Kaya 644 Magomeni kota zagomea kusaini mkataba kununua nyumba

Acha ushamba pimbi wewe, Magomeni ni City Center tangu lini?

Au ndio elimu ya MEMKWA?
 
Uondoke kwenye hizo nyumba mapema, hizi kelele zako hazitakisaidia chochote, zama zimebadilika.
Mngeijua mipango ya Mungu juu ya TANZANIA msingeendelea na dhuluma Kwa raia maskini.

Amin nakuambia, upanga utaponyooshwa juu ya nchi,

Mtalia Kwa machozi ya Damu lakini hapatakuwa na REHEMA tena.

Ukimnyanyasa maskini na yatima au mjane, unapambana na Mungu mwenyewe.

Vita hiyo ni kubwa msiingie, ni hatari kwenu na vizazi vijavyo nyuma yenu.

Aaaamen
 
wao wana bei gani sasa, mbona ni kama wanataka wapewe bure.
mimi nadhani iangaliwe bei ya soko ya kupanga maeneo hayo wapangishwe
wasikilizwe anyway
 
Ndo nasema jengeni zenu Kwa pesa mlizikopa na mzifanye za biashara mpate faida.

Hizo Zina maelekezo ya marehemu kuwa wapewe hao maskini waliopo kipaumbele.

Sasa kuwapandishia Bei Ili muwafukuze, hizo ni HILA.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji23][emoji23][emoji1787]
 
Poleni San wakza Anza kukumbia mji alekeeni kibaha huko ndani Ni Bora kuliko kuishi hapo magomeni pisheni vijan wauuza unga waingie hapo
 
Siyo nyumba, ni apartment, kuna tofauti kati ya nyumba na apartment.
Hamna tofauti. Labda useme condominium.

Pale ni karibu na mjini mtu hawezi kuuziwa bei ya chanika. Maana hata wakipewa kwa millioni 12, wataenda kuvuliwa na matajiri kwa ela ndefu tu. Kama mtu anaona hiyo hela ni kubwa ahamishiwe sehemu ambayo ata afford. Simple
 
Sahihi...umeona juzi kuna mdada kutoka bara,ndizi zake za biashara zimemwagwa?...na ni marufuku kuingiza ndizi Zenj?...huyu sio mtanzania?.
 
Sahihi...umeona juzi kuna mdada kutoka bara,ndizi zake za biashara zimemwagwa?...na ni marufuku kuingiza ndizi Zenj?...huyu sio mtanzania?.
Umejenga hoja muhimu lakini iko nje ya mjadala huu. Lakini nitakujibu hapa hapa.

Kikatiba muungano wetu una shida kubwa, na mara zote unambagua mtanganyika anapokuwa Zanzibar. Huenda kilichomkuta huyo mtu mpaka ndizi zake kutupwa ni matokeo ya muungano mbovu.

Upande wa pili, huenda mhusika alileta ndizi kinyume na utaratibu, hivyo sheria ikachukua mkondo wake!

Mwisho huenda mhusika amefanyiwa hayo yote kwa kubaguliwa kwa kuwa ni mtu kutoka bara, suluhisho ni kuupinga huo ubaguzi kwa nguvu zote na sio kulipiza ubaguzi kwa watu wengine.
 
Hujui lolote kuhusu uchumi bora ukae kimya!
 
Embu jamani tuwe wa kweli na halisi. Apartment za mijijini, zilizojengwa kisasa tena muundo wa ghorofa ni makazi yanayowafaa watu wa kipato cha juu na kipato cha kati, maskini haziwafai.
Kwanini? Sababu ziko hapa.
1. Unahitaji kulipa pesa nyingi zaidi kuweza kupangisha au kuzinunua.

2. Zimewekwa kwenye maeneo strategic kuwalenga watumishi na wafanyabiashara wanaofanya mishe miche zao maeneo karibu au kuelekea katikati ya miji.

3. Kuna gharama nyingine kadhaa za kijumuiya (service charges) zinamuhitaji mhusika kuzilipa kila mwezi, kama ulinzi, Parking, Usafi, Umeme, maji nk. Na mtanzania maskini hataweza daima.

4. Kanuni na masharti kibao ya kulinda ustaarabu wa kuweza kuishi kwenye jumuiya yanaorodheshwa na huwa ni kikwazo kwa jamii za maisha ya kimaskini.
 
