Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
kabisaa mkuu!. Hela unaona haifai bora ukimbie uachane na hela uokoe uhai wako[emoji16]Mzee wa Mmaa umetendea haki nia ya Uzi huu,nilitaka visa vya namna hiyo
yani unapga kazi unaona kabisa noo hiyo hela wasinipe,uhai wangu n wathamani sanaaa [emoji23] [emoji23]
Daaaah teacher kumbe ni wewe daaah pole sana [emoji23] ulikua una fundisha pale ubungo ukatia mtoto mimba ukatimuliwa kazi ukafungua kiduka madale kule daah pole sana maisha hayana formula oneSio kila hustle wife ajue eti kisa mnapendana. Kuna misala mingi kama mwanaume unatakiwa usimame mwenyewe tu mradi wao wasilale njaa. Kusema kila kitu sio uanaume. Binafsi nilipataga msala job wife alijua nipo likizo ndio baadae nikamwambia nimesimamishwa kazi. Hata baadae nilipotimuliwa alijua ni kwa sababu niliyokua nimemwambia kumbe sababu ni nyingine kabisa ambayo alikuja kuijua kama 4yrs later wakati maisha yalishasonga kivingine. Alijua baada ya kufungua makabrasha yangu kwenye briefcase alishangaa sana kujua kumbe nilikua na msala mkubwa kiasi kile na niliwezaje kupretend niko normal. Ulikua msala mzito wa kula mvua za kutosha ila niliupangua kivyangu na hadi leo akiniangalia hanimalizi
You cant hide upendo wako kwa mtu uliempendaga buanaaa,tena uliempenda bila kuamrishwa 😂Kuna muda nakupendaga sana ukiacha kile kipengele kimoja tu 😂😂😂
You are so real.
Yani kabisa, unatoka hapo kila kona ya mwili inaumaaaaa.Hata dushe inakimbilia ndaniiii daaah sitasahau ile kazi ya saidia fundi jamani.Aliyeugundua mchanganyiko wa kokoto, mchanga, saruji na maji, visa yake ya mbinguni itasumbua sana
Hajakosea nina hakika,unashangaa hiyo mkuu wakati kuna kiwanda malipo1850 tsh kwa siku??au umekosea kuandika.
#MaendeleoHayanaChama
Asante mkuu,katika kazi naziheshimu hii dunia ni kazi wanazofanya walinziall in all pole sana
Ukaona ya nini kujifiaKuna siku nipo maskani nishachoka zanguu,akaja jamaa akasema anaeweza kuchezea mavi twende kuna kazi huko,,
Nikamuuliza kazi gani? akasema mwenye nyumba anataka chemba ya choo tuchote mavi yote na ndooo tukamwage kwenye shamba lake ili ile chemba iongezwe urefu yani pale ilipo ifukuliwe zaidi kwenda chini..
ila huwezi kufukua zaidi bila kutoa kinyesi chote, tukamwambia si aite tu gari ya kunyonya mavi inyonye, Akasema njia ya kufika kwake gari ya mavi haifiki na hata wakifosi gharama ni kubwa mno inafika 1m na huyo mzee hiyo hela hana..
hivyo mzee katoa ofa ya watu kuchota mzgo wote na ndoo na kwenda kuumwaga huko shambani kwake, Tukauliza OFA yake sh ngapi?
Jamaa akasema kazi tunaifanya watu wa 4 tu mzee kasema atatoa 100,000 kwa kila mtu,jamaa mmoja akasema mwambie aongeze walau iwe 150,000 tukapge kazi, nazama chumvini nalamba inye live na ulimi sembuse hiyo harufu inishinde? mwambie aongeze dau...
Jamaa akavuta simu kwa mshua akamwambia vijana wa kazi wamepatikana ila wanasema 100k haitoshi waongeze 50k iwe 150k, mzee akajibu Sawa njooni.
Jamaa akasema oyaa mshua kakubali, Huyo mwingine akawambia sasa sikilizeni hapa tunaenda nunua mafuta ya Taaa kidumu cha lita 5 tunamwaga mwaga mule kwenye chema mote Harufu inakata kazi tunapga freshi..
Kusikia hivyo tukaona jamaa katoa idea nzuri sana,kweli haooo hadi kwa mangi tukanunua mafuta ya taaa haooo safari ikaanza kwenda site.
Tumefika tukaenda kwenye chemba, ilikua tayari ishabomolewa lile zege la juu hivyo limebaki shimo pana tu unaona inye live live,mafinyo finyo live live, Jamaa akamwaga mafuta ya taaa pwaaaaaa koteee..
Tukaletewa ndooo kila mtu na ndoo yake,gloves kazi ikaanza nikadumbukiza nikachota ndoo ya kwanza nikatoa,jamani jamani jamani nilienda kumwaga shambani nikapitiliza huko huko sikurudi nyuma tena.
Asee inye isikieni tu,ile 150,000 nikaona wala isinipe presha mimi,na niikose tu siwezzi chezea gwede gwede kama vile ni rost... nimeondoka nimefika maskani nasimulia waliobaki,nusu saa haijaisha namuona mwenzangu mwingine huyu hapa karudi, aaah weee kuna kazi za kufanya bwana sio kazi ya kuchezea tope la binadamu..
