Kazi nilizowahi zifanya na zikanishinda kwenye utafutaji

Namba 2 kutengeneza zile ngazi za madaraja kwenye barabara ambapo maji yanapita kwa chini

Unabeba mijimawe mikubwa kujaza course ya chini ni elfu 40 mwamba nikatoboa corse ya kwanza inayofuata tena kama unapanda ngazi unabeba mimawe mikubwa kozi ya tatu nili zima [emoji1787]

Nikabeba 80000 nikaaamsha hata kutembea nilikuwa siwezi sikurudi tena
 
Mimi nilipata muscle strain we acha tu
Nikaipiga chini
Mimi kesho yake mikono na vidole nilikuwa kama roboti, yaani kunyoosha mkono au kushika kitu ilikuwa shida.
Nikaenda kufanya vibarua viwandani, nilikuta wadada wanapiga kazi ngumu balaa ukikutana nao mwenge stand ya dala dala utadhani wanafanya kazi ofisini. Malipo ilikuwa 1850 kwa siku kazi masaa 8
 
Mimi nimelinda sana, Agakhan University, Agakhan Hospital, Jamatin msikini Kariakoo, Mahotel Kama Serena, New Africa, Ramada, Regency.

Bandari Kama TICTS, IMPALA, MOFED.

Residence za Wahindi ( Vibibi vya kihindi havilali, vinakuchungulia usiku mzima ).

Binafsi, Sina nguvu na Nina mwili mdogo ila Nina UNASIRI TANI 200.

Nilikiwa napiga bit watu wakubwa na wenye vyeo vikubwa sana huweni kuamini.

Nimewahi kumfungia Nje ofisa mkubwa sana wa kampuni, kwasababu nilikuwa namwambia afungue buti la gari nikague hataki.

Nimewahi kutishiwa kupigwa bastola na Maafisa Usalama usiku waliokuwa wanalinda makinikia

Pia, tumewahi kufungwa pingu na watu wa usalama wa Ikulu waliokuwa wamekuja kuchukua sample ya makinikia ya dhahabu tulipokuwa tunalinda.

Kitu kingine, nisichosahau Ni pale kontena la 40 feet, lililojaa KOROSHO zilizobanguliwa lilipoibwa na Bandarini wakakuta mawe, yaani kwenda Polisi na kukaa Mahabusu ilikuwa ni Kama kunywa maji.
Duh pole Sana Kwa yaliyokukuta..Nina uhakika haya yalikukuta enzi upo MOFED/Zambia cargo...enzi zile wameweka makontena ya makinikia pale karibu na lile jengo laa..au basi 😄

Ila pole sn Kwa kupitia zile challenge za kufungwa Pingu na kutishiwa na maafisa usalama wa ikulu
 
Mimi nishawahi kutwa na msala wa gerezani wa kazi flani Ngumu sana kuifanya,nikaona huu ushenzi

hiii kazi nisipoangalia ntaja fia hapa hapa,nikaangalia huku na kule kisha nikajidondosha chini puuuu

nikaanza kurusha miguuu kama nina dege dege,huku natoa mapovu( hapo nishakusanya mate kibaooo)

nikawa nayatema kwa pembeni kidogo kidogo,nikaskia wana wanasema Oyaa huyu atakua ana dege dege

askari akaitwa akaja akasema mbebeni muwekeni pale kivulini,nilipopelekwa kivulini nikasema hapa nikitulia

tuu ntalishwa rungu kwa sana watanishtukia, basi nikazidisha drama nikajirusha kama jongooo nakwambia

askari akaona huu msala atatufia huyu,nikabebwa ikaitwa TAX dakwa speed hadi gerezani,kufika gerezani nikajifanya

napumua haaaaaa huku nakoromaa,ndio ikawa pona yangu ila bila ile tekniki Ningefia pale walahi vile...
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]daah
 
3.Kuvua bahari ya upande wa sahare Tanga

Nilikuwa nina shida na nauli nikimbie Lusanga kuna mishe mchizi alinisanua nikapata kazi ya kuvua mwana aliniunga tu picha linaanza jioni ile nikatokea na ka t-shirt kangu manga nyepesi maana tulienda vua maji ya usiku [emoji3] wale wadigo na Wapemba wa ile mashua sijui boat whatever the case .. walikuwa wanacheka

