mengi

Kwa nini iwe Mwanza isiwe mahali pengine Kama Simiyu, Geita n.k?
Sasa nadhani kwakuwa kwenye hoja yako umejiuliza maswali. Hili lilipaswa pia Mona ya maswali la kujiuliza.
Ila kumbuka alisema hilo kwakuwa Rais anatarajia kwenda Mwanza. Sasa siku Rais akitaka kwenda Simiyu na kama mkuu wa mkoa wa Simiyu naye ni chizi Kama Chalamila tungeskia hilo pia. ( Japo sasa kwakuwa Chalamila ameshatumbiwa kwa uchizi wake huo, basi hata mikoa mingine yenye machizi hayatasema siku Mama akitaka kuitembelea).
 
Haya ni matokeo ya kusema kabla ya kufikiri kwa kina, au kusema bila ya kuwa na uwezo wa kufikiri kwa kina.

Mkuu, unajua huyu ni mtu mzima, tena msomi nasikia sijui ana PhD sijui ya nini, tena ni Mwalimu.

Hii inatoa picha gani?
 

Hakufikiri vyema,

Na huenda alisema Jambo linalopatana na akili yake hata Kama amepewa taarifa
 
Kwani hukuwahi msikia mwendazake akiwaambia watu wa Mwanza, akielezea kuwa anawateua "wehu" wenzake kwenye serikali yake?

Hivi unadhani kweli "upstairs" zake ziko sawa huyu Chalamila??

Kule Mbeya nafikiri alionyesha uwezo wake kuwa upo chini Ila mdomo kajaliwa kuongea shudu
 
Huyu Ni mlevi
Mara nyingi anaongea pombe ikiwa kichwani
Kigogo2014 kamshauri apige biyaaaaaaa
 
Hakufikiri vyema,

Na huenda alisema Jambo linalopatana na akili yake hata Kama amepewa taarifa
Hapa tunaweza kuwa tukakubaliana kwenye kufikiria vyema. Ila haiondoi ukweli wa kile ambacho yeye kama mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa mkoa wa Mwanza anaweza kuwa alikuwa anakijua kuhusu watu wa Mwanza.
 
Unaumiza watu unaowatumikia, ajabu Sana hii
Imefanyika Sana chini ya tawala dhalimu.
Mahakimu walishindana kuwanyima wapinzani Dhamana Ili kumfurahisha mwendazake Ili afurahi awape teuzi ya ujaji.
Mapolisi walishindana kukamata wapinzani na intelligence zisizoisha mbona siku hizi hizo intellegencia ya viashiria vya vurugu atusikii kwenye mikutano ya wapinzani.Wapo waliopewa teuzi baada ya kutishia kuwaua wapinzani.
Hakika tumepita kwenye bonde la uvuli wa mauti.
Mungu yu mwema Hakuna mwanadamu yeyeto aliyewahi ibeba dunia.
 

Serikali iwe makini linapokuja suala la kupata viongozi

Vinginevyo Polisi na wanausalama wetu wataumia bure tuu kutumikishwa hata Kwa mambo yasiyo na haki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…