Kazi nilizowahi zifanya na zikanishinda kwenye utafutaji

Mkuu hii ya ujenzi bora kwa waswahili wenzetu kwa mhindi au mchina wanaua mzee kaI mlima malipp kijiko
Asee ni kazi ngumu , hiyo site kuna dude fulani hivi linakua linazunguka mnamwaga mle mchanga ,kokoto , cement na maji !! Dude linamix huku linamwaga zege ! Halafu msimamizi mkali kichizi nilipangwa kwenye kumimina mchanga inabidi niweke ndoo nne zile kubwa za litre 20!! Aseee hiyo siku ndo nolijua mchanga ni mzito ! Nikasema ngoja nibadilishane na mwana maana sikuendana nao speed nikahamia kwenye kokoto inabidi ziingie ndoo saba kila awamu speed nako ikawa ndogo !!! Nikahamia kwenye kuchota maji ! Daah site kipengele
 
Dah mkuu[emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Mkuu ilikua wapi hiyo mimi siachi uwa ni kazi ndogo sana kuchota na kumwaga tu sema kwa mwenye kinyaa awezi.
 
Kila upande ni shida. Sasa kuna zege lile mnakoroga wenyewe noma na nusu. Sema zege za waswahili wenzetu bora malipo yana ridhisha
 
Ulinzi umesema mgumu katika kulinda usiku , si hivyo tu mgumu kwenye mashariti ya kazi , usiku ni mda wa kulala, mda wa kufanya kazi , malipo hafifu hafu unavyolinda ni vitu vya gharama, mshahara wako hata miaka kumi haulipi, ulinzi hauko fea
 
Daah site kipengele
kila kazi unayogusa yamoto 😂 , niliwahi omba kazi site ya kufyatua tofali asubuhi mapema 11 nimefika pale nikamkuta boss wa hapo akaniambia kazi iliyopo labda upange vibao vya tofali.

nikaona vibao vya tofali mbona vidogo dogo tu kazi simple hii, akaniambia malipo hapa ni 5000 ila kula ni hapa hapa..

nkajisemea kimoyo moyo,mimi vibao hivi ndio nipange hadi muda wa kula,basi kazi ikaanza,Bwana Bwana weee, nilipanga vile vibao tangia 12 asubuhi hadi 1 usiku mgao wa vijana wa tofali na mimi nikapewa changu,

jamaa akanisifia eti nimefanya vizuri kesho niwahi tena,Kimoyo moyo nikamwambia "aaah subutuuuu" nani aje na kesho... ndio sikurudi tena pale...
 
Nilikimbia kazi ya kushusha mizigo kwenye store ya kiwanda fulani.

Kwenye hicho kiwanda Kuna kitengo kinaitwa finance Sasa walikuwa wamebandika tangazo wanahitaji Kuajiri vijana 10 so kutokana na jina la kitengo nikashawishika kuomba kuajiriwa Kwa Imani kuwa kazi zitazokuwa zinafanyika pale zitarelate na mambo ya finance ili kujiakikishia kuwa napata hiyo nafasi nikaenda kuoongea na mshua fulani ili hakikishe connection hainipiti pembeni.

Picha linaanza tunapelekwa general store ya hiyo kampuni Kwa hiyo sisi ndio tutakuwa full responsible Kushusha mizigo yote inayoingia kwenye hiyo kampuni na kweli kampuni inapokea mizigo sio kitoto kuanzia cement, chokaa, Nondo, mabati, mbolea, dawa za kilimo in short ni general store haswa.

Sasa task yetu ya kwanza ilikuwa Kushusha mbolea Toka kwenye scania mzee nilikomaa Kushusha tumemaliza tunaona scania nyingine inaingia zile za kufuta na kontena mbili ilikuwa na cement wahuni wakaniambia Mimi ndio niwe nawatishwa aisee niliona Bora kubeba kuliko kuwatishwa sababu walikuwa wako chapu kinoma nikaomba kubeba wakakubali tunakaribia kumaliza tunaona nje ya Fensi scania nyingine inakuja na yenyewe cement nikaanza kugiveup wahuni wananiambia Kuna siku magari yanakuwa hayaji Kwa hiyo zipo siku tutarelax.

Nilipiga Ile kazi Kwa siku tatu sikuchukua malipo kwani walikuwa wanalipa baada ya wiki mbili na malipo was 3500 per day bila ya kujali uzito wa kazi wa siku husika.
 
Ulinzi umesema mgumu katika kulinda usiku , si hivyo tu mgumu kwenye mashariti ya kazi , usiku ni mda wa kulala, mda wa kufanya kazi , malipo hafifu hafu unavyolinda ni vitu vya gharama, mshahara wako hata miaka kumi haulipi, ulinzi hauko fea
Kampuni za ulinzi zina wanyonya sana walinzi,ndio mana sipo tayari kulindiwa na kampuni

Mishahara ni midogo mno halafu vitu vinavyolindwa vinamshawishi hata mlinzi mwenyewe

awe mwizi,yani ukilindiwa na kampuni usipokua makini ukajiachia unaibiwa na mlinzi wao huyo huyo

Makampun haya yanatesa watu mno,mtu ukiwa na tamaa mbona badala ya kulinda unaiba tuu ujilipe.
 
iyo kazi simpo. Ishu labda iwe umbali mpaka kuumwaga mzigo.
 
Halafu kuna mdada somewhere amekaa kaomba 10k katumiwa

anaona haitoshi kaitisha na ya kutolea,lediiiiiiiiiiiz nawambia Mbingu

mtaishia isoma kwenye bible,men wako na suffering si kawaida shauri lenu
 
iyo kazi simpo. Ishu labda iwe umbali mpaka kuumwaga mzigo.
we bwana wewe,ukiskia mtu anafanya kazi flani kisa inaonekana ndogo unahsi simple sana eeeh

Mkuu kuna kazi unapewa kiwandani,kazi ya kuosha tu chupa mjomba ukskia kuosha chupa

unahsi simpooooo, try and see uje utusimulie... Kitu chochote mtu anachotoa pesa ili ukifanye

jiulize mara mbili mbili "why" kaamua akulipe ufanye,ingekua rahisi angefanya mwenyewe mkuu.
 
Nimecheka sana loooh [emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]
 
Kuna mtu aliniambia kazi za kiwandani zinalipa sana,siku hiyo nimewahi kiwandani kufika nikasimama kwenye foleni yani ile foleni tu ilinifanya niachane na ile kazi nikatafute mishe zingine za kufanya.
😂😂hiyo ilinikuta mwanza kiwanda kimoja cha vinywaji eti utaratibu wa kuajiri ni unaamka asubuhi unaenda kusimama getini kama mbwa(nyomi la kufa mtu) halafu anatoka mtu huko ndani anapoint anaowataka then mliobaki mnaambiwa mjaribu kesho, ...malipo 6000 per day
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…