Niligundua kwa nini wanacheka tupo katika ya bahari ule upepo wa baridi niliokuwa napigiwa nao plus yale maji yakikurukia ushapata picha

Kwa nini nilijuta kuna kitu wenyeji wanaita sijui bawa la mvua wataalamu mtaiweka sawa ile maji yanaongezeka yanapanda juu kwa kasi yanavuka hadi kingo za beach ambapo watu wanakaa kunakuwa na maji yanasogea hio ishu ilitukutia usiku plus mawimbi maji yakawa yanaingia kwenye chombo chetu tuna kazi ya kuyatoa na visado boti linapigwa pushi na mawimbi mara chemli imeanguka imepasuka mpemba mmoja akanambia "wajua kuogelea weye ..mimi siokoi ntu nanusuru roho yangu mie " wengine wanakazi ya kutoa maji na visado huku wakisema "shahada" yaani kwa imani ya dini ya kiislamu unaenda peponi ukifa kama utaisema

Nilisema sirudii tena [emoji1787][emoji1787]
 
Mimi nishawahi kutwa na msala wa gerezani wa kazi flani Ngumu sana kuifanya,nikaona huu ushenzi

hiii kazi nisipoangalia ntaja fia hapa hapa,nikaangalia huku na kule kisha nikajidondosha chini puuuu

nikaanza kurusha miguuu kama nina dege dege,huku natoa mapovu( hapo nishakusanya mate kibaooo)

nikawa nayatema kwa pembeni kidogo kidogo,nikaskia wana wanasema Oyaa huyu atakua ana dege dege

askari akaitwa akaja akasema mbebeni muwekeni pale kivulini,nilipopelekwa kivulini nikasema hapa nikitulia

tuu ntalishwa rungu kwa sana watanishtukia, basi nikazidisha drama nikajirusha kama jongooo nakwambia

askari akaona huu msala atatufia huyu,nikabebwa ikaitwa TAX dakwa speed hadi gerezani,kufika gerezani nikajifanya

napumua haaaaaa huku nakoromaa,ndio ikawa pona yangu ila bila ile tekniki Ningefia pale walahi vile...
🤣🤣🤣🤣🤣 Mbavu zangu mie
 
3.Kuvua bahari ya upande wa sahare Tanga

Nilikuwa nina shida na nauli nikimbie Lusanga kuna mishe mchizi alinisanua nikapata kazi ya kuvua mwana aliniunga tu picha linaanza jioni ile nikatokea na ka t-shirt kangu manga nyepesi maana tulienda vua maji ya usiku [emoji3] wale wadigo na Wapemba wa ile mashua sijui boat whatever the case .. walikuwa wanacheka

Niligundua kwa nini wanacheka tupo katika ya bahari ule upepo wa baridi niliokuwa napigiwa nao plus yale maji yakikurukia ushapata picha

Kwa nini nilijuta kuna kitu wenyeji wanaita sijui bawa la mvua wataalamu mtaiweka sawa ile maji yanaongezeka yanapanda juu kwa kasi yanavuka hadi kingo za beach ambapo watu wanakaa kunakuwa na maji yanasogea hio ishu ilitukutia usiku plus mawimbi maji yakawa yanaingia kwenye chombo chetu tuna kazi ya kuyatoa na visado boti linapigwa pushi na mawimbi mara chemli imeanguka imepasuka mpemba mmoja akanambia "wajua kuogelea weye ..mimi siokoi ntu nanusuru roho yangu mie " wengine wanakazi ya kutoa maji na visado huku wakisema "shahada" yaani kwa imani ya dini ya kiislamu unaenda peponi ukifa kama utaisema

Nilisema sirudii tena [emoji1787][emoji1787]
😀😀😀😀umenikumbusha cku nimeeñda kuvua dagaa ziwa Victoria, aisee ulipga upepo mkali huku wanaita MSOKE sema kweli nilipga magoti kutubu dhambi zangu. Ila kesho yake nilirudi make Sikh hiyo tulitoka marundo

Majini paskie tu
 
Back
Top Bottom