Mwizukulu mgikuru
JF-Expert Member
- Oct 21, 2021
- 5,715
- 13,739
2014 napiga vibarua vya ujenzi nikakutana na mshikaji wangu mmoja anaitwa baba bahati....baba bahati akanipa connection ya kumwaga zege..
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
😂😂😂 umenikumbusha jamaa angu mmoja wa kuitwa bakayoko nakumbukuka aliingia site akiwa nywele fresh tu lakini mpaka kazi ya kumwaga zege inaisha mwamba nywele za katikati ya kichwa akawa hana"UTAPIGA KAZI MPAKA UITEE MMAA"
Nakumbuka enzi zile sina mishe yoyote na nasaka pesa.niliamka asubuhi moja na kuiingia mtaani, kupita mtaa fulani nkaona watu wamesimama nje ya geti ya site ya ujenzi wanahesabiwa.
Nikaona wanapangiwa kazi za kufanya, walikuwa watu kati 40 mpaka 50 hivi.Kidume mbio nkajipenyeza.
Sasa yule Mhandisi(nilikuja kumjua badae) aliyekuwa anahesabu watu na kupanga majukumu akaniweka kwenye kundi la 2( watu 23 maana yake tukawekwa magroup ma2 ya watu 23, 23 kama sikosei).
nikasikia yule mhandisi anatoa majukumu kwa group letu kuwa "" nyinyi wazee ni wazee wa MMAA"" na natoa 40,000 kwa kila mmoja kazi ikiisha.
Daah kusikia 40,000, nkaona kazi si ndo hii jamani.
Ila sasa sikuelewa alivyomaanisha "wazee wa mmaa",
kumbe banaaa ni wazee wa zege la jamvi la juu ya GHOROFA ya tatu.zege la kukesha, zege la kufa mtu,aaah manina
wenzetu wao yani kundi la pili wao ni kazi za chini.
*****************************************
Picha linaanza tulianza kupakua mifuko kama 300 ya cement, mchanga lori, kokoto lori, mixer na gari la maji .halafu kilichonitisha walishusha ndoo kubwakubwa za kubebea zege kama 200 hivi.
AISEEEEE, AISEEEE. ndo nilijua kwanini sisi tunaitwa"" wazee wa MMAAA" yani utapiga kazi mpaka uombe maji kama mtoto.
Zege linakorogwa chini unalipandisha kwa kichwa mpaka ghorofa ya 3.MANINAAAAAA
nilipiga trip kama 6 hivi,nikiwa napandisha trip ya 6, nkasikia lijamaa limoja eti kwann mimi mchumba nimekuja kwenye kazi za wanaume. Niliumia sana, nkajikaza trip kama 5 zingine.
ile trip ya mwisho, nkasikia shingo imekaza.[emoji16][emoji16][emoji16]nikajiuliza kwanini nifie site??
Nilimuaga msimamizi kuwa naiingia toilet 2mins , Akajibu ""chapu chapu dogo huu si muda wa kulemba kanye huku umesimama maana hii ngoma tunakesha mpaka uitee mmaa""
nilivyokata kona, nilikimbia mnooooo,zile trip 11 nilizopiga niliumwa 2 days[emoji2]
Sikuwahi kufanya kazi ya zege tena.
Kwa jinsi nilivyo- kila nkimhadithia wife kuwa nilipiga kazi za hovyo huwa anakataaa sanaaa, sijui why but anyway.
wakuu tusikate tamaaa maishani.
"wazee wa mmaa"[emoji23][emoji23]
Pia kingine kazi ya site aseee inataka uzoefu kuna watu ndo life lake kazi nyingine hataki ni mwendo wa site !! Na walio wengi wanakula kijitikila kazi unayogusa yamoto 😂 , niliwahi omba kazi site ya kufyatua tofali asubuhi mapema 11 nimefika pale nikamkuta boss wa hapo akaniambia kazi iliyopo labda upange vibao vya tofali.
nikaona vibao vya tofali mbona vidogo dogo tu kazi simple hii, akaniambia malipo hapa ni 5000 ila kula ni hapa hapa..
nkajisemea kimoyo moyo,mimi vibao hivi ndio nipange hadi muda wa kula,basi kazi ikaanza,Bwana Bwana weee, nilipanga vile vibao tangia 12 asubuhi hadi 1 usiku mgao wa vijana wa tofali na mimi nikapewa changu,
jamaa akanisifia eti nimefanya vizuri kesho niwahi tena,Kimoyo moyo nikamwambia "aaah subutuuuu" nani aje na kesho... ndio sikurudi tena pale...
