Kawe leo hii kuanzia Saa 1 hadi Saa 3 Usiku kulitokea nini hadi MP wa JWTZ Kufurika, Kukamata Watu, Kutembeza Kichapo na Kuzua taharuki?

Nchi hii aiseee 😆😆😆😆😆
 
Busara itumike, marehem kauwawa nje ya jeshi. Huko busara ingetumika kijana angekamatwa still na wala yeye asingejeruhiwa .
Mzee ukicheka na nyani siku zote utavuna mabua ukiwachekea waliofanya tukio matukio hayatoisha nishakutana na muuza chips mmoja anatamba kwamba yeye haogopi mwanajeshi mwanajeshi akimletea anampoteza na usisahau wale wana taratibu zao hawajafanya bila kufuata utaratibu, raia mnawadharau sana na kuwachukulia poa ndio maana wanatia adabu
 
Jeshi limekuwa too soft nowadays
 
Ujinga plus kigogo ni nani mbele ya Jeshi yaan kigogo umtume bodaboda akaue mwanajeshi alafu unavimba kua akiguswa utaua wewe nani useme akiguswa utaua mamlaka hayo unayatoa wapi?
 
Kikubwa nacho jifunza ni kua humble ukiwa na cheo heshimu watu sio una block njia kisa kanali wa Jwtz unajiona MUNGU mtu....

Pia hata Hawa vijana wa bajaji na bodaboda wapo wenye kauli mbovu na matusi na lugha zisizo faa kiasi kwamba mtu asie weza ku apply MEASUREMENTS AND EVALUATION SKILLS anaweza kujikuta anafanya ya bwana kanali ama Yale ya DITOPILE MZUZURI kumpiga pistol dereva wa daladala....

Kwa Sasa ni hayo R.i.p Afande kanali
 
Duh sometime Cheo ni Kikubwa ila kuna watu wana nguvu na hawana cheo cha muhim ukiona umri umeenda kuna mahali tumia hekima maana kuna vijana hawana cha kupoteza wapo tayari kwa lolote
Ni ushamba tu, hayo mambo huwa wanafanya wale wasiokuwa na cheo, sasa kanali mzima!!! Hapo mwenye hasara ni Kanali, ndii amepoteza, hyo wa bajaji hata anyongwe hana hasara.
 
Sasa mkuu wanajeshi wetu tunawapenda sana wakisema wawe wanatumia Nguvu kila sehemu si watatumaliza?
Maana kuna wakati tunakutana kwenye demu moja na kavaa kiraia au yuko kwenye Daladala konda anataka nauli yake.
Acha nidhamu ya uoga kikubwa ni kuheshimiana

Sent from my Infinix X669 using JamiiForums mobile app
 
Kuna mwanajeshi mkubwa nimekutana nae asubuhi hii yupo very frustrated how come raia mnakua na uadui na wanajeshi wa Nchi yenu why muwadharau watu wanaowalinda why mnawaonyesha dharau kiasi cha kuanza kuwaua wakianza kujibu mapigo mtaanza kulialia maana hawashindwi Ila taratibu na kanuni zao zinawabana, sio fair hata kidogo kwanini usimsikilize hata km kablock njia na mmepishana kauli ndio uchukue maamuzi ya kumuua?
 
Kwahiyo ukimezeshwa sumu ndio uende kuua ?


Kila mtu mwenye ugumu wa maisha akisema awe violent nchi itakalika?


Hawa bodaboda Huwa wanajiona

Hakika
 
Kutokana na maelezo,inasema kulipotokea mtifuano majibizano
Ndiyo mjeda akamtandika jamaa wa bajaji vibao na jamaa wa bajaji naye akachukua bisibisi na kumchoma
Mjeda
Na kichapo wanachokitoa ni kwa watu wa bajaji na bodaboda
Bado watu wanatakiwa kujifunza ya kuwa kwenye maisha lazima ujishushe na wakati mwingine bora ukae kimya,utaepuka mambo mengi sana

Ova
 
Acha nidhamu ya uoga kikubwa ni kuheshimiana

Sent from my Infinix X669 using JamiiForums mobile app
Ndio maana nimesema wao wana nguvu na hakuna anayeweza kupambana nao. Kwanza hatuna hiyo azma ya kupambana na jeshi letu.

Na wakiamaua kutumia nguvu kila mahali watatumaliza😆
We still believe ni watu wenye hekima na nidhamu ya hali ya juu
 
Wewe utakuwa ni mmoja wao. Unatetea ujinga. Mimi nashauri busara itumike
Sasa hapo nani katiwa adabu?
Acheni ufala wenu. Ninyi ni watu kama sisi na hamna uwezo huo mnaojidai nao tukiwa mmoja mmoja.
Mimi labda mje wengi. Nikiwa peke yangu nawe uko mwenyewe ntakupasua ukigusa mwili wangu. Huwezi kunionea kijinga jinga. Pelekeni ubabe wenu huko kwa wake zenu.
 
Shida inakuja kwamba nitajuaje huyu naye bishana naye kama ni Mwanajeshi? Especially kama amevaa kiraia.
Isije ikawa loophole kila mtu anajiita mwanajeshi akawa anatumia hiyo nafasi
Unajua mtaani pia kuna wahuni wengi.

Kitendo cha Kumshambulia Askari hadi amepoteza maisha kimeniumiza sana.

Licha ya kuwa kila binadamu ana thamani linapokuja swala la uhai wa mtu.

Kwa mujibu wa Ripoti anazotoa Gentamycin Mara kwa mara Ukanda wa Kawe na Mikocheni umejaa Thugs.

Ni mara nyingi sana Gentamycin ana ripoti vitendo vya uharibu na vibaka pande hizo.

Hii pia ni doa maana Hiyo location ya Kawe na Mikocheni iko Hugely and Overloaded na watu wa vyombo vyote vya ulinzi na Usalama na ofice zao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…