Kazi nilizowahi zifanya na zikanishinda kwenye utafutaji

[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28] pole sana...daah kweli ajira tatizo 3500 kwa siku?

#MaendeleoHayanaChama
 
Kwa kweli watoto wa kwanza huwa mnapitia mengi sana. Unakuta wewe ndio kiongozi wa wadogo zako ,wakati huo huo maisha ya wazazi yanakuwa hayajakaa sawa kwahiyo inakubidi utoe support.
 
enzi hizo nimemaliza high school nikaamua kusaka kibarua ili niweze kukidhi mahitaji yangu wakati nasubiria matokeo.

Kuna sehemu nilikua nakuta watu kibao asubuhi wakati naenda shule. Walikua wanasubiria matajiri wenye mashamba wanaenda kupiga day work kwa malipo ya 4000 per day.
Msimu wa mavuno ya mpunga huo,mazee nikajilipua kwenda pale. Mama mmoja akanichagua na team ya watu 10 kwenda kumvunia shambani kwake.


Kufika pale tukapewa vikwakwa,yani mnakata mpunga mnabeba na kuukusanya sehem maalum kwa ajili ya kupigwa. Kazi ni ya kuinama inuka siku nzima. Mpunga pia unawasha hatari, 2 hours later nilitembea kwa mguu kurudi town. Hakikua kikombe changu kile.
 
We jamaa unetisha sana yaani nimecheka kama mwehu[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Kisa cha pili. Somewhere Mkoa wa pwani.

Nimezurura weee nikawaona jamaa wanajaza kifusi kwa mchina nikajisemea acha nijaribu kazi ilikua ishafika nusu. Jamaa mmoja wa dodoma bahi mwingine wakutoka kigoma nikaongea na mchina akanidirect kwa hao jamaa niunge nao maana kazi walianza na wengine wakashindwa wakala kona.

Basi bwana jamaa wakakubali tukagawana majukumu mm nachimba wao wana beba kwa toroli afu wanapeleka kujaza kwenye jengo kwa chini. Sasa hesabu ilikua siku moja kazi tunaua. Bwana weee siku ile ikakata hatujamaliza kesho tukapiga tena sisi tukaona hapa tayari pashakaa level. Mchina anaesimamia anakuja jioni anasema hapa kuna mabonde jazeni tena.

Kudadeki muda huo mikono imepasuka mno. Tukajaza ile ile jioni kibingwa pakawa level. Kimbembe kwenye kulipwa siku hiyo ikapita tukaambiwa mje kesho mapema tu mchukue chenu bwana wee kesho huyoo tumefika saa 4 wengine saa 5 aisee tumesubiria wee hela hatupewi tukiuliza oooh mpaka mchina/boss mkuu asaini na hayupo. Dadadeki muda huo nishajichokea. Basi bwana siku hiyo nayo ikakata tukaja kesho nyingine tena kudai hela sasa mapema tu.

Jamaa wanatuangalia afu wanatuzunguka oohh subirini mpaka jioni. Tukaona hawa chenga chenga nyingi. Nikawaambia jamaa mm niliunga katikati kwenye hii kazi hivyo utata anzisheni mm.nitapump tulipwe. Kama kawaida siku zote waoga ndio wanaonewa. Jamaa mmoja yeye anasema aah tuombe kwa ustaarabu nikamjibu hapa hatuombo tunadai jasho letu.

Jamaa wa kigoma nikamsanua nikamwambia hapa tufanye kamgome flani chukua chepe na mm chepe tunarusha hiki kifusi nje barabara ya kuingia kwenye miradi yao pale. Bwana tukarusha kama chepe 3 tu mchia huyu. Acheni acheni tukamjibu kama hela hamna acha tukilipe kwa njia hii kuacha kwetu ni utulipe.

Aisee haizikupita dakika 5 yule meneja alikua dada wa kichina katoka huyo kaenda bank crdb jirani tu pale pale yaani hata dakika moja haishi ashafika benk akafanya yake huko dakika kama 15 au 20 huyu hapa akampa yule msimamizi alitupa kazi hela atulipe. Ikaisha hiyo. Ila nyieee acheni tu. Watu wanaopambana bila kuinuliwa au kushikwa mkono wanapitia mengi.
 
Inauma sana sana ,kufanya kazi halafu usilipwe au ucheleweshewe mshahara#INAUMA SANA
 
Aiseee
 
Shida si sifa
 
Kazi ya ujenzi


Bwana nimetoka fresh from chuo hapo nikakaa home week hapasomeki na wana kitaa uliowaacha nyuma ndio hivyo wako Bize basi nikamvuta mmoja nikamwambia akienda asubuhi anichukue

Kweli bwana wanasema mtu hakunyimi kazi ngumu

Kazi ilikuwa ya zege .. kwakweli aliyeumba zege anakatwa na mandonga [emoji3] bado kubeba simenti kuzitoa kwenye gari kuzipeleka juu ghorofani nyie acheni kila tukifika floor moja tunapumzka tunahema na ulimi nje kama mbwa nilikutana na mchomvu mwenzangu tukawa tunashika huku na huku ukitoka hapo vidole havikunji

Bado kwenye pesa mara ya kwanza nililipwa vzr tu kila siku ikafikia kipindi nakaa siku mbili au siku tatu ndio nilipwe hela zote huyo huyo fundi mkuu mlipaji anakukopa hela ya vocha [emoji3] au nauli siku nyengine utaskia dogo hauna buku 2000 leo kaka yako usiku nile siku nilivyolipwa hela yangu ya siku tatu sikurudi tena mambo ya kurudi nyumbani umepauka na cement mgongo na kiuno unauma hela hauna sikuyaweza


Na mafundi wakuu wanapata sana pesa tatizo chupi [emoji3] hawa jamaa hawana tofauti na askari
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…