Nilijua tu hili lazima litaibuka.....Kuna muda nakupendaga sana ukiacha kile kipengele kimoja tu πππ
You are so real.
Don't take JF too seriousMaisha bwana, mkuu umetoa story inauma, ila pia nimecheka mpaka wenzangu wakaniangalia , maana nimefikilia kitendo Cha kuwambia vibaka,mnafanya nini, nakutumbukia kwenye pipa, Sasa nikafikili vipi Kama wangeamua kukufuata kwenye pipa lako jisui ingekuaje, ila pia inawezekana ulitumiwa watu makusudi kukutest maana si ulikua mgeni, kujua Kama umelala au but all in all pole sana
Bakayoko ? Mmmmmmh kama namjua ila fresh acha ipite never mind.[emoji23][emoji23][emoji23] umenikumbusha jamaa angu mmoja wa kuitwa bakayoko nakumbukuka aliingia site akiwa nywele fresh tu lakini mpaka kazi ya kumwaga zege inaisha mwamba nywele za katikati ya kichwa akawa hana
unaupiga mwingi mkuu.[emoji16][emoji16]Ile wanaita mavi ya mse..nge, kitu laini lazima uchechemee, kupiga ile kazi wanaume wanavaa madela, magauni nk kuepuka michubuko mapajani ile kupanda na kushuka ngazi ukiwa na ndoo ya zege kichwani. Unapandisha na kushuka huku wanaimba au unaambiwa tafuta pesa malaya akale kuku. Daaaah si mchezo ..... Wengine tukisimulia hapa bendera inaweza shushwa nusu mlingoti mateso, manyanyaso, utapeli visa, mpaka vifo site hizi za ujenzi but still we are pushing hard .
Buku kwa siku??itakupeleka wapi?huwezi kuelewa we mtoto wa kishua.kuna watu maeneo wanalipwa buku per day.
Ni kweli kabisa mishahara mdogo ya hao walinzi inashawishi wao kuwa wadokozi, nimeshuhudia miaka ya nyuma baadhi ya vitu vya zile hotel kubwa za Dar na JKNIA vikiuzwa mitaani hasa vijiko Uma na glass zenye nembo za hotel hizo au mashirika ya ndege, nilipoulizia mara nyingi jamaa wanasema wanauziwa na walinzi na staffs wa kule kufidia malipo madogo ya mishaharaKampuni za ulinzi zina wanyonya sana walinzi,ndio mana sipo tayari kulindiwa na kampuni
Mishahara ni midogo mno halafu vitu vinavyolindwa vinamshawishi hata mlinzi mwenyewe
awe mwizi,yani ukilindiwa na kampuni usipokua makini ukajiachia unaibiwa na mlinzi wao huyo huyo
Makampun haya yanatesa watu mno,mtu ukiwa na tamaa mbona badala ya kulinda unaiba tuu ujilipe.
Mkuu, siwezi potezwa na jf , najua vizuri jf ni jukwaa limebeba watu wa kila aina, watukutu, wahongo,vipenyo, wakweli, wanamapambio, n.k but vipo vitu mtu akiandika vinakugusa MOJA KWa MOJA bila kujali nia ya mtoa mada yoyote, na Kama mada inaendana na hualisia lazima utapata hisia fulaniDon't take JF too serious
Utapotezwa.
Aisee cement ni nzito bwana asikwambie mtuAisee nimeekumbuka na mimi...ukisikia kazi ya kushusha cement wala usisogee.,nakumbuka 2017 nilipita sehemu nikakuta kuna semi nyingi zimepack,,,vijana wakiendelea na kazi za kupakua cement toka kwenye gari mpka store....aaah mm hapo sijala tokea jana afu njaa inauma nikajisemea ngoja nikomae hapa nipate 15000 niishi...duu...nakumbuka nilibeba mifuko 30 wakt hapo nishachoka balaa jasho kila mahali..mda huo speed imepungua miguu inatetemeka balaa..nilivochukua mfuko wa 31 nilidondoka nao na kazi ikaishiaa hapohapo nikapepewa buku mbili nakumbuka ..
Nilichogundua sio swala la nguvu pale ...mana nguvu nilikuwa nazo isipokuwa ni uzoefu
Kweli. Wale mafundi wanahonga mzee sio poaKazi ya ujenzi
Bwana nimetoka fresh from chuo hapo nikakaa home week hapasomeki na wana kitaa uliowaacha nyuma ndio hivyo wako Bize basi nikamvuta mmoja nikamwambia akienda asubuhi anichukue
Kweli bwana wanasema mtu hakunyimi kazi ngumu
Kazi ilikuwa ya zege .. kwakweli aliyeumba zege anakatwa na mandonga [emoji3] bado kubeba simenti kuzitoa kwenye gari kuzipeleka juu ghorofani nyie acheni kila tukifika floor moja tunapumzka tunahema na ulimi nje kama mbwa nilikutana na mchomvu mwenzangu tukawa tunashika huku na huku ukitoka hapo vidole havikunji
Bado kwenye pesa mara ya kwanza nililipwa vzr tu kila siku ikafikia kipindi nakaa siku mbili au siku tatu ndio nilipwe hela zote huyo huyo fundi mkuu mlipaji anakukopa hela ya vocha [emoji3] au nauli siku nyengine utaskia dogo hauna buku 2000 leo kaka yako usiku nile siku nilivyolipwa hela yangu ya siku tatu sikurudi tena mambo ya kurudi nyumbani umepauka na cement mgongo na kiuno unauma hela hauna sikuyaweza
Na mafundi wakuu wanapata sana pesa tatizo chupi [emoji3] hawa jamaa hawana tofauti na askari
Noma saana. Au ile kupasua zege lilokauka afu la kiwandani kwa sururu na nyundo kubwa. Aisee hizo kazi zinataka watu waliokomaa haswaa. Unapiga nyundo inaruka unapiga sururu inaruka mpaka utoboe hiyo layer aisee mikono imepasuka sio poaKuna kazi ya kuchimba lami kwa sururu ili kupata mtaro mzee mikono inakatika unashika sururu mpaka unasikia vidole vinaishiwa nguvu....hii tulipelekwa kufanya mbagala charambe aisee! Kesho sikurudi....hadi unajiuliza kwa nini wamwage kifusi wakandamize halafu ndio mje kuchimba unapata jibu hizo ni fakin job wanaofanya hawana pa kukimbilia ni shida zao ndio zinawatesa.
unaupiga mwingi mkuu.[emoji16][emoji16]
Matusi, nyimbo vimbwanga vingi mno kwenye zege za maghorofa.
Ila ningendelea na ile kazi nahisi ningemaliza salama.
wanakuambia mtu mzima
"ubwabwa utaitaa uwawa" kwa kazi ile iilivyongumu