Kazi nilizowahi zifanya na zikanishinda kwenye utafutaji

Namba 2 kutengeneza zile ngazi za madaraja kwenye barabara ambapo maji yanapita kwa chini

Unabeba mijimawe mikubwa kujaza course ya chini ni elfu 40 mwamba nikatoboa corse ya kwanza inayofuata tena kama unapanda ngazi unabeba mimawe mikubwa kozi ya tatu nili zima [emoji1787]


Nikabeba 80000 nikaaamsha hata kutembea nilikuwa siwezi sikurudi tena
 
Mimi nilipata muscle strain we acha tu
Nikaipiga chini
Mimi kesho yake mikono na vidole nilikuwa kama roboti, yaani kunyoosha mkono au kushika kitu ilikuwa shida.
Nikaenda kufanya vibarua viwandani, nilikuta wadada wanapiga kazi ngumu balaa ukikutana nao mwenge stand ya dala dala utadhani wanafanya kazi ofisini. Malipo ilikuwa 1850 kwa siku kazi masaa 8
 
Duh pole Sana Kwa yaliyokukuta..Nina uhakika haya yalikukuta enzi upo MOFED/Zambia cargo...enzi zile wameweka makontena ya makinikia pale karibu na lile jengo laa..au basi 😄

Ila pole sn Kwa kupitia zile challenge za kufungwa Pingu na kutishiwa na maafisa usalama wa ikulu
 
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]daah
 
3.Kuvua bahari ya upande wa sahare Tanga

Nilikuwa nina shida na nauli nikimbie Lusanga kuna mishe mchizi alinisanua nikapata kazi ya kuvua mwana aliniunga tu picha linaanza jioni ile nikatokea na ka t-shirt kangu manga nyepesi maana tulienda vua maji ya usiku [emoji3] wale wadigo na Wapemba wa ile mashua sijui boat whatever the case .. walikuwa wanacheka

Niligundua kwa nini wanacheka tupo katika ya bahari ule upepo wa baridi niliokuwa napigiwa nao plus yale maji yakikurukia ushapata picha

Kwa nini nilijuta kuna kitu wenyeji wanaita sijui bawa la mvua wataalamu mtaiweka sawa ile maji yanaongezeka yanapanda juu kwa kasi yanavuka hadi kingo za beach ambapo watu wanakaa kunakuwa na maji yanasogea hio ishu ilitukutia usiku plus mawimbi maji yakawa yanaingia kwenye chombo chetu tuna kazi ya kuyatoa na visado boti linapigwa pushi na mawimbi mara chemli imeanguka imepasuka mpemba mmoja akanambia "wajua kuogelea weye ..mimi siokoi ntu nanusuru roho yangu mie " wengine wanakazi ya kutoa maji na visado huku wakisema "shahada" yaani kwa imani ya dini ya kiislamu unaenda peponi ukifa kama utaisema

Nilisema sirudii tena [emoji1787][emoji1787]
 
🤣🤣🤣🤣🤣 Mbavu zangu mie
 
😀😀😀😀umenikumbusha cku nimeeñda kuvua dagaa ziwa Victoria, aisee ulipga upepo mkali huku wanaita MSOKE sema kweli nilipga magoti kutubu dhambi zangu. Ila kesho yake nilirudi make Sikh hiyo tulitoka marundo

Majini paskie tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…