Kuna watu wako speed kinoma !! Halafu kwenye kumtwisha mtu naogopa kinoma unaweza ukamtupia mfuko wa cement vibaya ukamvunja !!!Nilikimbia kazi ya kushusha mizigo kwenye store ya kiwanda fulani.
Kwenye hicho kiwanda Kuna kitengo kinaitwa finance Sasa walikuwa wamebandika tangazo wanahitaji Kuajiri vijana 10 so kutokana na jina la kitengo nikashawishika kuomba kuajiriwa Kwa Imani kuwa kazi zitazokuwa zinafanyika pale zitarelate na mambo ya finance ili kujiakikishia kuwa napata hiyo nafasi nikaenda kuoongea na mshua fulani ili hakikishe connection hainipiti pembeni.
Picha linaanza tunapelekwa general store ya hiyo kampuni Kwa hiyo sisi ndio tutakuwa full responsible Kushusha mizigo yote inayoingia kwenye hiyo kampuni na kweli kampuni inapokea mizigo sio kitoto kuanzia cement, chokaa, Nondo, mabati, mbolea, dawa za kilimo in short ni general store haswa.
Sasa task yetu ya kwanza ilikuwa Kushusha mbolea Toka kwenye scania mzee nilikomaa Kushusha tumemaliza tunaona scania nyingine inaingia zile za kufuta na kontena mbili ilikuwa na cement wahuni wakaniambia Mimi ndio niwe nawatishwa aisee niliona Bora kubeba kuliko kuwatishwa sababu walikuwa wako chapu kinoma nikaomba kubeba wakakubali tunakaribia kumaliza tunaona nje ya Fensi scania nyingine inakuja na yenyewe cement nikaanza kugiveup wahuni wananiambia Kuna siku magari yanakuwa hayaji Kwa hiyo zipo siku tutarelax.
Nilipiga Ile kazi Kwa siku tatu sikuchukua malipo kwani walikuwa wanalipa baada ya wiki mbili na malipo was 3500 per day bila ya kujali uzito wa kazi wa siku husika.
Mkuu hiyo inaitwa "KUSOTEA" mwajiri akija mnapigana vikumbo ikifika mida ya mchana kila mtu anasepa kesho mapema tena😂😂hiyo ilinikuta mwanza kiwanda kimoja cha vinywaji eti utaratibu wa kuajiri ni unaamka asubuhi unaenda kusimama getini kama mbwa(nyomi la kufa mtu) halafu anatoka mtu huko ndani anapoint anaowataka then mliobaki mnaambiwa mjaribu kesho, ...malipo 6000 per day
Kumtishwa mtu ni kazi ngumu achilia mbali kumtishwa mtu vibaya ila Kuna mziki wa kuvuta mfuko kuanzia katikati mpaka mwanzo wa kontena ni balaa na nusu ni heli wote muingie Kila mmoja ajitishwe mwenyeweKuna watu wako speed kinoma !! Halafu kwenye kumtwisha mtu naogopa kinoma unaweza ukamtupia mfuko wa cement vibaya ukamvunja !!!
Kazi za viwandani sio simple kabisa Kuna movie Charlie Champlin alikuwa anafanya kiwandani if I'm not wrong ilikuwa inaitwa modern times ilikuwa inatakiwa aende na speed ya mkanda matokeo yake alipata pyschology effects.we bwana wewe,ukiskia mtu anafanya kazi flani kisa inaonekana ndogo unahsi simple sana eeeh
Mkuu kuna kazi unapewa kiwandani,kazi ya kuosha tu chupa mjomba ukskia kuosha chupa
unahsi simpooooo, try and see uje utusimulie... Kitu chochote mtu anachotoa pesa ili ukifanye
jiulize mara mbili mbili "why" kaamua akulipe ufanye,ingekua rahisi angefanya mwenyewe mkuu.
Some time that's nasemega Kama Mungu amekupitisha yote alafu akakufungulia Milango , usijinyime Sana , FANYA maendeleo but pata mda wa kurelax,Kuna siku nipo maskani nishachoka zanguu,akaja jamaa akasema anaeweza kuchezea mavi twende kuna kazi huko,,
Nikamuuliza kazi gani? akasema mwenye nyumba anataka chemba ya choo tuchote mavi yote na ndooo tukamwage kwenye shamba lake ili ile chemba iongezwe urefu yani pale ilipo ifukuliwe zaidi kwenda chini..
ila huwezi kufukua zaidi bila kutoa kinyesi chote, tukamwambia si aite tu gari ya kunyonya mavi inyonye, Akasema njia ya kufika kwake gari ya mavi haifiki na hata wakifosi gharama ni kubwa mno inafika 1m na huyo mzee hiyo hela hana..
hivyo mzee katoa ofa ya watu kuchota mzgo wote na ndoo na kwenda kuumwaga huko shambani kwake, Tukauliza OFA yake sh ngapi?
