atlas copco
JF-Expert Member
- Jun 15, 2015
- 8,497
- 9,728
Junior acha usumbufu basiHii ni chai ila inafurahisha
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Junior acha usumbufu basiHii ni chai ila inafurahisha
Umenichekeshaa Sana[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]Kumbe jf kuna hadi kazi za hivi, mnatuvuruga kwakweli
[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]maisha ni mapambano"UTAPIGA KAZI MPAKA UITEE MMAA"
Nakumbuka enzi zile sina mishe yoyote na nasaka pesa.niliamka asubuhi moja na kuiingia mtaani, kupita mtaa fulani nkaona watu wamesimama nje ya geti ya site ya ujenzi wanahesabiwa.
Nikaona wanapangiwa kazi za kufanya, walikuwa watu kati 40 mpaka 50 hivi.Kidume mbio nkajipenyeza.
Sasa yule Mhandisi(nilikuja kumjua badae) aliyekuwa anahesabu watu na kupanga majukumu akaniweka kwenye kundi la 2( watu 23 maana yake tukawekwa magroup ma2 ya watu 23, 23 kama sikosei).
nikasikia yule mhandisi anatoa majukumu kwa group letu kuwa "" nyinyi wazee ni wazee wa MMAA"" na natoa 40,000 kwa kila mmoja kazi ikiisha.
Daah kusikia 40,000, nkaona kazi si ndo hii jamani.
Ila sasa sikuelewa alivyomaanisha "wazee wa mmaa",
kumbe banaaa ni wazee wa zege la jamvi la juu ya GHOROFA ya tatu.zege la kukesha, zege la kufa mtu,aaah manina
wenzetu wao yani kundi la pili wao ni kazi za chini.
*****************************************
Picha linaanza tulianza kupakua mifuko kama 300 ya cement, mchanga lori, kokoto lori, mixer na gari la maji .halafu kilichonitisha walishusha ndoo kubwakubwa za kubebea zege kama 200 hivi.
AISEEEEE, AISEEEE. ndo nilijua kwanini sisi tunaitwa"" wazee wa MMAAA" yani utapiga kazi mpaka uombe maji kama mtoto.
Zege linakorogwa chini unalipandisha kwa kichwa mpaka ghorofa ya 3.MANINAAAAAA
nilipiga trip kama 6 hivi,nikiwa napandisha trip ya 6, nkasikia lijamaa limoja eti kwann mimi mchumba nimekuja kwenye kazi za wanaume. Niliumia sana, nkajikaza trip kama 5 zingine.
ile trip ya mwisho, nkasikia shingo imekaza.[emoji16][emoji16][emoji16]nikajiuliza kwanini nifie site??
Nilimuaga msimamizi kuwa naiingia toilet 2mins , Akajibu ""chapu chapu dogo huu si muda wa kulemba kanye huku umesimama maana hii ngoma tunakesha mpaka uitee mmaa""
nilivyokata kona, nilikimbia mnooooo,zile trip 11 nilizopiga niliumwa 2 days[emoji2]
Sikuwahi kufanya kazi ya zege tena.
Kwa jinsi nilivyo- kila nkimhadithia wife kuwa nilipiga kazi za hovyo huwa anakataaa sanaaa, sijui why but anyway.
wakuu tusikate tamaaa maishani.
"wazee wa mmaa"[emoji23][emoji23]
We mzee turudi kwenye uzi wetu kule 🤣🤣🤣[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Kwa umbali ule nilikuwa naona kama vile tayari nimeshaingia mbinguni!!Mzee umenichekesha kweli,ulikua unahisi kama unawafata malaika huko huko walipo sio
Hapana hiyo ilikuwa pemba huko!!!Bububuu
[emoji23][emoji23]kwel aisee,Alikuwa sahihi ukimuokoa mtu ambaye hajui kuogelea usipokuwa makini mnakufa wote
Kuna namna fulani akikukamata anakurudisha chini na hakuachiii ng'o hata Umpige teke [emoji3]
[emoji3] mwenzangu na ww shangaa,kaz nyingine ni bora hata ujilipue,[emoji1787] uwe gaid tu alqaeda ujilipe mamilioni yako kibabe zaidi ,unatusua mapema,sio unakaa kinyonge bhn [emoji3]buku kweli ??!Buku kwa siku??itakupeleka wapi?
