Kazi nilizowahi zifanya na zikanishinda kwenye utafutaji

[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]maisha ni mapambano
 
1. Nimewahi pelekwa kusomba magogo ya mbao huko makete Safari ilianza usiku kwenda huko makete tulikua wanne Ila hatujuani njiani mi nikalala nashtuka jamaa ndo anasema tumefika ilikua Kama sa 9 usiku asubuhi tukakabidhiwa kazi yakutoa magogo bondeni kupeleka seheme nzuri mziki ulikua so mdogo siku ya kwanza nikakomaa siku ya pili nikakomaa Ila mabega yakawa yamegandisha damu siku ya tatu nikaona hapana na Kama ni hela Bora nisamehe tu nikaaga ngoja ninywe maji nikapotelea hukohuko na ubaya nilikuwa sikujui ikabidi nitembee niikute barabara nikatembea hadi naikuta shughuri ikaanza Sasa nitaenda wapi wakati sikufahamu Kuna mda nikawa najifariji hata nikipotea lakini bado nipo Tanzania katika harakati za kutembea nikaona gari inakuja zile zenye usajili wa DFPA nikapiga mkono ikasimama nikaomba msaada wakanipakia wakasema tunaenda kutokea mbeya nikasema sawa mniache mbeya mjini nikafika wakaniacha pale

2. Kazi ya kupandisha nzege ghorafa ya tatu nilifanya siku 1 nikaona Kama mgongo unataka kutumbukia ndani ya tumbo nikakomaa Hadi nalipwa kwa siku ilikua elfu 10 nilivomaliza nikaenda kununua Panadol na maji ya 500 ajabu kufungua mfuniko wa maji na mikono nikashindwa kabisa

3. Kiwanda Cha mikate nako kunashughuli kwelikweli.....

Nitaimalizia
 
Buku kwa siku??itakupeleka wapi?

#MaendeleoHayanaChama
[emoji3] mwenzangu na ww shangaa,kaz nyingine ni bora hata ujilipue,[emoji1787] uwe gaid tu alqaeda ujilipe mamilioni yako kibabe zaidi ,unatusua mapema,sio unakaa kinyonge bhn [emoji3]buku kweli ??!
 
Daah..kwamba ilimradi ufike mbeya..[emoji28][emoji28] mkuu ungeomba hata pesa ya siku ulizofanya kazi.

#MaendeleoHayanaChama
 
Kuingia kwenye sept tank ya mavi kusafisha...
Wanavuta maji na kinyesi chote, unashushwa ukakoroge udongo wote,
Horse ya gari inaendelea vuta, kazi yako kuisogeza...

Joto lake si la nchi hii, lazima umwagiwe maji ukiwa huko huko chini...

Kazi yenyewe ina udalali kuanzia pale Sayansi mtu anachukua 100,000 anakupa 30,000

NB: Nimeshuhudia mara 2
 
mkuu ungeomba hata pesa ya siku ulizofanya kazi.
Unajua kwanini watu wanaachaga malipo na kuondoka kimya kimya?!

Ni kwasababu ukienda omba malipo utaonekana mzembe na hata kama bosi

akisema akupe atakupa huku akikusema (siku nyingine acheni kukimbilia kazi za wanaume) Ulikua unajijua mtoto wa mama ulikuja kufanya nini hapa?

yani kuna maneno flani utatamkiwa hadi unaweza juta kufata hayo malipo, Sasa kwakua wengi tushajua kifuatacho ni kitu gani, Huwa tunajikataaa kimya kimya.

Maboss wengine umwambie umeshindwa kazi anakulipisha hela ya vifaa alivyowanunulia,mfano mimi ile kazi ya kuchota mavi kwenye chemba Boss alienda nunua gloves,ndooo,Boots akatuletea akiamini ni majembe ya kazi..

Mimi yakanishinda nikakimbia,hivi boss kama huyu umfate umwambie nilipe hata kidogo unafkiri kifuatacho nini?

Mkuu kuna maboss hawapendi kubipiwa kabisa wako serious wanataka kuona matendo na utimize ulichosema utafanya,sasa wewe itikia unaweza halafu fanya yakushinde halafu kadai malipo uone boss atapokupeleka!

Mungu hakukosea kukuumba na miguu mkuu,misala kama hiyo unaikimbia tu Hela kitu gani mzee
 
Unaonekana kwenye kukimbia upo vizuri,huna baya.
 
Noma saana. Au ile kupasua zege lilokauka afu la kiwandani kwa sururu na nyundo kubwa. Aisee hizo kazi zinataka watu waliokomaa haswaa. Unapiga nyundo inaruka unapiga sururu inaruka mpaka utoboe hiyo layer aisee mikono imepasuka sio poa
Ni hatari tupu...kuna kazi zingine yaani kama zina laana....maana mpaka uje umalize umekufa mwili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…