Kaya 644 Magomeni kota zagomea kusaini mkataba kununua nyumba

Kaya 644 Magomeni kota zagomea kusaini mkataba kununua nyumba

Walipewa Kodi miaka 3 wakapange kwengine,
Wakaambiwa watarudi wakae bure miaka 3.

Kwa hili nawalaumu serikali.

Inakuwaje mpangaji wa eneo la serikali wageuzwe kama wamiliki wa eneo?
Hao wakazi wa magomeni kota ni wapangaji tu.
walipaswa wapewe notice ya kuondoka ,,
Kama watashindwa kulipa gharama husika.

A tenant will always be a tenant.

Sent from my 2201117SG using JamiiForums mobile app
Nimeelewa, shida ya viongozi wenu ni kuleta siasa kila mahali, hilo la kukaa miaka 3 bure, kuwapa kodi ya miaka mi3 ni siasa tu!
 
Nakumbuka kama aliwapa miaka kadhaa ya kukaa bure halafu baadae waanze kulipa kodi
Ni Kweli, Chumba kimoja na sebule mkataba inasoma ml 50 Kwa miaka 20,

Unajua hesabu ya Kodi anayotakiwa kulipa Kwa mwezi Kwa hesabu hiyo?

Hivi Kuna mama ntilie au matching guys anaweza lipa 208,000 Kwa mwezi?

Na Masharti ya mkataba ni strict.
 
Kwa mbali naona wapemba,waarabu na wahindi watazinunua hizo!.
Wote hao waarabu, wapemba na wahindi ni watanzania na wana haki sawa sawa na watanzania wengine, tusipaguane kwa rangi ya ngozi zetu. Kama kwa hulka na tamaduni zao wanapenda kukaa katikati ya miji, kubanana maghorofani na wako tayari kulipa gharama zote za kuweza kumiliki hizo apartment basi tuwaheshimu kwa hulka walioichagua.
 
Marehemu hawezi kujiamulia tu yeye matumizi ya kodi za watu wengine jinsi anavyotaka.
Ndo nasema jengeni zenu Kwa pesa mlizikopa na mzifanye za biashara mpate faida.

Hizo Zina maelekezo ya marehemu kuwa wapewe hao maskini waliopo kipaumbele.

Sasa kuwapandishia Bei Ili muwafukuze, hizo ni HILA.
 
Wote hao waarabu, wapemba na wahindi ni watanzania na wana haki sawa sawa na watanzania wengine, tusipaguane kwa rangi ya ngozi zetu. Kama kwa hulka na tamaduni zao wanapenda kukaa katikati ya miji, kubanana maghorofani na wako tayari kulipa gharama zote za kuweza kumiliki hizo apartment basi tuwaheshimu kwa hulka walioichagua.
Hakuna First class citizen,

Wala hakuna Second class citizen.

We are all equal.

Wewe ni mmoja wa watia ZENGWE Ili wapangaji hao wafukuzwe.

Justice is Coming in Tanzania.

Aaamen
 
Uondoke kwenye hizo nyumba mapema, hizi kelele zako hazitakisaidia chochote, zama zimebadilika.
Hali ya kiuchumi ya wapangaji hao ukilinganisha na mwaka 2015 imeporomoka mara dufu.

Hizo gharama walizoomba wauziwe ml 17 zilitakiwa zishuke Hadi ml 12 na walipe Kwa miaka Hadi 20.

Narudia, mkitaka faida, Serikali haipo Kwa ajili ya kumake PROFIT, IPO kusaidia raia.

Jengeni nyumba zenu binafsi ndo mpange faida,

Ukipewa nafasi ktk kuutumikia Umma wa Watanzania, tanguliza maslah ya umma mbele.

Aaamen
 
Hao wananchi wapangaji wako wangapi na wamelipa kodi kiasi gani kuchangia ujenzi wa hizo nyumba, na sisi wananchi tusio wapangaji tuko wangapi na tumelipa kodi kiasi gani kuchangia ujenzi wa hayo maghorofa.
Mjadala ufanyike wa wazi,

Pande zote zikae na wafikie mwafaka Kwa HAKI.

AMRI hazitakiwi ktk suala hili, majadiliano ndo yanatakiwa.

Siku alipochaguliwa mtoto wa Nanii ktk wizara hiyo, nilijua tuna KAZI kubwa ya kufanya.

Justice is Coming to TANZANIA.

Aaamen
 
Back
Top Bottom