Kuna siku nipo maskani nishachoka zanguu,akaja jamaa akasema anaeweza kuchezea mavi twende kuna kazi huko,,
Nikamuuliza kazi gani? akasema mwenye nyumba anataka chemba ya choo tuchote mavi yote na ndooo tukamwage kwenye shamba lake ili ile chemba iongezwe urefu yani pale ilipo ifukuliwe zaidi kwenda chini..
ila huwezi kufukua zaidi bila kutoa kinyesi chote, tukamwambia si aite tu gari ya kunyonya mavi inyonye, Akasema njia ya kufika kwake gari ya mavi haifiki na hata wakifosi gharama ni kubwa mno inafika 1m na huyo mzee hiyo hela hana..
hivyo mzee katoa ofa ya watu kuchota mzgo wote na ndoo na kwenda kuumwaga huko shambani kwake, Tukauliza OFA yake sh ngapi?
Jamaa akasema kazi tunaifanya watu wa 4 tu mzee kasema atatoa 100,000 kwa kila mtu,jamaa mmoja akasema mwambie aongeze walau iwe 150,000 tukapge kazi, nazama chumvini nalamba inye live na ulimi sembuse hiyo harufu inishinde? mwambie aongeze dau...
Jamaa akavuta simu kwa mshua akamwambia vijana wa kazi wamepatikana ila wanasema 100k haitoshi waongeze 50k iwe 150k, mzee akajibu Sawa njooni.
Jamaa akasema oyaa mshua kakubali, Huyo mwingine akawambia sasa sikilizeni hapa tunaenda nunua mafuta ya Taaa kidumu cha lita 5 tunamwaga mwaga mule kwenye chema mote Harufu inakata kazi tunapga freshi..
Kusikia hivyo tukaona jamaa katoa idea nzuri sana,kweli haooo hadi kwa mangi tukanunua mafuta ya taaa haooo safari ikaanza kwenda site.
Tumefika tukaenda kwenye chemba, ilikua tayari ishabomolewa lile zege la juu hivyo limebaki shimo pana tu unaona inye live live,mafinyo finyo live live, Jamaa akamwaga mafuta ya taaa pwaaaaaa koteee..
Tukaletewa ndooo kila mtu na ndoo yake,gloves kazi ikaanza nikadumbukiza nikachota ndoo ya kwanza nikatoa,jamani jamani jamani nilienda kumwaga shambani nikapitiliza huko huko sikurudi nyuma tena.
Asee inye isikieni tu,ile 150,000 nikaona wala isinipe presha mimi,na niikose tu siwezzi chezea gwede gwede kama vile ni rost... nimeondoka nimefika maskani nasimulia waliobaki,nusu saa haijaisha namuona mwenzangu mwingine huyu hapa karudi, aaah weee kuna kazi za kufanya bwana sio kazi ya kuchezea tope la binadamu..