Jua linachomoza, madimbwi yamekauka kwa Upendo wa Mungu na watu kwa maelfu wanaelekea viwanja vya Kawe Tanganyika packers kumsindikiza kipenzi cha watanzania Dr Magufuli.
Karibuni nyote.
Rip Mwalimu Nyerere
Up dates;
DKT: MAGUFULI: VYAMA VYENYE BENDERA VYENYE RANGI NYEKUNDU VINAASHIRIA MABAYA
Katika Mkutano wa kampeni wa mgombea wa urais wa kupitia CCM, Dkt. Magufuli amesema baba wa Tiafa mwalimu Julius Kambarage Nyerere alipata uhuru wa nchi hii bila kumwaga damu
Leo tunaadhimisha miaka 21 tangu kifo chake. Lakini anakumbukwa kwa kulipatia uhuru taifa la Tanzania bila mtu yoyote kufa katika harakati za kuutafuta uhuru
Amesema hiyo ndio sababu bendera ya nchi yetu haina rangi nyekundu, tofauti na nchi nyingi za Afrika ambazo zina rangi nyekundu
Amesema kuna baadhi ya vyama vya siasa vina rangi nyekundu, ambavyo haviashirii dalili nzuri. Dkt. Magufuli ameyasema hayo alipokuwa Tegeta kwa Ndevu akielekea Kawe kufanya mkutano wa Kampeni
DKT. MAGUFULI: ALIYEKUWA MBUNGE WA HAPA HAKUWAHI KUNIOMBA
Mgombea urais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM, Dkt. John Magufuli amesema Oktoba 13, alipigiwa simu na Mgombea Ubunge Jimbo la Kawe kwa tiketi ya CCM kuhusu adha za wananchi wa Basihaya
Amesema aliyekuwa mbunge wa Kawe, jimbo ambalo Bashaya ni sehemu yake, hakuwahi kumuomba kuhusu shida ya mitaro ambayo ilifanya makazi waingiliwe na maji kwa mvua iliyonyesha jana
Aidha amemtaja Gwajima kuwa aliwatembelea wananchi hao na kusaidia kuokoa vitu vyao vilivyokuwa vikichukuliwa na maji
Magufuli ameahidi kutenga Tsh bilioni 5 katika bilioni 32 iliyotengwa kwa ajili ya ukarabati wa mitaro mkoani Dar es Salaam
Dkt. Magufuli akizungumza na wananchi wa Kunduchi, Mtongani
Ndugu zangu wa Mtongani. Mnafahamu…Tunahitaji kufanya mabadiliko makubwa. Jimbo hili linmechelewa sana.
Aliyeongoza kwenye kura za maoni ni mtoto wangu, mtoto wa dada yangu. Anaitwa Furaha. Lakini nikasema hapana. Aliyefuatia aliwahi kuwa Mbunge wa East Africa, nikasema hapana. Nimewaletea Gwajima aje afufue maendeleo ya Kawe.
Wana Kawe musilete mambo ya ubaguzi ya udini na maeneo. Nimekuwa nikiwatetea pembeni pembeni, nikiuliza matatizo ya Kawe wala sipewi.
Mara unaona mtu haingii Bungeni, au anaingia Bungeni akiwa ameziba mdomo. Nataka wanaofungua mdomo ili wanieleze shida za wana Kawe.
Dkt. Magufuli akiwa Boko Basihaya
Ningeweza kutoka Ikulu na kwenda moja kwa moja kwenda Tanganyika Packers. Lakini jana Gwajima pamoja na Diwani waliniambia kuwa kuna sehemu za Kawe zimeharibika kutokana na mvua, nikasema nitapita kuona.
Na mimi nafahamu hapa huwa kunakuwa na maji mengi. Watu wanapata shida. Lakini sijawahi kuombwa hata siku moja kwamba wananchi wa hapa wanapata shida.
Tumetenga bilioni 32 kwaajili ya kushughulikia mitaro [jijini Dar Es Salaam]. Bilioni 5 nitazileta kuja kushughulikia hapa. Lakini tukubaliane, musinichanganyie [na viongozi wa Upinzani]. Huwa naumia sana. Miaka 10 bado hamuelewagi tu?
Tegeta Kwa Ndevu
Marais wote waliopita kabla yangu hawakumwaga damu. N mimi katika miaka yangu mitano sikumwaga damu. Amani nchini Tanzania ni kitu kikubwa sana.