Kawe leo hii kuanzia Saa 1 hadi Saa 3 Usiku kulitokea nini hadi MP wa JWTZ Kufurika, Kukamata Watu, Kutembeza Kichapo na Kuzua taharuki?

Duh sometime Cheo ni Kikubwa ila kuna watu wana nguvu na hawana cheo cha muhim ukiona umri umeenda kuna mahali tumia hekima maana kuna vijana hawana cha kupoteza wapo tayari kwa lolote
Bisi bisi noma sanaaa, awo vijana wana vifaa vidogo vidogo vya hatari ukizubaa tuu wanakuswekaa

Madereva wengi wana kasilaha fulani wanatembea nachoo
 
Mimi nimemjibu kulingana na majukumu aliyoyaulza sasa haya maelezo yako yana husiana vipi na nilichokijibu mkuu
 

Kumbe Kanali alianzisha yeye mwenyewe mtiti uliomshinda...

Ubabe mwingi, ona kauawa kwa kidude kidogo misichoweza hata kutoboa mbao...
 
R.I.p kanali.............
Inavyosemekana dereva bajaji anaundugu na kigogo mkubwa tu hapa bongo.....so ngoma inaenda kua drooo........waswahili wanasema ukiyajuaaa ya mbele wenzako wanajua ya nyuma....
Na uyo kigogo kasema dogo asiguswe hata na kidole ataua mtu............
 
Lakini wakati mwingine hawa mandava wanakoseaga! Wakiwa uraiani wanataka kuabudiwa! Wanavunja sheria wakitaka waogopwe! Hayo mambo ya kutishatisha watu uraiani yamepitwa na wakati! Raia wamevurugwa!
 
Nakubaliana nawe 100% ila Dereva Bajaji hakujua kuwa Jamaa alikuwa ni Mjeda tena Kanali kama inavyodaiwa.
Hata kama angejua wao Wana nafasi ya kuwa polite kwa raia na wafanye maamuzi ya busara Sana, huwa wanakosea hapo Tu kuwa wanaweza Fanya chochote eneo lolote bila kujali wanasumbua raia pia. Binadamu tuna Julia tofauti Sana, kama inawezekana wapigwe stika usoni isema JWTZ mpaka akizeeka
 
Mimi nimemjibu kulingana na majukumu aliyoyaulza sasa haya maelezo yako yana husiana vipi na nilichokijibu mkuu
OK sawa mkuu ila hata kama pana vifungu vipo hivyo ni vya hovyo au wewe unaonaje unadhani hivyo vifungu vinaweza kutumika hata hapo DRC Jeshi lichape raia hovyo kama hapa uone kama patakalika...
 
Huyo bajaji man atateswa sanaaaa kabla ya kupotezwa..atapata kifo Cha mateso otherwise mamlaka za juu za jeshi ziingilie ....maana hiyo kesi najua haitaenda polisi itamalizwa hapo jeshini....
Na ndugu wa huyo dogo nao hawatakubali kwahiyo wataisha wengi
 
Broo sio kweli kuhusu karateka sisi ni watu waungwana mno hatufanani na hao wapuuzi wengine
 
Mi ningekuwa familia ya askari, nisingeenda mahakamani, ningewaroga ukoo mzima wapukutike kama mkungu wa ndizi unaoozea mtini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…