Hili swala la nyumba hizi Serikali wasipokuwa makini litakuja kuwachafua; na hasa katika kipindi hiki ambacho tunaelekea uchaguzi mkuu, ukizingatia kuwa muasisi wa wazo hilo hayupo tena, ameshatangulia mbele ya haki.

Hawa watu walikuwa na makazi yao pale ambayo yalibomolewa na hatimaye nyumba hizo kujengwa.

Ushauri wangu katika hili ni kwamba; Serikali wanatakiwa aidha wa-subsidize kwenye bei hiyo kwa kiasi kikubwa ili wakazi hao waweze kuzinunua, au wakazi hao wapewe nyumba hizo bure.

Setikali wasipofanya hivyo kitakachokuja kuibuka huko mbele ya safari ni maneno kwamba JPM aliwajali na sasa hayupo wanaanza kunyanyasika,; na haya maneno hayatatoka kwa wakazi hao, ila kwa watu wengine ambao Serikali ya CCM inawajua pia. Na kama itakuja kupelekea maneno hayo yakatamkwa, watamkaji lazima wataonekana wako sahihi kwa kila mtu atakayebahatika kuwasikia wanayatamaka

Serikali inaweza kuepusha tatizo hili kwa kuwapa wakazi hao nyumba hizo BURE kama kitendo kimojawapo cha kumuenzi muasisi wa wazo la wakazi hao kujengewa nyumba hizo, Hayati JPM
Ikiwezekana wawape BURE, hayupo mtanzania atakayelalamika kwa wakazi hao kupewa BURE nyumba hizo.
 
Nakubaliana na wewe kwa 100%
 
Ndugu

JPM aliwapa wakae bure miaka 5 baada ya hapo waanze kulipa, hao waliokaa hapo wote ni wenye akili timamu na wangekuwa na maswali wangeuliza kipindi hicho

Hili swala la kiuchumi sio swala la siasa. Hao wapangaji hawana uwezo wa kuifanya CCM isishinde

Kama JK aliwavimbia walimu waliotapakaa nchi nzima na kukataa kura zao na bado akashinda hao wapangaji 10 ndio wataweza?
 
Habari wana JF.
Kwenye siku ya uzinduzi wa hizo nyumba nilibahatika kusikiliza hotuba ya Mh. Rais, ya Wakazi husika na ya Mtendaji wa wakala (TBA) hivyo nadhani kuna kitu muhimu hakitajwi kabisa.

Mh. Rais aliwaambia hao wakazi kwamba watakaa kwenye hizo nyumba kwa kipindi fulani bila kulipa kodi kama alivyokuwa amewaahidi hayati JPM. Zaidi ya hapo aliridhia ombi lao la kuwa Mpangaji mnunuzi kwa kufuata mwongozo utakaotolewa na Wakala wa Majengo.

Kwa Muhtadha tajwa hapo juu ni dhahiri wahandishi wa habari hawajafanya "Homework" yao vizuri. Kwa kufuata maagizo ya Rais siku ya uzinduzi, hao wakazi wangeliweza kuendelea kuwa wapangaji wa kawaida (kuanza kulipa Kodi baada ya "grace period") au kuwa wapangaji wanunuzi (kuanza kulipa deni la ununuzi kidogo kidogo kuanzia sasa).

Kwa maoni yangu Serikali iongee na Wakala kuhusu bei zinazolalamikiwa LAKINI iwe makini na watu wasiohusika wanaweza kuwatumia hao wakazi kuzipata hizo nyumba kwa bei ya mtelemko.

Ahsante
 
Dunia nzima masikini hatuishi Downtown kwenye makazi rasmi yenye hadhi

wawape fursa ya kuuza hizo nyumba, watakuja Wahindi watanunua kwa bei ya juu na watabaki na chenji ya kwenda kujenga Majohe baada ya kulipia TBA
Mkuu waziuze hizo nyumba kwani za kwao?

Wewe leo umpangishe mpangaji uende ulaya ukakae huko halafu unarudi baada ya miaka 20 unataka kupaendeleza anaanza kulalamika. Unajenga jengo jipya unamuweka akae buree kwa mwaka mzima. ukifika wakati unamtoa anaanza kulialia, niambie utaacha kuwaita Majembe Auction?
 
Kwanza hao wanaokaa hapo watakuwa ni wajukuu

Wakienda kuchunguza watakuta hao sio waliopangishwa na serikali miaka hiyo ya nyuma

Walipe kodi au wahame
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…