#MaendeleoHayanaChama
Daah..kwamba ilimradi ufike mbeya..[emoji28][emoji28] mkuu ungeomba hata pesa ya siku ulizofanya kazi.1. Nimewahi pelekwa kusomba magogo ya mbao huko makete Safari ilianza usiku kwenda huko makete tulikua wanne Ila hatujuani njiani mi nikalala nashtuka jamaa ndo anasema tumefika ilikua Kama sa 9 usiku asubuhi tukakabidhiwa kazi yakutoa magogo bondeni kupeleka seheme nzuri mziki ulikua so mdogo siku ya kwanza nikakomaa siku ya pili nikakomaa Ila mabega yakawa yamegandisha damu siku ya tatu nikaona hapana na Kama ni hela Bora nisamehe tu nikaaga ngoja ninywe maji nikapotelea hukohuko na ubaya nilikuwa sikujui ikabidi nitembee niikute barabara nikatembea hadi naikuta shughuri ikaanza Sasa nitaenda wapi wakati sikufahamu Kuna mda nikawa najifariji hata nikipotea lakini bado nipo Tanzania katika harakati za kutembea nikaona gari inakuja zile zenye usajili wa DFPA nikapiga mkono ikasimama nikaomba msaada wakanipakia wakasema tunaenda kutokea mbeya nikasema sawa mniache mbeya mjini nikafika wakaniacha pale
2.kazi ya kupandisha nzege ghorafa ya tatu nilifanya siku 1 nikaona Kama mgongo unataka kutumbukia ndani ya tumbo nikakomaa Hadi nalipwa kwa siku ilikua elfu 10 nilivomaliza nikaenda kununua Panadol na maji ya 500 ajabu kufungua mfuniko wa maji na mikono nikashindwa kabisa
3. Kiwanda Cha mikate nako kunashughuli kwelikweli..... Nitaimalizia
Unajua kwanini watu wanaachaga malipo na kuondoka kimya kimya?!mkuu ungeomba hata pesa ya siku ulizofanya kazi.
Unaonekana kwenye kukimbia upo vizuri,huna baya.Unajua kwanini watu wanaachaga malipo na kuondoka kimya kimya?!
Ni kwasababu ukienda omba malipo utaonekana mzembe na hata kama bosi
akisema akupe atakupa huku akikusema (siku nyingine acheni kukimbilia kazi za wanaume) Ulikua unajijua mtoto wa mama ulikuja kufanya nini hapa?
yani kuna maneno flani utatamkiwa hadi unaweza juta kufata hayo malipo, Sasa kwakua wengi tushajua kifuatacho ni kitu gani, Huwa tunajikataaa kimya kimya.
Maboss wengine umwambie umeshindwa kazi anakulipisha hela ya vifaa alivyowanunulia,mfano mimi ile kazi ya kuchota mavi kwenye chemba Boss alienda nunua gloves,ndooo,Boots akatuletea akiamini ni majembe ya kazi..
Mimi yakanishinda nikakimbia,hivi boss kama huyu umfate umwambie nilipe hata kidogo unafkiri kifuatacho nini?
Mkuu kuna maboss hawapendi kubipiwa kabisa wako serious wanataka kuona matendo na utimize ulichosema utafanya,sasa wewe itikia unaweza halafu fanya yakushinde halafu kadai malipo uone boss atapokupeleka!
Mungu hakukosea kukuumba na miguu mkuu,misala kama hiyo unaikimbia tu Hela kitu gani mzee
Ni hatari tupu...kuna kazi zingine yaani kama zina laana....maana mpaka uje umalize umekufa mwili.Noma saana. Au ile kupasua zege lilokauka afu la kiwandani kwa sururu na nyundo kubwa. Aisee hizo kazi zinataka watu waliokomaa haswaa. Unapiga nyundo inaruka unapiga sururu inaruka mpaka utoboe hiyo layer aisee mikono imepasuka sio poa