luchelele mzunguko
JF-Expert Member
- Feb 12, 2021
- 1,206
- 1,641
Sawa nichek manNmeipata mkuu,kule sio home ni kwenye harakati tu nikajikuta nipo kule
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sawa nichek manNmeipata mkuu,kule sio home ni kwenye harakati tu nikajikuta nipo kule
Yaani🤣🤣🤣Kumbe jf kuna hadi kazi za hivi, mnatuvuruga kwakweli
[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28] pole sana...daah kweli ajira tatizo 3500 kwa siku?Nilikimbia kazi ya kushusha mizigo kwenye store ya kiwanda fulani.
Kwenye hicho kiwanda Kuna kitengo kinaitwa finance Sasa walikuwa wamebandika tangazo wanahitaji Kuajiri vijana 10 so kutokana na jina la kitengo nikashawishika kuomba kuajiriwa Kwa Imani kuwa kazi zitazokuwa zinafanyika pale zitarelate na mambo ya finance ili kujiakikishia kuwa napata hiyo nafasi nikaenda kuoongea na mshua fulani ili hakikishe connection hainipiti pembeni.
Picha linaanza tunapelekwa general store ya hiyo kampuni Kwa hiyo sisi ndio tutakuwa full responsible Kushusha mizigo yote inayoingia kwenye hiyo kampuni na kweli kampuni inapokea mizigo sio kitoto kuanzia cement, chokaa, Nondo, mabati, mbolea, dawa za kilimo in short ni general store haswa.
Sasa task yetu ya kwanza ilikuwa Kushusha mbolea Toka kwenye scania mzee nilikomaa Kushusha tumemaliza tunaona scania nyingine inaingia zile za kufuta na kontena mbili ilikuwa na cement wahuni wakaniambia Mimi ndio niwe nawatishwa aisee niliona Bora kubeba kuliko kuwatishwa sababu walikuwa wako chapu kinoma nikaomba kubeba wakakubali tunakaribia kumaliza tunaona nje ya Fensi scania nyingine inakuja na yenyewe cement nikaanza kugiveup wahuni wananiambia Kuna siku magari yanakuwa hayaji Kwa hiyo zipo siku tutarelax.
Nilipiga Ile kazi Kwa siku tatu sikuchukua malipo kwani walikuwa wanalipa baada ya wiki mbili na malipo was 3500 per day bila ya kujali uzito wa kazi wa siku husika.
Kwa kweli watoto wa kwanza huwa mnapitia mengi sana. Unakuta wewe ndio kiongozi wa wadogo zako ,wakati huo huo maisha ya wazazi yanakuwa hayajakaa sawa kwahiyo inakubidi utoe support.Kweli mkuu, sisi watu tuliotokea familia za sayari ya tunayapitia Mengi mpaka kutoboa, mbaya unajikuta wewe ndo mtoto wa kwanza,familia ipo na umaskini wa kutupa, unaanza pambana na kukomaa kimaisha hata kabla ya umri,ila bwana Mungu huwa anatupigania
We jamaa unetisha sana yaani nimecheka kama mwehu[emoji1787][emoji1787][emoji1787]Kuna siku nipo maskani nishachoka zanguu,akaja jamaa akasema anaeweza kuchezea kinyesi twende kuna kazi huko,,
Nikamuuliza kazi gani? akasema mwenye nyumba anataka chemba ya choo tuchote kinyesi yote na ndooo tukamwage kwenye shamba lake ili ile chemba iongezwe urefu yani pale ilipo ifukuliwe zaidi kwenda chini..
ila huwezi kufukua zaidi bila kutoa kinyesi chote, tukamwambia si aite tu gari ya kunyonya kinyesi inyonye, Akasema njia ya kufika kwake gari ya maji taka haifiki na hata wakifosi gharama ni kubwa mno inafika 1m na huyo mzee hiyo hela hana..
hivyo mzee katoa ofa ya watu kuchota mzgo wote na ndoo na kwenda kuumwaga huko shambani kwake, Tukauliza OFA yake sh ngapi?
Jamaa akasema kazi tunaifanya watu wa 4 tu mzee kasema atatoa 100,000 kwa kila mtu,jamaa mmoja akasema mwambie aongeze walau iwe 150,000 tukapge kazi, nazama chumvini nalamba inye live na ulimi sembuse hiyo harufu inishinde? mwambie aongeze dau...
Jamaa akavuta simu kwa mshua akamwambia vijana wa kazi wamepatikana ila wanasema 100k haitoshi waongeze 50k iwe 150k, mzee akajibu Sawa njooni.
Jamaa akasema oyaa mshua kakubali, Huyo mwingine akawambia sasa sikilizeni hapa tunaenda nunua mafuta ya Taaa kidumu cha lita 5 tunamwaga mwaga mule kwenye chema mote Harufu inakata kazi tunapga freshi..
Kusikia hivyo tukaona jamaa katoa idea nzuri sana,kweli haooo hadi kwa mangi tukanunua mafuta ya taaa haooo safari ikaanza kwenda site.
Tumefika tukaenda kwenye chemba, ilikua tayari ishabomolewa lile zege la juu hivyo limebaki shimo pana tu unaona inye live live,mafinyo finyo live live, Jamaa akamwaga mafuta ya taaa pwaaaaaa koteee..
Tukaletewa ndooo kila mtu na ndoo yake,gloves kazi ikaanza nikadumbukiza nikachota ndoo ya kwanza nikatoa,jamani jamani jamani nilienda kumwaga shambani nikapitiliza huko huko sikurudi nyuma tena.
