Kazakhstan, nchi yenye waislam wengi yapiga marufuku hijab mashuleni

Ila hizi Dini zina shida aiseeee. Nadhani rastafarian ni Imani mzuri Zaidi
Shida wanazo watu tu wenyewe zaidi kuliko hizo dini, mfano wewe ungekuwa rastafarian kwa ishu kama hii ya ijabu mtazamo wako ungekuwa ni upi?
 
NA NGUO WAAMBIE WASIVAE.
MPAKA WAKIKUA WATAJIAMULIA KUWA WAVAE AU WAENDELEE KUTOVAA.
 
Lakini ukiangalia ni ujinga kuvaa hijab, unakuta katoto ka miaka 3 nako kanavalishwa magunia sasa sijuwi ili iweje.
Ila mkuu mtoto hawezi kukwepa athari za mitazamo ya wazazi wake ndio wapo, lakini pia mavazi ni mapambo pia sio wote wenye kuvaa kwa sababu za kiimani..
 
ukijiita jina la babu yako wanasema laana ila majina ya wageni ndo yana baraka ushenzi mtupu
Jina ni jina tu mkuu ujiite la Babu au la nani, wanaigeria wenzetu wanatumia majina yao ya asili ila unakuta uzungu mwingi na dini za ukristo na uislamu zimewatawala pamoja na kuwa na majina yao ya asili. Kwahiyo vitu vyengine ni vidogo tusivikuze.
 
Wako sahihi sana dini isichanganywe na taaluma ni kuwachanganya watoto

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umeandika nini? Mbona wazee wa wakiristo wanawake hawatembei wakiwa na vimini? Wanajistiri tena kwa kanga na hijab. Hijab ni heshima; mtoto mdogo wa kiislam anaheshima
Hamna kitu hapo, hayo mavazi ni ya asili kwa watu wa mashariki ya kati lakini kwa sisi waafrika sio utamaduni wetu hata huko mashariki ya kati kuna wengine ktk nchi kama Misri, Lebanon na Israel hawazitumii.
 
Tatizo ni aina la vazi au ni vazi la dini? Sijaelewa hijab inamkera vp mtu mwengine?
Ingekuwa tatizo ni kero tu ingekuwa siyo jambo kubwa ila tatizo inaleta udini mashuleni ...kumbuka hivi sasa walimu wameanza kushutumiwa kuwakagua wanafunzi nywele kisa hijabu..kesi zimekuwa zikiusishwa na dini ...wakati mahospitalini wanawake wanavuliwa nguo zote. Hivyo udini umeanza kujengeka mashuleni tofauti na zamani tulipo kuwa tunasoma sisi wanafunzi wote walikuwa sawa ...ni sawa sawa uruhusu wanafunzi waislamu kuvaa kanzu mashuleni wakati wasio waislamu wanavaa unifomu...kumbuka udini una tabia ya kujengeka polepole na kuleta madhara baadae

Sent from my SM-A325F using JamiiForums mobile app
 
Mambo mengine tunayakuza tu tu mkuu, Unataka kuniambia hizo jamii zengine kama wazungu na huko Asia kila jamii inaabudu kwa tamaduni zao?
Ndio hivyo na hawawezi kukubali kuacha kutumia majina yao kwa kisingizio cha dini ila ni waafrika tu ndio malimbukeni wa kurubuniwa.
 
Bado sijaona tatizo tunatakiwa tuishi kwa kuvumiliana kwa yale yenye kuvumilika, sioni shida kwa mwanafunzi kuvaa hijabu hasa ikiwa kwa hiyari yake muhimu usafi uzingatiwe. Ukitaka kusema hijabu ni udini na kutaka kuzuia udini shuleni basi hata kuvaa rozari itabidi izuiliwe.
 
Wanafunzi wa kiislam Tanzania hawavai hijabu ila wanajifunika kichwa tu kama wanavyovaa masister wa Romani catholic
 
Naunga mkono hoja 🤝💯
 
Ndio hivyo na hawawezi kukubali kuacha kutumia majina yao kwa kisingizio cha dini ila ni waafrika tu ndio malimbukeni wa kurubuniwa.
Unadhani kuwa wao wanazingatia hayo masuala ya imani zao na majina yao kama ambavyo wewe unaona? Nimetoa mfano wa Nigeria ambao ni waafrika hutumia sana majina yao ya asili ambapo wewe unaweza kuona wanazingatia hasa hilo jambo ila ukiangalia maisha yao ya uzungu mwingi na imani za ukristo na uislamu ndio zilizo tawala sasa huko kuzingatia majina ya asili kuna faida gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…