Dah nimecheka Sana pole Sana mkuu"UTAPIGA KAZI MPAKA UITEE MMAA"
Nakumbuka enzi zile sina mishe yoyote na nasaka pesa.niliamka asubuhi moja na kuiingia mtaani, kupita mtaa fulani nkaona watu wamesimama nje ya geti ya site ya ujenzi wanahesabiwa.
Nikaona wanapangiwa kazi za kufanya, walikuwa watu kati 40 mpaka 50 hivi.Kidume mbio nkajipenyeza.
Sasa yule Mhandisi(nilikuja kumjua badae) aliyekuwa anahesabu watu na kupanga majukumu akaniweka kwenye kundi la 2( watu 23 maana yake tukawekwa magroup ma2 ya watu 23, 23 kama sikosei).
nikasikia yule mhandisi anatoa majukumu kwa group letu kuwa "" nyinyi wazee ni wazee wa MMAA"" na natoa 40,000 kwa kila mmoja kazi ikiisha.
Daah kusikia 40,000, nkaona kazi si ndo hii jamani.
Ila sasa sikuelewa alivyomaanisha "wazee wa mmaa",
kumbe banaaa ni wazee wa zege la jamvi la juu ya GHOROFA ya tatu.zege la kukesha, zege la kufa mtu,aaah manina
wenzetu wao yani kundi la pili wao ni kazi za chini.
*****************************************
Picha linaanza tulianza kupakua mifuko kama 300 ya cement, mchanga lori, kokoto lori, mixer na gari la maji .halafu kilichonitisha walishusha ndoo kubwakubwa za kubebea zege kama 200 hivi.
AISEEEEE, AISEEEE. ndo nilijua kwanini sisi tunaitwa"" wazee wa MMAAA" yani utapiga kazi mpaka uombe maji kama mtoto.
Zege linakorogwa chini unalipandisha kwa kichwa mpaka ghorofa ya 3.MANINAAAAAA
nilipiga trip kama 6 hivi,nikiwa napandisha trip ya 6, nkasikia lijamaa limoja eti kwann mimi mchumba nimekuja kwenye kazi za wanaume. Niliumia sana, nkajikaza trip kama 5 zingine.
ile trip ya mwisho, nkasikia shingo imekaza.[emoji16][emoji16][emoji16]nikajiuliza kwanini nifie site??
Nilimuaga msimamizi kuwa naiingia toilet 2mins , Akajibu ""chapu chapu dogo huu si muda wa kulemba kanye huku umesimama maana hii ngoma tunakesha mpaka uitee mmaa""
nilivyokata kona, nilikimbia mnooooo,zile trip 11 nilizopiga niliumwa 2 days[emoji2]
Sikuwahi kufanya kazi ya zege tena.
Kwa jinsi nilivyo- kila nkimhadithia wife kuwa nilipiga kazi za hovyo huwa anakataaa sanaaa, sijui why but anyway.
wakuu tusikate tamaaa maishani.
"wazee wa mmaa"[emoji23][emoji23]
Mkuu hii ya ujenzi bora kwa waswahili wenzetu kwa mhindi au mchina wanaua mzee kaI mlima malipp kijikoAsante sana mtoa mada !! Nyakati kama hizo za kupambania kombe mwanaume unakua umejikataa kabisa !!
Mimi kazi ngumu niliyosema sitawahi kurudi ni kazi ya ujenzi !! Siku moja nikasema ngoja nikacheki site !! Nilivyofika nikakuta wahuni washaanza kazi ila yule msimamizi akanambia Dogo subiri hapa nyie mtashusha Cement ! Mara Gari likaingia limefunga mifuko 400 ya cement nilikua na mwanagu mmoja tukapata na mtu mmoja tukawa watatu
Tunahamisha mifuko kutoka kwenye gari kuipeleka store moja inawekwa kwa kupangwa kwenda tuliahidiwa kila mfuko tunaubeba kwa sh 100 hivyo tuna 40k tugawane !! Nilichubuka sana maeneo ya mgongo !! Kesho sikurudi
Nikaenda site nyingine huko nilikuta ndo wanatengeneza foundation ya chini kabisa ya Ghorofa , kwa hiyo ilikua kumwaga zege wenyewe wanaita "Ghala' tulipiga kazi toka saa mbili asubuhi unaambiwa zege hailali mpaka saa sita usiku muhindi akatulipa 12500.
Ila kuna watu wanakua wameridhika na kazi tu fresh
Da kweli mkuu ,kazi ukishaipitia lazima twaswira na huruma itakujia , ila sio wote hufikili haya mkuu, Sema ni Mungu amekuinua na kutambua ulipotoka ndo maana unawatendea yaliyo mazuri walinzi wakoAsante mkuu,katika kazi naziheshimu hii dunia ni kazi wanazofanya walinzi
binafsi siamini mlinzi 1,huwezi linda kwangu uwe peke ako,pili siwezi kubali mlinzi
wangu apate mshahara mdogo,ki ufupi nawajali walinzi wangu mpka wanashangaaga
wananiona nina pesa labda,ila ukweli ni kwamba naelewa msoto wanaopitia usiku
hasa vipindi vya mvua na baridi,yani walinzi na waheshimiwe ile kazi ni ngumu sana sana sana..