Asee inye isikieni tu,ile 150,000 nikaona wala isinipe presha mimi,na niikose tu siwezzi chezea gwede gwede kama vile ni rost... nimeondoka nimefika maskani nasimulia waliobaki,nusu saa haijaisha namuona mwenzangu mwingine huyu hapa karudi, aaah weee kuna kazi za kufanya bwana sio kazi ya kuchezea tope la binadamu..
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]enzi hizo nimemaliza high school nikaamua kusaka kibarua ili niweze kukidhi mahitaji yangu wakati nasubiria matokeo.
Kuna sehemu nilikua nakuta watu kibao asubuhi wakati naenda shule. Walikua wanasubiria matajiri wenye mashamba wanaenda kupiga day work kwa malipo ya 4000 per day.
Msimu wa mavuno ya mpunga huo,mazee nikajilipua kwenda pale. Mama mmoja akanichagua na team ya watu 10 kwenda kumvunia shambani kwake.
Kufika pale tukapewa vikwakwa,yani mnakata mpunga mnabeba na kuukusanya sehem maalum kwa ajili ya kupigwa. Kazi ni ya kuinama inuka siku nzima. Mpunga pia unawasha hatari, 2 hours later nilitembea kwa mguu kurudi town. Hakikua kikombe changu kile.
Inauma sana sana ,kufanya kazi halafu usilipwe au ucheleweshewe mshahara#INAUMA SANAKisa cha pili. Somewhere Mkoa wa pwani.
Nimezurura weee nikawaona jamaa wanajaza kifusi kwa mchina nikajisemea acha nijaribu kazi ilikua ishafika nusu. Jamaa mmoja wa dodoma bahi mwingine wakutoka kigoma nikaongea na mchina akanidirect kwa hao jamaa niunge nao maana kazi walianza na wengine wakashindwa wakala kona. Basi bwana jamaa wakakubali tukagawana majukumu mm nachimba wao wana beba kwa toroli afu wanapeleka kujaza kwenye jengo kwa chini. Sasa hesabu ilikua siku moja kazi tunaua. Bwana weee siku ile ikakata hatujamaliza kesho tukapiga tena sisi tukaona hapa tayari pashakaa level. Mchina anaesimamia anakuja jioni anasema hapa kuna mabonde jazeni tena. Kudadeki muda huo mikono imepasuka mno. Tukajaza ile ile jioni kibingwa pakawa level. Kimbembe kwenye kulipwa siku hiyo ikapita tukaambiwa mje kesho mapema tu mchukue chenu bwana wee kesho huyoo tumefika saa 4 wengine saa 5 aisee tumesubiria wee hela hatupewi tukiuliza oooh mpaka mchina/boss mkuu asaini na hayupo. Dadadeki muda huo nishajichokea. Basi bwana siku hiyo nayo ikakata tukaja kesho nyingine tena kudai hela sasa mapema tu. Jamaa wanatuangalia afu wanatuzunguka oohh subirini mpaka jioni. Tukaona hawa chenga chenga nyingi. Nikawaambia jamaa mm niliunga katikati kwenye hii kazi hivyo utata anzisheni mm.nitapump tulipwe. Kama kawaida siku zote waoga ndio wanaonewa. Jamaa mmoja yeye anasema aah tuombe kwa ustaarabu nikamjibu hapa hatuombo tunadai jasho letu. Jamaa wa kigoma nikamsanua nikamwambia hapa tufanye kamgome flani chukua chepe na mm chepe tunarusha hiki kifusi nje barabara ya kuingia kwenye miradi yao pale. Bwana tukarusha kama chepe 3 tu mchia huyu. Acheni acheni tukamjibu kama hela hamna acha tukilipe kwa njia hii kuacha kwetu ni utulipe. Aisee haizikupita dakika 5 yule meneja alikua dada wa kichina katoka huyo kaenda bank crdb jirani tu pale pale yaani hata dakika moja haishi ashafika benk akafanya yake huko dakika kama 15 au 20 huyu hapa akampa yule msimamizi alitupa kazi hela atulipe. Ikaisha hiyo. Ila nyieee acheni tu. Watu wanaopambana bila kuinuliwa au kushikwa mkono wanapitia mengi.
AiseeeMimi kesho yake mikono na vidole nilikuwa kama roboti, yaani kunyoosha mkono au kushika kitu ilikuwa shida.
Nikaenda kufanya vibarua viwandani, nilikuta wadada wanapiga kazi ngumu balaa ukikutana nao mwenge stand ya dala dala utadhani wanafanya kazi ofisini. Malipo ilikuwa 1850 kwa siku kazi masaa 8
Noma mzee. Mbona kazi hizi ngumu ngumi zipo mkononi. Binafsi tushashikana saana mashati au kuchimbana mikwala na mafundi ujenzi. Maana hawaaminiki.Inauma sana sana ,kufanya kazi halafu usilipwe au ucheleweshewe mshahara#INAUMA SANA
Shida si sifacheka sana ila omba yasikukute, huwezi kuwa babu mwenye wajukuu na hujapitia hizi za hustle haha..discpline ni kutokukata tamaa, uwe na kiu ya kutaka kesho yako iwe bora kuliko ya juzi.
Af kazi za siku hizi ngumu sana maana zina maboss na machawa wao. shida tupu
Haya maisha haya [emoji3]We kenge umenichekesha sana[emoji23][emoji23]
Leo watu wamevurugwa yan wanafunguka ya moyoni[emoji23][emoji23], hawa wakweli sasa tuwasubir wale wakishua wazee wa nyuzi za magariKumbe jf kuna hadi kazi za hivi, mnatuvuruga kwakweli
Swali kutoka kwa juniya
naona kaka yangu ameamua arudi kazi ya machimboni imemshinda,nawasilishaKuchimba dhahabu,unaingia ndani ya shimo lililochimbwa locally.Yani kifo nje nje shimo likiporomoka