Jamaa akasema kazi tunaifanya watu wa 4 tu mzee kasema atatoa 100,000 kwa kila mtu,jamaa mmoja akasema mwambie aongeze walau iwe 150,000 tukapge kazi, nazama chumvini nalamba inye live na ulimi sembuse hiyo harufu inishinde? mwambie aongeze dau...
Jamaa akavuta simu kwa mshua akamwambia vijana wa kazi wamepatikana ila wanasema 100k haitoshi waongeze 50k iwe 150k, mzee akajibu Sawa njooni.
Jamaa akasema oyaa mshua kakubali, Huyo mwingine akawambia sasa sikilizeni hapa tunaenda nunua mafuta ya Taaa kidumu cha lita 5 tunamwaga mwaga mule kwenye chema mote Harufu inakata kazi tunapga freshi..
Kusikia hivyo tukaona jamaa katoa idea nzuri sana,kweli haooo hadi kwa mangi tukanunua mafuta ya taaa haooo safari ikaanza kwenda site.
Tumefika tukaenda kwenye chemba, ilikua tayari ishabomolewa lile zege la juu hivyo limebaki shimo pana tu unaona inye live live,mafinyo finyo live live, Jamaa akamwaga mafuta ya taaa pwaaaaaa koteee..
Tukaletewa ndooo kila mtu na ndoo yake,gloves kazi ikaanza nikadumbukiza nikachota ndoo ya kwanza nikatoa,jamani jamani jamani nilienda kumwaga shambani nikapitiliza huko huko sikurudi nyuma tena.
Asee inye isikieni tu,ile 150,000 nikaona wala isinipe presha mimi,na niikose tu siwezzi chezea gwede gwede kama vile ni rost... nimeondoka nimefika maskani nasimulia waliobaki,nusu saa haijaisha namuona mwenzangu mwingine huyu hapa karudi, aaah weee kuna kazi za kufanya bwana sio kazi ya kuchezea tope la binadamu..
🤣🤣🤣🤣🤣Residence za Wahindi ( Vibibi vya kihindi havilali, vinakuchungulia usiku mzima ).
Mshukuru MUNGU kwa yote kama umepitia njia nyororo!!wengine hawana ndugu wala mjomba wa kuwashika mkono,mjomba ni nafsi yako,na ndugu ni mwili wako na viungo vyako vikiwa vizima.Ila kuna kazi ukizifanya unaweza kuwa kichaa kabisa
Hakika mkuu. Kuna time ukiona mtu anaenda kwa sangoma kutafuta za kichawi muache tu kasota shida sio kitu kizuri.Some time that's nasemega Kama Mungu amekupitisha yote alafu akakufungulia Milango , usijinyime Sana , FANYA maendeleo but pata mda wa kurelax,
Watu ambao tumetokea familia za chini mpaka kutoboa tunayapitia Mengi,
Kumbe jf kuna hadi kazi za hivi, mnatuvuruga kwakweli
Kweli mkuu, sisi watu tuliotokea familia za sayari ya tunayapitia Mengi mpaka kutoboa, mbaya unajikuta wewe ndo mtoto wa kwanza,familia ipo na umaskini wa kutupa, unaanza pambana na kukomaa kimaisha hata kabla ya umri,ila bwana Mungu huwa anatupiganiaHakika mkuu. Kuna time ukiona mtu anaenda kwa sangoma kutafuta za kichawi muache tu kasota shida sio kitu kizuri.
Sasa project itakuaje si ulisema una range my wanguHuu ndio Uzi wetu wazee wa kazi, achana na zile mambo sijui range Rover, my house Mara viwanja vikali kumbe hata chai haujaonja, hapa ni wapambanaji. Unasoma nyuzi Hadi unajiona peke Yako ndio umekosea ramani. Watu wote JF mambo matamumatamu.
Nikiweka shughuli zangu hapa jambo letu litaota mbawa, mpango mzima utafariki.
Sasa project itakuaje si ulisema una range my wangu
Mi hiii ningemaliza, 150k ya bureKuna siku nipo maskani nishachoka zanguu,akaja jamaa akasema anaeweza kuchezea mavi twende kuna kazi huko,,